Kwa hiyo kwa mujibu wako wewe unaona kuwa utu na heshima ya raisi vina thamani zaidi ya Nsia kwa vile tu raisi kachaguliwa na watu wengi?
Well, mimi kama Ngabu ninastahili heshima kama binadamu mwingine yeyote yule regardless ya cheo au nafasi yoyote aliyonayo mtu mwingine. Heshima yangu, utu, na ubinadamu wangu ni sawasawa kabia na ule wa Kikwete, Obama, Malkia Elizabeth, Nsia, Aunty Mudy, Masanilo, Juma Kilaza na wengineo. I am not above or under anyone.
Kinachoniudhi mimi ni hii outrage wanayoionyesha baadhi ya watu humu kwa vile tu aliyefanyiwa mbaya ni raisi. Ebo! Vipi leo muonyeshe kukasirishwa hivi wakati kila siku raia wa kawaida wanabandikwa huko utamu.
Inakuwa kama vile heshima ya raisi ni bora zaidi kuliko heshima ya watu wengine. Watu mbona hamuwaki hivi muonapo picha za akina Nsia na wengineo? Acheni unafiki wenu bana.
Sitaki ligi lakini nadhani hapo tutakubaliana kupingana bila kupigana. Heshima ya mwenye mamlaka ya madaraka haiizidi heshima yangu mimi kama raia wa kawaida ninayestahili kutendewa kwa heshima na kuwatendea kwa heshima binadamu wengine kama mimi.
Hata thread zetu nyingi hapa JF kwa tabaka kubwa tu la waTZ zinaonekana ni za uchochezi na zilizovuka mipaka, Muulize Dr. Nchimbi, Mh. Masha, n.k. JF Nayo Ifungwe?
Alafu ukiangalie trend ya ze Utamu ilikuwa inajikusanyia mashabiki na walikuwa wanatengeneza pass wafike golini, na golini ndio huyo waliyemfikia leo. Nasita kusema zeUtamu watakuwa na ufadhiri wa maadui zake mkuu wa kaya kisiasa, waliorecruit vijana wenye vipaji na akili kwa ajili ya kuwaisaidia kuelekea 2010. Ngoja tuone.
Juzi Juzi hapa ilipotolewa picha ya Kagisi wengi hapa mkajifanya mna data za kutuaminisha kuwa mwisho wa ile web umefika, matokeo yake imeboreshwa mara dufu, hata sisi tuwe makini kabla hatujatoa utabiri wetu tunapoteza credibility zetu.
Kabisa kabisa Raisi ni mamlaka mazee, huwezi linganisha NN na JK labda kama unataka ligi!
Nsia na JK wote ni binadamu sawa lakini Jk ni kiongozi wa nchi tena ni alama ya taifa letu, mara kadhaa huwakilisha taifa letu kwenye mikutano ya dunia sijasikia nsia akifanya hivyo, hata hivyo kuna heshima anapewa rais hata katika sheria hawezi kufunguliwa mashtaka ya jinai akiwa bado ni rais. Sifurahishwi na kitendo cha kubandikwa picha za nsia lakini naogopa inapofikia zinabandikwa picha za rais.
Nimepata picha zake, nimejua alisoma wapi na lini na kwa sasa anafanya kazi. Sina sababu ya kutishia sababu sioni sababu ya kufanya hivyo. Nimeomba aache upuzi wake vinginevyo nitamweka wazi hapa jf sina utani na uchafu kwani siwezi kukubali uchafu.
Kinachoniudhi mimi ni hii outrage wanayoionyesha baadhi ya watu humu kwa vile tu aliyefanyiwa mbaya ni raisi. Ebo! Vipi leo muonyeshe kukasirishwa hivi wakati kila siku raia wa kawaida wanabandikwa huko utamu.
Inakuwa kama vile heshima ya raisi ni bora zaidi kuliko heshima ya watu wengine. Watu mbona hamuwaki hivi muonapo picha za akina Nsia na wengineo? Acheni unafiki wenu bana.
Kinachonichukiza mimi ni huu unafiki wa kuthamini watu wengine na kutowathamini wengine. Sikatai kuwa hiyo picha ni repulsive lakini kwa mtu yeyote mwenye akili atagundua kuwa ni ya kutengeneza.
Acheni double standards na karibuni ktk karne ya 21!
Nimeshaona picha ya Bush akimdinya Osama. Nimeshaona picha ya Mama Clinton akiigiza kwenye porno. Bill Clinton ndio usiseme kabisaaa. Sarah Palin tayari watu wameshamtengenea porno. Hawa nao wote ni viongozi wanaowakilisha taifa lao.
Kutengeneza picha kama hiyo si kazi ngumu kama unajua kutumia photoshop. Hata mimi ninaweza kuzitengeneza picha kama hizo halafu nikazisambaza kwenye barua pepe.
Kinachonichukiza mimi ni huu unafiki wa kuthamini watu wengine na kutowathamini wengine. Sikatai kuwa hiyo picha ni repulsive lakini kwa mtu yeyote mwenye akili atagundua kuwa ni ya kutengeneza.
Acheni double standards na karibuni ktk karne ya 21!
Please close th e blog outright. Hata kama ungekuwa ukweli haingii akilini kwa mtu mwenye akili timamu kupiga au kuonyesha uozo wa nanmna hii. HUYU ZEUTAMU ACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA MARA MOJA. hivi hamna IT wa kuiblock nchi hii??
16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.
naikumbuka ile mwanakijiji na mwafrika wa kike walisema wana picha ya namna hio.....ndio maana nasema tuanze sisis wenyewe hapa JF......
inasikitisha sana.i wish ningewajua watu wanaohost hiyo site.wangenitambua aisee
wee rudi kwenu "Nyarugusu" ndio utajua tofauti yako na "Rais".....kwi kwi kwi kwi....