Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Je tuhahitaji tena Ze Utamu?

Status
Not open for further replies.
Kwa kweli picha ile imekifu hapa umevuka mipaka ya utamaduni wetu wa kitanzania. Haifai haifai hata kama una lako rohoni ungetumia njia nyingine lakini sio hiyo.

Unajua mara nyingi muuaji anapofanya kitendo cha kumuua mwenzie na pindi akimaliza na kuingalia maiti huwa roho inamsuta na huamua kujiua mwenyewe, nadhani aliyefanya hili yampasa ajisute na ikiwezekana ajiweke kamba au awaombe watanzania wote msamaha

Hapa umepitiliza yule ni Presidaa tunamheshimu hata kama ana mapungufu ni mheshimiwa wetu stop!!!
 
The thread of the Day!!!! But does not worth our precious time. It is enough now!! Please mods, get rid of it.

Currently Active Users Viewing This Thread: 120 (46 members and 74 guests)
Maane, amagoma, Baba_Enock, Chada, Chakaza, chavala, Che Kalizozele, chrispine, cool girl, CottonEyeJoe, dmaujanja1, Domo Kaya, Faith, Field Marshall ES, Giroy, Hofstede, Ibrah, Ikena, Jaylee, Kang, Kidatu, Kijakazi, Killuminati, kisale, Kufakunoga, KYACHAKICHE, LazyDog, Magehema, Magobe T, Mbu, mchizi, mduduwashawasha, mmasaihalisi, mshiiri, Mtu B, Mutensa, mziwanda, Ngosha123, Nyani Ngabu, Sem, Sikonge, Son of Alaska, Tabu, TreasureFred, Tshala

Even with you to be able to post this post you have viewed first. Haven't you?
 
Hivi polisi wanaposema ze utamu wanadhalilisha viongozi ina maana hizo picha zilizowekwa kweli ni za jk ?

Mimi naona wanaiongezea ze utamu umaarufu wasiostahili.
 
what I think, with the freedom of expression, we should distinguish things based on sensitivity. What has appeared recently wil prompt banning of that very freedom, the hunt down will start and always the state will win, no doubt. President is an institution, and not a person. So the state is at liberty to act, though that is against is civil liberty. Whether that is applicable in Tz remains to be debated. but the pic was really sensitive as far as the STATE of Tz is concerned.
 
kwa mara ya kwanza nimeingia utamu nikaiona hiyo picha, nimetapika hadi nikapata kizunguzungu,i am speechless!
 
Hata kama hiyo picha ni ya "kutunga" - lengo ni kumwanika Mkuu uchi mbele ya dunia! Kwa wenye kuamini, nadhani hakuna dhambi kubwa kama ya kuangalia utupu wa babako! Huyo aliyeweka hii picha kwenye hiyo site basi ajue amemuweka "baba" uchi mbele ya kadamnasi na asubiri adhabu kubwa sana siku ya kiama kama hatatubu na kututaka radhi watanzania wote.
Alaaniwe!
 
Nakubaliana na Mzee mwanakijiji; hatuwezi kuwa na double standards katika maadili ya jamii yetu. Matusi ni matusi akitukanwa mtu mdogo au mtu mkubwa yote ni matusi ;hayastahili kuvumiliwa katika jamii yeyote iliyostaarabika. Hii blog ya utamu haitusaidii lolote katika kujenga jamii yenye maadili mema na hata kama ndio uhuru wa habari uhuru wa aina hii hautufai sisi Watanzania.Utamu has overstepped the boundaries of respect to us all in this country, I call upon the powers that be to take stern measures against all the culprits.
 
Hii blog ya utamu haitusaidii lolote katika kujenga jamii yenye maadili mema na hata kama ndio uhuru wa habari uhuru wa aina hii hautufai sisi Watanzania.Utamu has overstepped the boundaries of respect to us all in this country, I call upon the powers that be to take stern measures against all the culprits.


This is a testimony of how depraved our society has become.
 
Niliwahi kusema hapa before ya kwamba uhuru nao una mipaka yake....
Kwanza yule ni mtu mzima, pili ni mume wa mtu, tatu kuna raia wa Tanzania wanamwita baba, nne kuna watu na akili zao timamu tu wanamwita mjomba, baba mdogo, baba mkubwa n.k......na mwisho ni rais wa nchi yangu. Kuna vitu vingi sana napingana nae kama kiongozi wa nchi niipendayo nikiamua kuviorodhesha hapa Invisible atanipigia kelele najaza server lake, lakini kuna mstari ambao haupaswi kuvukwa, nao ni personal attacks.
Kama unaona una muda mwingi sana mikononi na umeshanunua au umedownload somewhere photoshop software yako halafu huna cha kufanya, go outside for a walk; beba vyuma, au fanya lolote kwa ajili ya maendeleo yako na walioko karibu yako, lakini sio kejeli, udhalilishaji na ujuha wa kiasi kile. Mimi naungana na jeshi la polisi katika kumsaka huyo aliyefanya kituko kile......Mimi Nikikung'amua tu...naku-turn in....😡😡
 
Naona kuna POST zimeshafika kalibia 300 na kitu je kuna action yoyote imechukuliwa juu ya hili swala au tunaongea point lakini vitendo 0????
 
Naona kuna POST zimeshafika kalibia 300 na kitu je kuna action yoyote imechukuliwa juu ya hili swala au tunaongea point lakini vitendo 0????

Wametoa picha ya mheshimiwa raisi kule utamu japo bado inaendelea na mambo yake.
Pia jeshi la polisi linawatafuta wamiliki wa hiyo blogu.
 
Niliwahi kusema hapa before ya kwamba uhuru nao una mipaka yake....
Kwanza yule ni mtu mzima, pili ni mume wa mtu, tatu kuna raia wa Tanzania wanamwita baba, nne kuna watu na akili zao timamu tu wanamwita mjomba, baba mdogo, baba mkubwa n.k......na mwisho ni rais wa nchi yangu. Kuna vitu vingi sana napingana nae kama kiongozi wa nchi niipendayo nikiamua kuviorodhesha hapa Invisible atanipigia kelele najaza server lake, lakini kuna mstari ambao haupaswi kuvukwa, nao ni personal attacks.
Kama unaona una muda mwingi sana mikononi na umeshanunua au umedownload somewhere photoshop software yako halafu huna cha kufanya, go outside for a walk; beba vyuma, au fanya lolote kwa ajili ya maendeleo yako na walioko karibu yako, lakini sio kejeli, udhalilishaji na ujuha wa kiasi kile. Mimi naungana na jeshi la polisi katika kumsaka huyo aliyefanya kituko kile......Mimi Nikikung'amua tu...naku-turn in....😡😡



Mkuu upo sawa kabisa lakini hayo ndio matokeo ya kuwafanya watu wajinga bila kufahamu mjinga ana be have vipi
HIYO NI KAMA SUICIDE BOMBER AND MESAGE SENT NOW
Sasa hao polisi wataanza kuwashughulikia wanaofahamika kama Mzee mwanakijiji, michuzu na wengineo
Utamu kila kitu fake hivyo ni vigumu sana kupatikana
 
Nakubaliana na Mzee mwanakijiji; hatuwezi kuwa na double standards katika maadili ya jamii yetu. Matusi ni matusi akitukanwa mtu mdogo au mtu mkubwa yote ni matusi ;hayastahili kuvumiliwa katika jamii yeyote iliyostaarabika.

Kuna wengine wanaojiona wao ni duni mbele ya raisi kwa vile yeye ni raisi na wao ni raia wa kawaida tu. Binafsi naona raisi ni mtu (binadamu) wa kawaida tu. Heshima anayostahili kupewa kama binadamu na mimi naistahili. Kwa standard yao wao wanaona ni sawa kwa watu wa kawaida kubandikwa huko utamu lakini inapokuja kwa raisi...oooh noooo...wanasema raisi si sawa na watu wengine. Halafu kila siku watu tunakuna vichwa na kujiuliza kwa nini sisi Waafrika tulitawaliwa na tunaendelea kubaguliwa....
 
Uchunguzi wangu wa haraka haraka inanionesha huyu jamaa anayejiita zeutamu
anapatika USA, state ni texas na city ni Houston.
Host IP address ni: 174.132.156.66

IP postcode: 77002
IP address latitude: 29.7523
IP address longtude: -95.3670

Tafadahali ni vyema aache upuuzi na uchafu wake mara moja kwani tunaweza kuanika mpaka jina lake kamili, alisoma wapi na hata ikiwezekana picha zake pamoja na kwamba tulisoma computer migombani.

Vema sana Mkuu Kidatu, tatizo la vijana wetu wengine(nasema vijana maana hiki kitu hakiwezi kufanywa na mtu mzima mwenye hadhi ya kusimama hadharani) malezi yao yana walakin mkubwa sana.
Si ajabu kijana kama huyu akaweka hata picha za baba yake na mama yake katika mfano huo wa tovuti yao.
Ni kitendo cha kulaaniwa, ila kulaanai hakutoshi waanikwe hadharani. Hiyo ni adhabu tosha ili na wazazi wao wapate kujua wanacho kifanya huko US.Cha kufanya ni kuwaanika majina yao na walipo pamoja na ndugu zao waliowapeleka huko.Lawama lazima ziende kwao kwa kushindwa kwao kuwalea watoto wao ipasavyo..
 
Jeshi la polisi lieajiri ma-expert wangapi wa computers? lina wataalamu wangapi tunaoweza kusema wanaweza kupambana na hali hii?? at least kujaribu hata ku-track, maana kusubiri matokeo ni hatari!

kesho wataweka zingine tena!!!!!
 
Wana JF,

Wengi ni majeruhi wa the utamu. Tumelaani kwa nguvu zote kwa mkuu wa nchi kuwekwa picha yake (bahati mbaya hiyo picha sijaiona) na sababu za msingi za kulaani hii blog ni kwamba inakiuka maadili ya watanzania. Labda kwa faida yangu na wengine wasiojua kama mimi maadili ya watanzania ni yapi? Je kuna literature yoyote ambayo inaweza kutumiwa kama reference tunapozungumzia maadili ya Watanzania?. Je mkuu wa nchi hapashwi kujadiliwa negatively kwenye mitandao? Mbona hapa JF JK amesemwa sana tu kwa mapungufu kibao both kwenye utendaji wake kama Rais na hata ushikaji wake na baadhi ya watu ambayo ki msingi ni masuala binafsi?

Naomba kupendekeza kwamba wale wote wanaoukubali uongozi wa aina yoyote kwenye nchi ni wakati wao sasa kuhakikisha wanakuwa mfano wa kuigwa katika jamii badala ya kujihusisha na vitendo visivyofaa kama vile kuwa na nyumba ndogo na kuchukua machangudoa mitaani. Viongozi watakaoanikwa kwa kukutwa na mambo haya sitawaonea huruma hata kidogo wakitundikwa kwenye mitandao.

Tiba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom