Je tatizo ni watu au mfumo?

Je tatizo ni watu au mfumo?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
17,287
Reaction score
40,946
Hivi ni kweli ni rahisi kulalamika ukiwa nje ya mfumo eti kwa sababu wewe si mnufaika wa moja kwa moja?

Kwa mfano, unaweza kusema mtu fulani ni fisadi. Lakini je, ukipewa nafasi ya huyo mtu, una uhakika kwamba na wewe hutageuka kuwa fisadi?

Mfano👇

Mtu asiye na kipato anaweza kuapa kwamba yeye hawezi kununua magari ya gharama kubwa kwa sababu anaona ni anasa na ni matumizi ya kupita kiasi

Lakini nadhani wakati huo anakuwa hana uwezo wa kifedha, hivyo huwaona wanaofanya hivyo kama wanafuja mali

Je, ikitokea siku pesa zikamjia, bado atabaki na msimamo huo, au atataka kubebwa kichwani na hataki hata kukanyaga ardhi?

Hii ina maana gani?
Je, mara nyingi watu hulalamika kwa sababu wako nje ya mfumo na hawanufaiki nao?

Mwisho kabisa, kama ni kweli kwamba binadamu anaweza kubadilika anapoingia kwenye mfumo wa madaraka au kunufaika nao, ni mfumo gani imara unapaswa kuwekwa ili kuzuia tabia ya (kulamba asali? )

Kama tatizo ni mfumo Je

Mfumo gani unaweza kuwafanya viongozi wasijisahau wanapopewa madaraka na wasije wakafanya yale yale waliyokuwa wanawakosoa waliowatangulia?

NB: Sina chama chochote
Lakini napenda nchi yenye ustawi bora
ShesRise_1 🤚
 
Nafasi na pesa huongeza mwanya wa tabia za ndani kujitokeza. Kama mtu ana nidhamu, itaonekana zaidi; kama hana, pia itaonekana zaidi .
Ukipewa mamlaka au fedha,

1. unapata uhuru zaidi wa kuchagua unachotaka kufanya.​
2. Uhuru huo huondoa vikwazo vilivyokuwa vinakuzuia kuonyesha hasira, ubinafsi, ukarimu, au nidhamu yako.​
Katika nchi yetu kama wananchi tuna wajibu mkubwa wa kusimamia, kuuliza, na kudai uwajibikaji wa viongozi wetu. Hili ni muhimu kwa sababu sisi ndio waajiri halisi wa serikali na viongozi wanapaswa kufanya kazi kwa maslahi yetu . Binafsi nafikiri mambo yafuatayo yanaweza kuwa na msaada.​
1. Katiba na sheria zenye mipaka wazi ya madaraka, ili kiongozi asijione juu ya sheria​
2. Muda maalum wa uongozi na ukomo wa mihula, ili mtu asishikilie mamlaka kwa muda mrefu​
3.Taasisi huru za usimamizi na kupambana na rushwa, ili matumizi mabaya ya madaraka yagundulike mapema​
4.Vyombo huru vya habari na wananchi wenye sauti, ili viongozi waendelee kukumbushwa kwamba wanaangaliwa na nchi ni yetu sote.​
 
Asante sana mkuu🙏
1. Katiba na sheria zenye mipaka wazi ya madaraka, ili kiongozi asijione juu ya sheria​
Hivi hili la katiba limefikia wapi?
2. Muda maalum wa uongozi na ukomo wa mihula, ili mtu asishikilie mamlaka kwa muda mrefu​
Myaka kumi ni mingi?
Inafaa ipunguzwe?
Mfano badala ya myaka 5 kwa muhula mmoja iwe myaka mi ngapi?
3.Taasisi huru za usimamizi na kupambana na rushwa, ili matumizi mabaya ya madaraka yagundulike mapema​
Sawa
4.Vyombo huru vya habari na wananchi wenye sauti, ili viongozi waendelee kukumbushwa kwamba wanaangaliwa na nchi ni yetu sote.​
Shukrani sana karibu tena🙏🙏
 
Kwani walioweza kama Norway au Denmark walifanyaje? Ni kujisahau tu.
Miundombinu zikiboreshwa vizuri kuna haja gani ya kulimbikiza mali ya wizi?
Kwahiyo tuboreshe miundo mbinu kwanza okay
karibu tena mkuu
 
Kuna nadharia inaitwa the lucifer effect, hii nadharia inasema kuwa watu wema pia wanaweza kutenda maovu kama watawekwa kwenye mfumo au mazingira yanayoruhusu au kuhimiza huo uovu kutokea.

Mara nyingi huwa tunadhani ufisadi ni tabia ya mtu lakini ukweli ni kwamba madaraka yenyewe huwa yana poison fulani hivi, mtu anapoingia kwenye mfumo wenye mianya ya kufanya ufisadi lazima ataanza kuona fursa za kufanya ufisadi badala ya uwajibikaji.

Fuatilia vijana wanaopiga kelele mitandaoni kuhusu usawa na uadilifu, walio wengi inapotokea nafasi akateuliwa kuwa mkurugenzi au mbunge, wengi wao huwa wanaanza kufikiria kujijenga kwanza, hapa tuna mifano hai ya viongozi wengi tu, na hayo yanatokea kwa sababu mfumo unawapa psychological permission ya kufanya madudu.

Iko hivi watu wengi hawachukii ufisadi isipokuwa huwa wanachukia kutokuingizwa kwenye mzunguko wa ufisadi, hii ndio sababu kwanini huo mfumo una shamiri, ukimpa nafasi yule anayelalamika naye ataanza kutafuta namna ya kufanya upigaji ili afidie muda aliopoteza akiwa anataabika mtaani, hii life vengeance wapo nayo watu wengi sana.

Tunahitaji institutional constraints, mfumo imara ni ule unaomfanya hata mtu muovu ashindwe kutenda maovu.

Kuhitimisha tu, tatizo nilionalo mimi ni mzunguko wa kijamii, sisi kama jamii tumetengeneza mfumo ambapo mafanikio ya mtu yanapimwa kwa jinsi anavyoweza kuhonga, kubeba watu, na kuishi maisha ya kifahari, tunapomlaumu fisadi hapa tunasahau kuwa yeye ni zao la societal expectations zetu,
kiongozi hawezi kujisahau kama raia wanamfuatilia kila hatua, ufisadi ni matokeo ya collective silence ya raia wanaosubiri zamu yao ifike na wao waingie kwenye mfumo ili walambe asali.
 
Yes nakubari yes yes

Nakubari

Exactly

Brother 🫡🫡♥️♥️♥️
 
Wewe unaonekana ni mtu Mzalendo sana, but life in general is a bitch..

People are zombies they don't care. Hasa kwa huku kwenye ardhi ya laana.

If you really want to bring change, start on a family level, democracy is but an illusion matajiri wanafanya Ufuska, ili wasilipe kodi.

Watu wenye nia njema don't survive, si ulimwona magufuli.. A perfect example..

Human nature iko egocentric na hakuna kitu utafanya. People are users, wafanyie wema but utaishia kulia peke yako ukifulia.

It is what it is. Love yourself first. Fanya kile uwezacho kwa uwezo wako.. Watu watakao Badilika kwa kukuona wewe ni zawadi tosha ila kubadili watu is a zero sum game
 
Wewe unaonekana ni mtu Mzalendo sana, but life in general is a bitch..

People are zombies they don't care. Hasa kwa huku kwenye ardhi ya laana.

If you really want to bring change, start on a family level, democracy is but an illusion matajiri wanafanya Ufuska, ili wasilipe kodi.

Watu wenye nia njema don't survive, si ulimwona magufuli.. A perfect example..

Human nature iko egocentric na hakuna kitu utafanya. People are users, wafanyie wema but utaishia kulia peke yako ukifulia.

It is what it is. Love yourself first. Fanya kile uwezacho kwa uwezo wako.. Watu watakao Badilika kwa kukuona wewe ni zawadi tosha
Shukrani karibu tena
ila kubadili watu is a zero sum game
Hakuna anaetaka kubadili watu
Ila tutamani kuona mifumo ikibalishwa
Hapo tayari kila kitu kitajiendesha
 
Shukrani karibu tena

Hakuna anaetaka kubadili watu
Ila tutamani kuona mifumo ikibalishwa
Hapo tayari kila kitu kitajiendesha
Mfumo ndo watu wenyewe.
It takes a generation kama sio hata vizazi zi3 kuendelea.. Swala la muungano tu si unaona tunavyo tapatapa?
 
Hivi ni kweli ni rahisi kulalamika ukiwa nje ya mfumo eti kwa sababu wewe si mnufaika wa moja kwa moja?

Kwa mfano, unaweza kusema mtu fulani ni fisadi. Lakini je, ukipewa nafasi ya huyo mtu, una uhakika kwamba na wewe hutageuka kuwa fisadi?

Mfano👇

Mtu asiye na kipato anaweza kuapa kwamba yeye hawezi kununua magari ya gharama kubwa kwa sababu anaona ni anasa na ni matumizi ya kupita kiasi

Lakini nadhani wakati huo anakuwa hana uwezo wa kifedha, hivyo huwaona wanaofanya hivyo kama wanafuja mali

Je, ikitokea siku pesa zikamjia, bado atabaki na msimamo huo, au atataka kubebwa kichwani na hataki hata kukanyaga ardhi?

Hii ina maana gani?
Je, mara nyingi watu hulalamika kwa sababu wako nje ya mfumo na hawanufaiki nao?

Mwisho kabisa, kama ni kweli kwamba binadamu anaweza kubadilika anapoingia kwenye mfumo wa madaraka au kunufaika nao, ni mfumo gani imara unapaswa kuwekwa ili kuzuia tabia ya (kulamba asali? )

Kama tatizo ni mfumo Je

Mfumo gani unaweza kuwafanya viongozi wasijisahau wanapopewa madaraka na wasije wakafanya yale yale waliyokuwa wanawakosoa waliowatangulia?

NB: Sina chama chochote
Lakini napenda nchi yenye ustawi bora
ShesRise_1 🤚
Ukiwa na Pesa utamiliki Kila kitu ulichokitamini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom