Je, Tanzania wabunge wetu wanajua majukumu yao? Je, wana uwezo wa hayo majukumu?

ryan riz

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
422
675
1. Hakuna wazo jipya lolote ambalo wamewahi kutoa lenye tija na manufaa kwa wananchi.

2. Kila kinacholetwa na serikali hupita bila kikwazo chochote hata kama hakina manufaa.

3. Kwenye suala la kuongeza makusanyo ya kodi hakuwa wazo lenye afya au mantiki walilowahi pendekeza zaidi kuiachia serikali na wao kuja tu kupitisha.

4. Hakuna wazo bunifu lolote kwenye kuinua elimu yetu na pia namna nzuri ya kuindesha elimu.

5. Hakuna wazo bunifu kwenye kuvumbua,kubuni namna ya kukuza sekta za uchumi zaidi kuiacha serikali ifanye kila kitu wao waje kupitisha au kulaumu.

6 ...

JUKUMU LAO KUBWA WANALOLIWEZA NI KUPITISHA KILA KITU KILICHOLETWA BUNGENI.

NB: Asilimia 2 ya wabunge ambao angalau huchangia vya maana ni wale wale hujurudia sasa kwenye mambo ya maana sasa sijui hawa wengine bungeni walienda kwa ajili ya nini?
 
Majukumu yao yapo kwenye kile walichonadi kwa wananchi

Ilani♥️🇹🇿💪
 
Zaidi ya 50% ya wabunge wapo kwa maslahi yao, yaani kwao ile ni ajira tu na sio wajibu.
 
Back
Top Bottom