Wabunge wa wasiojua majukumu yao ya kazi wapumzike

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Wabunge wasiojua majukumu yao yaani kazi kupiga makofi na kupitisha makablasha bila kusoma wanapitisha nini wabunge waasi kwa wananchi wanaofunga ndoa na serikali kuwabagaza wananchi.

Ninyi wabunge njoo mniambie majukumu yenu Je ni kutetea serikali? Mnajua maana ya uakilishi? Je, sheria mnazopitisha ni kwaajili ya nani? Rejea sheria ya mistu Na.14-2002 inavyoumiza mwananchi, nakumbuka Spika Ndugai aliwahikusema; "Sijui sheria hizi tulizipitisha tukiwa tumelewa?"

Ebu fikiri mimi nipande mti niupalilie, niutunze, nipambane na moto unaochomwa hovyo, ukikua niende kununua kibali cha kuukata, nikimaliza nikanunue kibali cha kusafirisha, kama ni mbao nataka kujenga nikanunue kibali kama ni kuni ninunue kibali kwa Mkurugenzi hata hajui mateso niliyopitia hadi mti umekuwa wakati huo huo ardhi nailipia hivi, sisi tunamilki nini?

Halafu wabunge kwa unafiki wakishapigwa nao wanarudi kwetu kulalamika wakati sheria walipitisha kwa miswada ya dharula mpaka hapo unaona madhara ya kuwa na wabunge makasuku?

Mimi sitaki mbunge mfadhili, sitaki aninunulie hata maji ya 500 sitaki, ninachotaka aende bungeni anitetee, awasilishe mawazo yangu aniambie serikali kwamba wanataka nchi iendeshwe hivi, kodi hii hawaitaki wanataka zahanati, sio tunataka zahanati wanatujengea josho wakati mifugo hatuna, tunataka soko wanatujengea zahanati wakati madawa hakuna.

Nani alikwambia huduma za afya ni majengo tu! Majengo hayawezi kumtibu mtu tunataka vipimo na madawa acheni kuchezea afya zetu, tunataka maji wanatujengea shule wakati muda mwingi watoto wamautumia kutafuta maji. Hii ndiyo kazi ya mbunge sio ufadhili.

Safari hii wabunge wa Mwendokasi wote hatuwataki waende wakajiajiri kama ambavyo wamekuwa wakiwambia vijana wajiajili kwakuwa tayari mtaji wanao waende wakaanzishe mashamba kilimo na ufugaji, wakafanye biashara tuanataka kuona wakilipa kodi maana wao ni mabingwa wa kutunga sheria ngumu za kodi bila kuangalia mazingira ya biashara alafu baada ya miaka 20 tutawarudisha bungeni akili zitakuwa zimeishakaa sawa ili waondoe sheria kandamizi japo najua wengi watakuwa wamepoteza uwezo wao wa kuamua na kufikiri.

Hawa wabunge wanawaona wananchi hawawezi kufikiri vizuri waache tabia ya kutoa ahadi za kujenga miundo mbinu hiyo ni kazi ya serikali lazima itajenga wao wapambane kuinua uchumi wa wananchi wakulima ni masikini, wawatafutie mitaji ili waongeze thamani ya mazao yao na masoko, vijana hawana ajira badala ya kuibana serikali itoe mikopo vijana waanzishe viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani na serikali isaidie kutafuta masoko wao wamekazana na barabara, hata iweje serikali itajenga tu.

Kwani kuna mbunge aliyeshauri daraja la Tanzanite lijengwe au zile flyovers? Sasa wananchi tusiwarudishe bungeni wabunge wa aina yake. Hizo nyimbo wameimba tangu enzi za mwalimu Nyerere.

Matatizo ya uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja yanatoka na udhaifu wa Bunge wabunge kushindwa kabisa kuibana serikali kuhakikisha inatumia rasilimali zetu ipasavyo kuondokana na umaskini ulioimbwa tangu Uhuru.

@katikabakama.
 
Wabunge wasiojua majukumu yao yaani kazi kupiga makofi na kupitisha makablasha bila kusoma wanapitisha nini wabunge waasi kwa wananchi wanaofunga ndoa nacserikali kuwabagaza wananchi.

Safari hii wabunge wa MWENDOKASI wote hatuwataki
Mkuu ichumu lya , naunga mkono hoja.
Jee uliwahigi kukutana na mabandiko haya?

P
 
Wabunge wasiojua majukumu yao yaani kazi kupiga makofi na kupitisha makablasha bila kusoma wanapitisha nini wabunge waasi kwa wananchi wanaofunga ndoa na serikali kuwabagaza wananchi.

Ninyi wabunge njoo mniambie majukumu yenu Je ni kutetea serikali? Mnajua maana ya uakilishi? Je, sheria mnazopitisha ni kwaajili ya nani? Rejea sheria ya mistu Na.14-2002 inavyoumiza mwananchi, nakumbuka Spika Ndugai aliwahikusema; "Sijui sheria hizi tulizipitisha tukiwa tumelewa?"

Ebu fikiri mimi nipande mti niupalilie, niutunze, nipambane na moto unaochomwa hovyo, ukikua niende kununua kibali cha kuukata, nikimaliza nikanunue kibali cha kusafirisha, kama ni mbao nataka kujenga nikanunue kibali kama ni kuni ninunue kibali kwa Mkurugenzi hata hajui mateso niliyopitia hadi mti umekuwa wakati huo huo ardhi nailipia hivi, sisi tunamilki nini?

Halafu wabunge kwa unafiki wakishapigwa nao wanarudi kwetu kulalamika wakati sheria walipitisha kwa miswada ya dharula mpaka hapo unaona madhara ya kuwa na wabunge makasuku?

Mimi sitaki mbunge mfadhili, sitaki aninunulie hata maji ya 500 sitaki, ninachotaka aende bungeni anitetee, awasilishe mawazo yangu aniambie serikali kwamba wanataka nchi iendeshwe hivi, kodi hii hawaitaki wanataka zahanati, sio tunataka zahanati wanatujengea josho wakati mifugo hatuna, tunataka soko wanatujengea zahanati wakati madawa hakuna.

Nani alikwambia huduma za afya ni majengo tu! Majengo hayawezi kumtibu mtu tunataka vipimo na madawa acheni kuchezea afya zetu, tunataka maji wanatujengea shule wakati muda mwingi watoto wamautumia kutafuta maji. Hii ndiyo kazi ya mbunge sio ufadhili.

Safari hii wabunge wa Mwendokasi wote hatuwataki waende wakajiajiri kama ambavyo wamekuwa wakiwambia vijana wajiajili kwakuwa tayari mtaji wanao waende wakaanzishe mashamba kilimo na ufugaji, wakafanye biashara tuanataka kuona wakilipa kodi maana wao ni mabingwa wa kutunga sheria ngumu za kodi bila kuangalia mazingira ya biashara alafu baada ya miaka 20 tutawarudisha bungeni akili zitakuwa zimeishakaa sawa ili waondoe sheria kandamizi japo najua wengi watakuwa wamepoteza uwezo wao wa kuamua na kufikiri.

Hawa wabunge wanawaona wananchi hawawezi kufikiri vizuri waache tabia ya kutoa ahadi za kujenga miundo mbinu hiyo ni kazi ya serikali lazima itajenga wao wapambane kuinua uchumi wa wananchi wakulima ni masikini, wawatafutie mitaji ili waongeze thamani ya mazao yao na masoko, vijana hawana ajira badala ya kuibana serikali itoe mikopo vijana waanzishe viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mazao ili kuongeza thamani na serikali isaidie kutafuta masoko wao wamekazana na barabara, hata iweje serikali itajenga tu.

Kwani kuna mbunge aliyeshauri daraja la Tanzanite lijengwe au zile flyovers? Sasa wananchi tusiwarudishe bungeni wabunge wa aina yake. Hizo nyimbo wameimba tangu enzi za mwalimu Nyerere.

Matatizo ya uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja yanatoka na udhaifu wa Bunge wabunge kushindwa kabisa kuibana serikali kuhakikisha inatumia rasilimali zetu ipasavyo kuondokana na umaskini ulioimbwa tangu Uhuru.

@katikabakama.
WANAPASWA TUWAPUMZISHE NA SIYO WAPUMZIKE.

"WABUNGE POSHO."
 
Back
Top Bottom