Je, Wabunge wa CCM wafundishwe maana ya Auditing? Hakuna pesa iliyoibwa au kupotea kwenye report ya CAG

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Kwa katiba ya Tanzania ni mahakama tu ndio inathibitisha nani mwizi au sio mwizi na siyo ukaguzi wa CAG au kamati maalum ya bunge

Kama kila mwaka watu wanaiba mbona hawaendi mahakamani?

Kwa ufupi wabunge baadhi wa ccm wafundishwe maana ya ukaguzi au auditing

Ukaguzi unafanywa kwa kuwa na hadidu za rejea au references mara nyingi ni Sera na sheria

Mkaguzi anaangalia sera na sheria inasema nini kuhusu matumizi na ni kitu gani kimefanyika

Wamiliki wa sera na sheria ni bunge lenyewe,Serikali hapa mawaziri na makatibu wao pamoja na mahakama

Ukisikia watu hawajafuata taratibu tambua wamiliki wa hizo taratibu ndio wamewaambia wapindishe taratibu

Mawaziri na makatibu wakuu wana uwezo wa kuwachukulia hatua za nidhamu watumishi kama kweli wameiba pesa lakini kiuhalisia pesa hazijaibwa bali wao ndio wamewaelekeza watumishi wa chini kupindisha sheria

Wabunge wengi wa ccm wanatafuta umaarufu au upenyo wa kusikika ili walau wapate uteuzi wa Rais na kuwa mawaziri

Kelele bungeni bila mpangilio zina lipa sana ,kuna wabunge wamekuwa mawaziri kwa kelele zao bungeni ,Mifano ni mingi sana kuanzia Hussein Bashe,Kitila Mkumbo na Mwigulu mwenyewe alitolewa baada ya kupiga kelele wakati wa corona akarudishwa kuwa waziri

Mambo ya fedha yana sheria zake na kanuni zake zinazopangwa ,Pale kanuni isipofuatwa ya matumizi kwenye report ya CAG yanaitwa matumizi hewa au matumizi yaliyokosa uthibitisho

Wakati wa dharula serikali inabadili matumizi ya pesa iliyopangwa ili kupambana na dharula au wakati mungine kutoa pesa toka kifungu kimoja kuhamishia kifungu kingine kukidhi mahitaji,kwenye Auditing hili huitwa ni tatizo na matumizi yasiyofuata taratibu au sheria

Wabunge baadhi wa ccm wao kwa kufuata mkumbo wanasema pesa zinaibiwa na watendaji wa serikali,Tangu lini mtendaji wa serikali huko halmashauri akageuza matumizi ya pesa bila barua toka kwa wakubwa wake?

Maswali ya kujiuliza?

1.Ni nani anaethibitisha pesa zimeibwa ,Ni wabunge au Mahakama?

2.Na kama pesa zinaibwa ni watu wangapi wapo mahakamani kwa kosa la wizi kwenye kelele za wabunge?

3.Kwanini wananchi walipowatuhumu wabunge wamehongwa pesa za bandari hawakuchukuliana hatua za kinidhamu wao wenyewe? Au kwenda mahakamani ?

Ukifuatilia kelele za bungeni ni kelele za kutaka kusikika au umaarufu,Sifa ya mwanasiasa ni kutajwa tajwa mdomoni na watu ili usisahaulike wakati wa uchaguzi ndio maana wabunge wanaongea pesa zimeibwa lakini huyo mwizi anaiba kila mwaka bila kufikishwa mahakamani

Je, waliozidisha invoice kwenye ile ndege wapo mahakamani?

Je, waliosaini mkataba wa bandari wapo mahakamani?

Je, waliohamishia wanyama chato wapo mahakamani?

Je, walionunua mabehewa ya enzi za vita za vietnam wapo mahakamani?

Sifa ya mwanasiasa ni kutajwa tajwa midomoni mwa watu asisahaulike,Hakuna pesa kwenye report ya CAG aliposema imeibwa bali ni wabunge wenyewe na Mawaziri ndio wanapindisha kanuni na taratibu za matumizi ya pesa na mzigo anaangushiwa mtendaji wa halmashauri au Manispaa
 
Mbuzi wa kafara anatolewa ili wabunge waonekane wamefanya kazi....... wapewe semina.. labda wanajua ila wanajizima data
 
Luhaga Mpina sijui kaishia darasa la ngapi...mtu anasema trillion 280.

Wakati mapato ya nchi mwaka mzima hayafiki trillion 25.. na wapo wanao muamini
 
Luhaga Mpina sijui kaishia darasa la ngapi...mtu anasema trillion 280..
Wakati mapato ya nchi mwaka mzima hayafiki trillion 25.. na wapo wanao muamini
Wabunge wanatafuta umaarufu ili Samia awasikie wapate teuzi

Mpina yeye mwenyewe amepora mashamba Morogoro

Hana credibility yeyote ya kupiga kelele ,Hafai hata kuwa mtendaji wa mtaa
 
Luhaga Mpina sijui kaishia darasa la ngapi...mtu anasema trillion 280..
Wakati mapato ya nchi mwaka mzima hayafiki trillion 25.. na wapo wanao muamini

kwahiyo boss mtu akisema pato lako kwa mwaka ni milioni 15 wakati wewe unapokea milion 1.2 kwa mwezi anakuwa anadanganya si eti eh???

NOTE:siamini katka upotevu wa 280T,ingawa mhusuka anawezakuwa alikosea pia kutaja kiasi.
 
Mawaziri wanamiliki vilabu vikubwa vya mpira wa miguu, unadhani pesa ya kuviendesha inatoka wapi
 
kwahiyo boss mtu akisema pato lako kwa mwaka ni milioni 15 wakati wewe unapokea milion 1.2 kwa mwezi anakuwa anadanganya si eti eh???

NOTE:siamini katka upotevu wa 280T,ingawa mhusuka anawezakuwa alikosea pia kutaja kiasi.
Hajasema pato la mwaka..
Kasema tumeibiwa yote na zaidi...
Ina maana hata mishahara haijalipwa...wala barabara hazijajenngwa ..pesa yote imeibiwa ...na pesa ilyo ibiwa ni ya miaka 10 ndani ya miaka miwili...inawezekanaje??
 
Makamba alitaja vijiji 400+ kuwa ndio idadi kamili ya vijiji vyote kule pembezoni mwa nchi KISHA akasema vijiji 500+ vimefungiwa umeme wa REA.

Raisi, akateua mtoto kutoka shule, akatengua kabla ya kumuapisha! Akarudia uzembe huu mara kadhaa mpaka juzi pale kwa wale akina posta masta.

Najaribu kusema, makosa yapo na hasa yakijjrudia rudia.

Huhitaji kujua namba, auditing, hesabu za fedha, taratibu na sheria za fedha ILI kujua kuwa kwa sasa, PESA ya umma INACHOTWA kweli kweli.

Huhitaji wabunge kusema ili UJUE kuwa kuanzia raisi mpaka mfagizi, WOTE NI UKOO WA PANYA.

Loopholes ndio kichochoro cha WAMELO wa pesa za umma NA always wanajua kutafuta justification.

Mtu anauliza, "mbona hawajapelekwa mahakamani", mahakama ipi sasa? Nani wa kumpeleka?
  • Polisi kaajiriwa kwa ki memo, rushwa au kujuana
  • Hakimu kahitimu kwa rushwa ya fedha, ngono, kuiba mitihani, kununua jina etc

Mwizi mwenyewe ndio ana kinga ya kutoshitakiwa, ambapo, wezi wenzake ndio ukoo wa nzi wa kijani etc.

Bado unahoji?
 
Uongo ukichanganya na ukweli kinachopatikana ni uwongo mtupu...

Kama mtu anaiba milioni 2 wewe unakuja kusema kaiba bilioni 20..
Wewe ni muongo tu....

Kusema pesa inachotwa ni Jambo moja na kutaja kiasi cha uwongo ni Jambo lingine...

Zunguka wee ....lakini uwongo ni uwongo
 
Hajasema pato la mwaka..
Kasema tumeibiwa yote na zaidi...
Ina maana hata mishahara haijalipwa...wala barabara hazijajenngwa ..pesa yote imeibiwa ...na pesa ilyo ibiwa ni ya miaka 10 ndani ya miaka miwili...inawezekanaje??

nina uhakika alikusudia figure nyingine sio hiyo aliyoitaja.

hata mwigulu katika kujibu kwake alijikita ktk kubishia usahihi wa figure sio ufafanuzi katika tuhuma.
 
nina uhakika alikusudia figure nyingine sio hiyo aliyoitaja.

hata mwigulu katika kujibu kwake alijikita ktk kubishia usahihi wa figure sio ufafanuzi katika tuhuma.
Usiseme Una uhakika.
Mbona hasahihishi sasa?
Mtu ana exegerate kusudi akikusudia kuwachota wajinga ....wewe unakuja mtetea Kwa kuamini kakosea figure...
Kila siku anakosea?
Manake kila siku anataja mabilioni ambayo haya make sense
 
Kusema pesa inachotwa ni Jambo moja na kutaja kiasi cha uwongo ni Jambo lingine...
Wangapi wameshindwa kutamka namba walizoandikiwa, iwe bungeni au nje ya bunge?

Nimekupa mfano wa mtu wenu wa karibu, umenielewa?

PESA YA UMMA INAKOMBWA.

Miradi IMESIMAMA kwa kukosa pesa! KILA KITU KINARUDI NYUMA, pesa zinaenda KIZIMKAZI na MIFUKONI MWAO.

NCHI HAINA TENA UWEZO WA KUNUNUA BILA MIKOPO.
 
MTN.jpeg
 
Mbona unaongea Kwa hisia na sio fact?
Pesa ya umma inayokombwa ipi?kiasi gani? mradi gani umesimama??

Why mnapenda kuzungumza vilivyopo kichwani mwenye kama facts?

Umeisoma vizuri ripoti ya CAG au na wewe unahitaji darasa kama ndugu GUSSIE alivyosema?
 
Back
Top Bottom