Elimu kwa Wabunge wa Tanzania

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,318
12,622
Upo wajibu wa Rais, wajibu wa Makamu wa Rais, waziri mkuu, Mawaziri, wabunge, spike na wananchi. Hivyohivyo kwenye ngazi ya familia uko wajibu wa baba, wajibu wa mama na wajibu watoto. Kila wajibu (role) una matarajio (expectations) kwa wale unaowahudumia na mara nyingi kama sio mara zote kila wajibu una malipo yake,

Kama vile ambavyo watoto hawampigii makofi ya pongezi baba anapowaletea chakula au kuwanunulia nguo ndivyo hivyohivyo kila mtu aliyepewa jukumu (na malipo ya jukumu hilo) asivyohitaji kusifiwa sana, kupigiwa makofi kila anapotimiza majukumu yake. Zawadi kuu ya mtu anaetimiza majukumu yake sawasawa na matarajio ya watu wake ni kuheshimiwa na zawadi ya asiyetimiza majukumu ni kulaumiwa na kubezwa na kuondolewa kwenye nafasi.

Inawakera sana wapiga kura wenu kumsikia na kumuona mwakilishi wake bungezi akipoteza muda na nafasi ya kuwatetea kwa kumsifia sana mtu aliyetimiza majukumu yake vizuri. Yaani na watoto wapige makofi kila siku mama abapopika chakula, wapige makofi kumshukuru dada aliyefagia sebule, Tunataka mbunge atumie kila nukta/sekunde anayoipata mule bungeni kwaajili Yao na taifa.

Pili, wazungu hawana kitu Cha Bure hata kimoja. Ukiona anakupa, anakulipia na kukutembelea lazima ushituke kwelikweli. Ukienda kule Ulaya na Marekani Kuna watu maskini sana, wagonjwa sana, na wasio na chakula Wala pakulala lakini serikali haiwajali lakini inatoa msaada kwako wewe mmatumbi, shitukeni.

Mfano, Marekani anakopa China ili atupe sisi msaada!! Umeshaona wapi mtu anakopa Ile akatoe sadaka na zaka? Shitukeni humo bungeni mnaposikia misaada na mikopo imemiminwa Tanzania.

Unakaria kuwa upuuzi unapomsikia mtu anashangilia kupewa mapesa mengi na wazungu halafu huyohuyo analaumu sana kuenea kwa ushoga nchini. Kama mazuzu vile.

Dawa pekee ni kujitegemea, kulipishana Kodi, na kuzilinda Kodi zetu kwa nguvu zetu dhidi ya wezi na wabadhilifu baaasi.
 
Kwahyo wazazi wakinunua chakula huwezi sema Asante? Umeletewa chakula mezani umekula umemaliza huwezi sema Asante kwa aliyekipika? Kwahyo hela ya mkopo haitakiwi kutolewa sadaka makanisan au kwa watu wenye uhitaji?

Kushukru na kupongeza kwa mtu kutekeleza majukumu yake ipasavyo ni desturi na nikawaida kwa mtu yyote yule ndo maana hata chuleni/vyuoni baada yakumaliza masomo tunapewa pongezi ya vyeti ingawa kusoma na kufaulu ilikuwa ni wajibu watu.

Umeleta hoja ya mtu jeuri Sana? Eti kusomeshwa ni wajibu wazazi kwahyo unapopewa pay in slip ya ada Hakuna haja ya kusema asante...unapotoka
 
Kushukuru na kupongeza ni tofauti kabisa.. mtoto akiletewa gauni atashukuru na sio kupongeza Kwa kuwa huo ni wajibu wa baba yake.
 
Kusema Asante ni tabia TU maana hata aliyefuta meza ya chakula tunamwambia Asante, lakini hata tusipomwambia Asante lazima afute TU kwakuwa analipwa kwa kuifuta meza. Hivi unataka watoto mmojammoja wasimame na kumsifu baba Yao na kupiga makofi kwa kuleta tv nyumbani. Kazi ya baba ni kuleta na watoto ni kufuta meza baada ya kule na kumheshimu baba Yao mengine yote ni ziada (makruhu). Yaani mtoto akimletea baba kibiriti Cha kuwashia sigara yake baba apige makofi.
 
Kupongeza kunamtia moyo mtoaji
Tofautisha kupongeza na kujipendekeza, na huko kujipendekeza kunatokana na kuingia madarakani bila ridhaa za wananchi, bali mbeleko ya vyombo vya dola ambavyo rais ndio ana mamlaka navyo.
 
Kupongeza kunamtia moyo mtoaji
Kutimiza jukumu lako ambalo jamii inatarajia ulitimize hakujitaji mtu kutumia dk 5 kumshukuru. Mzazi anaemsomesha mtoto wake hadi chuo kikuu mtoto wake anatakiwa kufanya nini kumshukuru mzazi wake? Kutimiza majukumu yako kikamilifu Kunaleta Ile kitu inaitwa self motivated. Yaani Rais anapoamka na kukuta nchi salama, vifo vimepungua, vijana Wana ajira, hakuna anaemtukana Wala kumsumbua, watoto wote wanakwenda shule, COVID 19 imekwisha inatosha sana kumpatia faraja. Kusifiwa na zawadi ni level ya chini kabisa ya binadamu kama ville watoto wa chekechea na primary school.
 
Kushukuru na kupongeza ni tofauti kabisa.. mtoto akiletewa gauni atashukuru na sio kupongeza Kwa kuwa huo ni wajibu wa baba yake.
Kushuru ni kusema asante, haichukui hata nusu sekunde. Kuna wakati hata Rais anachukizwa na hii tabia ya hovyo. Rais anajua kuwa hizo pongezi ni unafiki na wala hazitoki kwa wananchi wake bali ni shida ya tumbo ya mpongezaji. Rais anafahamu kuwa wanachi bado wanazo KERO nyingi sana ambazo zinahitaji kutatuliwa. Rais anajua kuwa watu hawana maji, shule na hospital hakuna watumishi, anajua bei za kila kitu ziko juu. mama anafahamu kuwa hawahawa ndio walewale na hivihivi tangu wakati wa JK na JPM wanaosifia kichawachawa kwa kutumia matumbo Yao. Anafahamu kuwa yeye akiondoka watasifia hivihivi kwa Rais ajae.
 
Kwahyo wazazi wakinunua chakula huwezi sema Asante? Umeletewa chakula mezani umekula umemaliza huwezi sema Asante kwa aliyekipika? Kwahyo hela ya mkopo haitakiwi kutolewa sadaka makanisan au kwa watu wenye uhitaji?

Kushukru na kupongeza kwa mtu kutekeleza majukumu yake ipasavyo ni desturi na nikawaida kwa mtu yyote yule ndo maana hata chuleni/vyuoni baada yakumaliza masomo tunapewa pongezi ya vyeti ingawa kusoma na kufaulu ilikuwa ni wajibu watu.

Umeleta hoja ya mtu jeuri Sana? Eti kusomeshwa ni wajibu wazazi kwahyo unapopewa pay in slip ya ada Hakuna haja ya kusema asante...unapotoka
Kusema Asante ni kumshukuru sio kumpongeza, hata Mungu huwa tunamshukuru, hatumpongezi. Pongezi zenu kwa Rais hazina uhalisia, zimejaa unafiki mtupu kwakuwa wananchi wanamdai sana Rais wao madai ambayo hata wabunge wao wanayafahamu na hata Rais mwenyewe anayajua ndio maana halali na kutulia kwaajili yetu. Royal tour ni ushahidi ya hili nsemalo. Kazi yenu nyie mliyotumwa na wananchi ni kusema nini bado sio nini tayari, nini hamjapata sio nini mmepata, nini hamjakula sio nini mlichokula tayari. Kazi nyingine ni kumsaidia Rais kunusa hatari kwa taifa na kwa watu wenu. Wabunge wote semeni "Wazungu hawana kitu Cha Bure" ili kila mkiona vitu vya Bure, upendeleo, na mteremko kutoka kwa Wazungu mjiulize wote mara tatutatu swali la "kwanini sisi? Wanataka nini? na kwanini Sasa?".
 
Rais huyu anafahamu kuwa wengi mnachojali ni matumbo yenu. Anafahamu kuwa mliimba iyena iyena nyakati zote na awamu zote hata wakati wizi wa EPA, escrow, Richmond, kutaisha mashirika, kuuza nyumba za serikali, kuingia mikataba ya uchimbaji madini, kulalamikia makenikia, kununua ndege kwa cash na hata watanzania wengine wakiokotwa kwenye fukwe na wengine kupotea. Waliimba iyena hata Jecha alivyofanya yake bila kujali roho ngapi zitapotea kwa kufuta uchaguzi kipuuzi kama vile.
 
Upo wajibu wa Rais, wajibu wa Makamu wa Rais, waziri mkuu, Mawaziri, wabunge, spike na wananchi. Hivyohivyo kwenye ngazi ya familia uko wajibu wa baba, wajibu wa mama na wajibu watoto. Kila wajibu (role) una matarajio (expectations) kwa wale unaowahudumia na mara nyingi kama sio mara zote kila wajibu una malipo yake,

Kama vile ambavyo watoto hawampigii makofi ya pongezi baba anapowaletea chakula au kuwanunulia nguo ndivyo hivyohivyo kila mtu aliyepewa jukumu (na malipo ya jukumu hilo) asivyohitaji kusifiwa sana, kupigiwa makofi kila anapotimiza majukumu yake. Zawadi kuu ya mtu anaetimiza majukumu yake sawasawa na matarajio ya watu wake ni kuheshimiwa na zawadi ya asiyetimiza majukumu ni kulaumiwa na kubezwa na kuondolewa kwenye nafasi.

Inawakera sana wapiga kura wenu kumsikia na kumuona mwakilishi wake bungezi akipoteza muda na nafasi ya kuwatetea kwa kumsifia sana mtu aliyetimiza majukumu yake vizuri. Yaani na watoto wapige makofi kila siku mama abapopika chakula, wapige makofi kumshukuru dada aliyefagia sebule, Tunataka mbunge atumie kila nukta/sekunde anayoipata mule bungeni kwaajili Yao na taifa.

Pili, wazungu hawana kitu Cha Bure hata kimoja. Ukiona anakupa, anakulipia na kukutembelea lazima ushituke kwelikweli. Ukienda kule Ulaya na Marekani Kuna watu maskini sana, wagonjwa sana, na wasio na chakula Wala pakulala lakini serikali haiwajali lakini inatoa msaada kwako wewe mmatumbi, shitukeni.

Mfano, Marekani anakopa China ili atupe sisi msaada!! Umeshaona wapi mtu anakopa Ile akatoe sadaka na zaka? Shitukeni humo bungeni mnaposikia misaada na mikopo imemiminwa Tanzania.

Unakaria kuwa upuuzi unapomsikia mtu anashangilia kupewa mapesa mengi na wazungu halafu huyohuyo analaumu sana kuenea kwa ushoga nchini. Kama mazuzu vile.

Dawa pekee ni kujitegemea, kulipishana Kodi, na kuzilinda Kodi zetu kwa nguvu zetu dhidi ya wezi na wabadhilifu baaasi.
Bhaeleze. Wabunge wengi ni weupe kichwani. Kumbuka hawa wamepitishwa kwa mkono wa chuma cha jiwe, hawakuchaguliwa na wananchi. They are totally bogus.
 
Sio weupe kihivyoo, bali walivyoupata ubunge wao ndio chanzo Cha tatizo. Unapokuwa na uhakika kuwa nisingekuwa mbunge bila hiki na kile inakufanya uwaze tumbo lako kwanza kabla ya majukumu ya ubunge. Wakina Nyerere, kwame, Mandela hawakumbukwiu eti kwakuwa walikuwa Marais, no no no, wanakumbukwa kwasababu wameacha alama zisizofutika kwenye mgongo wa ardhi na kwenye jamii. Mtu aliyepanda mti mmoja wa kivuli kabla hajakufa ni Bora kuliko mbunge mjinga, muoga na anasifia na kupiga makofi kila jambo hata lile analoliamini kuwa ni baya kwake, kwa watu wake, kwa Tanzania, kwa dunia na hata kwa Mungu. Brother hatuishi milele hebu tuchague vitu vya kuwaachia wezetu tutakopokufa.
 
Back
Top Bottom