Rais Samia: Polisi hakikisheni ‘Vi-clip clip’ visirushwe, msimame kwenye mambo yenu

Rais Samia: Polisi hakikisheni ‘Vi-clip clip’ visirushwe, msimame kwenye mambo yenu

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
28,905
Reaction score
92,331
Yeye kwake Kosa sio Jeshi la Polisi Kuchukua Rushwa .....ilo aaahhhhhh.

Kosa ni 'Clip za Rushwa kuwekewa mitandaoni'.

Yaan kwa Mfano, Umeoa, umefunga zako CCTV ndani, umesafiri, Mkeo kaleta Mchepuko ndani, unamfuma na kumwonyesha hizo Video.

MKE Anaanza kukulaumu akijitahidi kuonyesha kua Kosa ni Lako wewe, kwann uweke Kamera 🤣🤣

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Mei 28, 2026 Jijini Dar es salaam amesema Askari Polisi wanapaswa kurekebisha mwenendo usiofaa unaochafua taswira ya Jeshi la Polisi mbele ya Wananchi.

Dkt. Samia ameyasema hayo wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi zilizofanyika katika Chuo cha Polisi Kurasini, ambapo amesisitiza umuhimu wa nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa Askari wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Tumezoea huko nyuma kuona Askari wakisimamisha magari na wakifanya mambo ambayo hayakubaliki, sasa hizo ndio nyanja za medani muende mkarekebishe hayo, yale tunayoyaona viclip vinavyorushwa rushwa visirushwe askari wetu msimame kwenye mambo yenu” amesema Rais Samia.

Anataka aiache Tanzania ikiwa inanuka Rushwa. Nilisha waambia, Samia hana cha kupoteza. Hata muuane yeye hajali..

Mla rushwa hawezi kemea rushwa
Umesema vyema hana cha kupoteza kwao Oman huyo. Yaani Tanzania sasa hivi inatajirisha Oman na watu wa vyombo vya usalama wapo tu.
Nadhani ata watu wa vyombo vya usalama wengi sidhani ni watanzania halisi
 
Yeye kwake Kosa sio Jeshi la Polisi Kuchukua Rushwa .....ilo aaahhhhhh.

Kosa ni 'Clip za Rushwa kuwekewa mitandaoni'.

Yaan kwa Mfano, Umeoa, umefunga zako CCTV ndani, umesafiri, Mumeo kaleta Mchepuko ndani, unamfuma na kumwonyesha hizo Video.

MKE Anaanza kukulaumu akijitahidi kuonyesha kua Kosa ni Lako wewe, kwann uweke Kamera 🤣🤣
Duh nimesoma mara mbilimbili kumbe Samia anasema "visirushwe" nilifikira anataka "virushwe", kumbe hataki! Doh!
 
Ukisikia kupatwa kwa Tanganyika ndiyo huku sasa!

Hao askari wa usalama barabarani wamekuwa ni kero kubwa kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto, hususani magari! Wamekuwa na tabia ya kulazimisha kupewa rushwa mchana kweupe! Tena wana tabia ya kujipangia mpaka kiwango cha kuchukua! Ukikataa kuwapatia hiyo rushwa wanayoitaka, wanakuandikia faini!!

Halafu kama kiongozi badala ya kuangalia namna ya kuvikomesha hivi vitendo vya hovyo, unakuja na maelezo ya kutaka kudhibitiwa kwa clip zinazowaonesha hawa fisi wasiotosheka na mishahara yao wakipokea hizo rushwa!! Kazi kweli kweli.
 
Yeye kwake Kosa sio Jeshi la Polisi Kuchukua Rushwa .....ilo aaahhhhhh.

Kosa ni 'Clip za Rushwa kuwekewa mitandaoni'.

Yaan kwa Mfano, Umeoa, umefunga zako CCTV ndani, umesafiri, Mumeo kaleta Mchepuko ndani, unamfuma na kumwonyesha hizo Video.

MKE Anaanza kukulaumu akijitahidi kuonyesha kua Kosa ni Lako wewe, kwann uweke Kamera 🤣🤣
Huwa anatoa boko everytime akiongea public, what in the hell? Yaani wanao expose madudu badala walindwe eti hakikisha clip zisirushwe?

We have failed kama taifa,
 
Screenshot_20260528_175802_Instagram Lite.jpg
 
Back
Top Bottom