Je, Roma Mkatoliki anaandaliwa kuwa shahidi wa ICC?

CCM wajipange, wabeberu safari hii wataondoka na vichwa vingi sana utawala huu.

Kidogo kidogo wameanza kula "MATAPISHI" yao, wamepeleka muswada bungeni (kama kawaida yao kwa HATI YA DHARURA) kuomba sheria ya Arbitration ibadilishwe ili migogoro ya madini iwe inasuluhishwa kwenye Mahakama Ya Biashara Ya Kimataifa.

Kwa mtazamo wangu, watu wasiojulikana watakuja kufanya "MAAMUZI" magumu sana kwa yule "MKUU WA MIKOA YOTE TANZANIA", ili kuficha aibu yao.

To be continued. . . . . . .
Hapo mwisho kabla ya To be continued pananifikirisha
 
ROMA kapewa hadhi ya Ukimbizi USA?
Naye yule Beneficial wa Chuga naye ana tatizo gani na mamlaka maana wote wako huko kwa Trump toka mwaka Jana.
Ni vizuri ukacheck facts zako ili ulete habari za ukweli vinginevyo ule "Ujuaji" unaosemwa unao kule jukwaa la " pongezi na malalamiko" utaonekana ni kweli
Mbona Benificial alisharudi kitambo, na aliporudi aka-perform 'Cheka Tu' akielezea aliyoyaona USA...
 
Kwaiyo, Wewe Unakataa hawezi Kushitakiwa ICC? Tupe sababu zako

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashindwq hata kuargue maana aliyeleta habari amebaka tasnia. Mimi nilidhani angeiondoa, tofaauti na hapo atafuye mtu amuandikie halafu ndio great thinkers tutilike. Hakuna alichoanzika cha kufanya ni argue zaidi ya ramri tu!
 
Nimeshangazwa na hadhi ya ukimbizi aliyopewa Roma Mkatoliki nchini Marekani. Hii pengine inatokana na kule kukamatwa kwake na wale WASIOJULIKANA kisha katika hali ya kushangaza sana na kwa muda uliopangwa Roma akapatikana akiwa hoi majeruhi na majeraha ya kuteswa.

Baada ya kupata nafuu majeraha yale ya mwili aliongea kilichompata. Lakini kukiwa na kila dalili kwamba alificha ama aliogopa kuongea mengi. Kutoka hapo Roma hakuwa sawa tena kama zamani. Kuna mzimu ulikuwa unamuandama.

Nusu ya pili ya mwaka jana 2019 Marekani na washirika wake wakaanza kutoa maangalizo na matamko kuhusiana na hali ya kuzorota kwa haki za binadamu, usalama na uhuru wa kutoa maoni. Ni katika kipindi hicho Roma alitimkia Marekani na hatimaye vikafuatia vikwazo kwa baadhi ya viongozi kusafiri na kuingia marekani sambamba na kunyimwa misaada na mikopo nk

Kwenye taarifa ya Marekani hawakumung'unya maneno walimtaja kiongozi mmoja kama wa kwanza kuwekewa kikwazo cha kusafiri Marekani.

Ni kiongozi huyo huyo aliyeahidi kupatikana kwa Roma ndani ya muda fulani naye pia akapatikana kweli. Kiongozi huyo ana lundo la tuhuma za kuteka. Waliotekwa na kupotea ni wengi. Ni Roma na wachache wamebahatika kutekwa na kurudi hai.

Kwenye taarifa ya Marekani wameweka wazi kuwa vikwazo ni hatua za mwanzo tuu.. Kwa maana hiyo hatua zaidi zinafuata. Je ni hatua gani hizo? Je ni mashtaka ICC?

Kama ni mashtaka ICC, Maana yake kutahitajika ushahidi usio acha shaka na mashahidi pia. Roma ni mhanga wa kutekwa na Marekani kaenda kama mkimbizi.

Huyu anaweza kuwa shahidi muhimu sana, hivyo kuepuka kudhurika ama kutishwa asitoe ushahidi pengine ndio maana kakimbiziwa mbali aje kumkaanga mtu. Wengine ni Msaidizi wa Membe na Msaidizi wa Zitto wako wapi hawa?

Jr™️
Marekani sio mwanachama wa ICC na hajihusishi kabisa nayo.
 
Mnapata wapi ujasiri wa kujadili mambo magumu wakati leo TEAM YA WANANCHI iko uwanjan kutoa ladha kwa watz
 
Jr
Wamchukue na Mo Dewji akawe shahid wa kesi za kutekana.
 
ROMA kapewa hadhi ya Ukimbizi USA?
Naye yule Beneficial wa Chuga naye ana tatizo gani na mamlaka maana wote wako huko kwa Trump toka mwaka Jana.
Ni vizuri ukacheck facts zako ili ulete habari za ukweli vinginevyo ule "Ujuaji" unaosemwa unao kule jukwaa la " pongezi na malalamiko" utaonekana ni kweli
Uzi umekaa kama swali ili kutoa mwanya mkubwa wa member kuujadili, kwa hiyo kama lipo unalolijua unaweza kujadili bila kumshambulia mleta mada kama huna kaa kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa maada ndo boya kwa kuleta vitu ambavyo hata havielewi, kisa kujitia unuaji wa kila kitu. Yeye abaki kwenye matunguli huku awaachie wenye weledi wao. Unaleta issue ya ICC halad huelezi how Roma anaweza kuwa shahidi kwa angle ipi na makosa yapi and against who. Huo ndo ugreat thinker, siyo kuleta habari au arguement ambayo haina basis yoyote. Huu ni ujuha!
Nimehitimisha kuwa wewe ni mjinga na una personal hatred na Mshana Jr. Umeambiwa Mara chungu nzima toa wewe ufafanuzi maana hoja ya Mshana iko kwenye msingi endelevu tujadili uwezekano huo, badala yake unakomaa na upuuzi wako kuwa yeye ni mjuaji.
Usianzishe ligi usizoziweza wewe kijana, acha tupeane maujuzi na kama mleta mada kuna mahali hakuelewa ataelewa, ebo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom