OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 420
- 670
Rais Samia akiongea na waandishi wa Habari leo amekataa kuwa watanzania hawatumii chini ya dola moja kama inavyolipotiwa ambapo ametumia kabila la wahadzabe kama kabila la chini ambao wanaishi kwa kula matunda na asali ambayo hawanunui. Hivyo ukiweka kifedha inawezekana wanatumia gharama kubwa.
Mbali na kauli hiyo nimewaza sana kuhusu watu wanaopinga matumizi ya Per Capita income kama kipimio cha utajiri na umasikini. Hata hivyo, taasisi za maendeleo zinapima umasikini kivingine na sio tena kutumia GDP per Capita. Kwa tafsiri ya sasa ya maendeleo sio tena masuala ya kifedha bali kwenye 'Freedoms and Choices', na namna ambavyo mtu anaweza ku-command mazingira yake. Hapa ndipo utaona umasikini.
Katika ku-command mazingira na kuongeza freedoms and choices tunaangalia, Je huduma kama maji, ziko mbali kiasi gani? Je, mmeweza kuamrisha maji yaje nyumbani kwako au umelazimishwa kuyafuata maji yaliko?. Je unaweza kutiisha viumbe wadogo walioko mwilini mwako(Microbes) au wadudu wanakuamrisha na kukuua?. Je unakula mara mbili kwa siku kwa kuamua au kuamamrishw na mfuko wako?
Kwa hiyo ndugu zetu wahadzabe ambao wanaingia porini kutafuta matunda, wameshindwa kuamrisha matunda ywe kwenye maeneo yao (Gathering) stage ambayo makabila mengine yameshapita miaka mingi iliyopopita. Je kitendo cha wao kushindwa kuamrisha kitu kidogo kama hivho kinawafanya wawe wenye maendeleo.?
Ni kweli kuwa GDP per Capita ina kasoro nyingi katika kupima uchumi lakini haifanyi mtu kuwa tajiri kwa kushindwa kuamrisha mazingira yake. Bado Tanzania ni masikini, anaamrisha na hali ya hewa, magonjwa, natural calamities etc.
Signed
OEDIPUS