Je, Rais yuko sahihi kuhusu umasikini?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Rais Samia akiongea na waandishi wa Habari leo amekataa kuwa watanzania hawatumii chini ya dola moja kama inavyolipotiwa ambapo ametumia kabila la wahadzabe kama kabila la chini ambao wanaishi kwa kula matunda na asali ambayo hawanunui. Hivyo ukiweka kifedha inawezekana wanatumia gharama kubwa.

Mbali na kauli hiyo nimewaza sana kuhusu watu wanaopinga matumizi ya Per Capita income kama kipimio cha utajiri na umasikini. Hata hivyo, taasisi za maendeleo zinapima umasikini kivingine na sio tena kutumia GDP per Capita. Kwa tafsiri ya sasa ya maendeleo sio tena masuala ya kifedha bali kwenye 'Freedoms and Choices', na namna ambavyo mtu anaweza ku-command mazingira yake. Hapa ndipo utaona umasikini.

Katika ku-command mazingira na kuongeza freedoms and choices tunaangalia, Je huduma kama maji, ziko mbali kiasi gani? Je, mmeweza kuamrisha maji yaje nyumbani kwako au umelazimishwa kuyafuata maji yaliko?. Je unaweza kutiisha viumbe wadogo walioko mwilini mwako(Microbes) au wadudu wanakuamrisha na kukuua?. Je unakula mara mbili kwa siku kwa kuamua au kuamamrishw na mfuko wako?

Kwa hiyo ndugu zetu wahadzabe ambao wanaingia porini kutafuta matunda, wameshindwa kuamrisha matunda ywe kwenye maeneo yao (Gathering) stage ambayo makabila mengine yameshapita miaka mingi iliyopopita. Je kitendo cha wao kushindwa kuamrisha kitu kidogo kama hivho kinawafanya wawe wenye maendeleo.?

Ni kweli kuwa GDP per Capita ina kasoro nyingi katika kupima uchumi lakini haifanyi mtu kuwa tajiri kwa kushindwa kuamrisha mazingira yake. Bado Tanzania ni masikini, anaamrisha na hali ya hewa, magonjwa, natural calamities etc.

Signed

OEDIPUS
 
Hata waliopo mijini wanalazimika kujenga jirani na mtandao wa maji na ule wa umeme. Mtu akijenga pembezoni sana hapati hizo huduma.

Kwahiyo hakuna mtu anafanya komandi kwa huduma Bali huduma inakomandi watu.
Conclusion: We are poor.
 
Ukiona unashindwa kumwagilia, unasubiri hadi mvua inyeshe ndio ulime. Hapo umeshindwa ku-command. Mtu mwenye command hana majira wala vipindi
 
Ni kweli Africa vipimo vya umaskini haviwork vizuri maana unakuta mtu anaingiza cash 2500 kwa siku lakini matumizi yake ni over 5000.
Mtu yupo kijijini wiki nzima anaweza kufanya manunuzi ya 500 tu ya vocha kupigia ndugu na jamaa.
Zaidi ya hapo chakula anacho anachuma mboga porini au kuwinda ndege na wanyama, chanzo cha nishati(kuni/mkaa) anao. Amejenga anafuga ng'ombe kwahiyo anapata maziwa.
Anaishi maisha mazuri yasiyohusisha hela.
 
Hakuna kipimo kimoja cha maendeleo. Kila kimoja ni muhimu lakini peke yake hakijitoshelezi. Ndiyo maana **** GDP per capita, Gini na HDI.
 
Nimemsikiliza Rais Samia na mifano yake ya nyama kwa Masai na jamii inayozalisha matunda akitolea mfano yanavyouzwa ghali Ulaya kwakuwa ni organic.

GDP haipimi quality of life, inapima financial values.. Mtu wa Muheza vijijini ukimuambia uza gunia la machungwa kwenye mazingira yako uende hospitali ukajitibie, anaweza asipate mteja, kila mtu anayo yanaoza japokuwa gunia hilo likifika ulaya ni dollars za kutosha kufanya mambo mengi..

Ulaya mbali, nyama kilo moja ya mmasai Dar ni zaidi ya dollar tatu, lakini umasaini haiwezi kukupa hiyo hela ukanunue mchele kutoka Mbarali..
 
  • Thanks
Reactions: OLS
Ni kweli Africa vipimo vya umaskini haviwork vizuri maana unakuta mtu anaingiza cash 2500 kwa siku lakini matumizi yake ni over 5000.
Mtu yupo kijijini wiki nzima anaweza kufanya manunuzi ya 500 tu ya vocha kupigia ndugu na jamaa.
Zaidi ya hapo chakula anacho anachuma mboga porini au kuwinda ndege na wanyama, chanzo cha nishati(kuni/mkaa) anao. Amejenga anafuga ng'ombe kwahiyo anapata maziwa.
Anaishi maisha mazuri yasiyohusisha hela.

Huwa tunaita exclusion of non-market transactions ambayo ni mapungufu ya matumizi ya GDP lakini mama hajaongelea hili, mama kaongelea thamani yake, kwamba matunda yanayoliwa Tanzania yana thamani kubwa Ulaya hata kama vijijini yanaoza bila mnunuzi kwa sababu ni organic.. Yale matunda yako vijijini na yatapimwa kwa thamani yake yakiwa huko
 
Rais Samia akiongea na waandishi wa Habari leo amekataa kuwa watanzania hawatumii chini ya dola moja kama inavyolipotiwa ambapo ametumia kabila la wahadzabe kama kabila la chini ambao wanaishi kwa kula matunda na asali ambayo hawanunui. Hivyo ukiweka kifedha inawezekana wanatumia gharama kubwa.

Mbali na kauli hiyo nimewaza sana kuhusu watu wanaopinga matumizi ya Per Capita income kama kipimio cha utajiri na umasikini. Hata hivyo, taasisi za maendeleo zinapima umasikini kivingine na sio tena kutumia GDP per Capita. Kwa tafsiri ya sasa ya maendeleo sio tena masuala ya kifedha bali kwenye 'Freedoms and Choices', na namna ambavyo mtu anaweza ku-command mazingira yake. Hapa ndipo utaona umasikini.

Katika ku-command mazingira na kuongeza freedoms and choices tunaangalia, Je huduma kama maji, ziko mbali kiasi gani? Je, mmeweza kuamrisha maji yaje nyumbani kwako au umelazimishwa kuyafuata maji yaliko?. Je unaweza kutiisha viumbe wadogo walioko mwilini mwako(Microbes) au wadudu wanakuamrisha na kukuua?. Je unakula mara mbili kwa siku kwa kuamua au kuamamrishw na mfuko wako?

Kwa hiyo ndugu zetu wahadzabe ambao wanaingia porini kutafuta matunda, wameshindwa kuamrisha matunda ywe kwenye maeneo yao (Gathering) stage ambayo makabila mengine yameshapita miaka mingi iliyopopita. Je kitendo cha wao kushindwa kuamrisha kitu kidogo kama hivho kinawafanya wawe wenye maendeleo.?

Ni kweli kuwa GDP per Capita ina kasoro nyingi katika kupima uchumi lakini haifanyi mtu kuwa tajiri kwa kushindwa kuamrisha mazingira yake. Bado Tanzania ni masikini, anaamrisha na hali ya hewa, magonjwa, natural calamities etc.

Signed

OEDIPUS
Kwa hizi arguments zako na parameters ulizotumia nadhani idadi ya maskini ni kubwa sana tena sana.
Anyway; nimekuelewa!
 
  • Thanks
Reactions: OLS
Ni kweli Africa vipimo vya umaskini haviwork vizuri maana unakuta mtu anaingiza cash 2500 kwa siku lakini matumizi yake ni over 5000.
Mtu yupo kijijini wiki nzima anaweza kufanya manunuzi ya 500 tu ya vocha kupigia ndugu na jamaa.
Zaidi ya hapo chakula anacho anachuma mboga porini au kuwinda ndege na wanyama, chanzo cha nishati(kuni/mkaa) anao. Amejenga anafuga ng'ombe kwahiyo anapata maziwa.
Anaishi maisha mazuri yasiyohusisha hela.
Hakuna kitu kama hicho,sasa hivi maisha ya vijijini yamekuwa magumu,afadhari ya mjini
 
Back
Top Bottom