Je, Rais ana mamlaka ya Kumvua Mtu "Ubunge"?

Je, Rais ana mamlaka ya Kumvua Mtu "Ubunge"?

Ni makamu wa raisi pekee ndie ana uhakika wa kumaliza kipindi chote wengine wote ,ukiondoa wenye nadhifa za kuchaguliwa na wananchi wanawekwa na kuondolewa panapo matakwa ya alie wateua
Acha ubishi wa kijinga , soma katiba
110(6a,b -7) iyo kuhusu jaji mkuu.
Ngoja nikutafutie na ya mbunge, pamoja na CAG
 
Ila mbunge atakayepewa maelekezo ya kimkakati kujiuzulu ana mamlaka ya kujiuzulu na atapangiwa kazi ingine.
Kwa ccm mdomo unafungwa kwa zip hakuna kuhoji.
 
Tupe kifungu cha katiba kinachoweza kumfanya Mbunge kuacha ubunge kwa ajili ya majukumu mengine mapya ya kikazi.
Mfano Asha Rose Migiro alivyoacha uwaziri wake kwa ajili ya majukumu mengine.

Tusaidiane mawazo.
67(2)g
Mtu atalosa sifa za kuwa mbunge
ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa
mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza
au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa
Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
 
Tupe kifungu cha katiba au sheria kinachosema katiba imevunjwa hadi raisi anapaswa kuomba radhi ndio tuendelee kukujadili .
usipotekeleza takwa la kikatiba na kwenda kinyume chake maana yake nini?
ukipenda,hata chongo utaita kengeza
 
usipotekeleza takwa la kikatiba na kwenda kinyume chake maana yake nini?
ukipenda,hata chongo utaita kengeza
Unadhani hiyo idadi ya wanawake ndio kavunja katiba ?subiri uone hadi mwisho ndio utoe hizo methali zako.
 
Lakini bado haifuti ukweli kwamba possi alikwishateuliwa kuwa mbunge miongoni mwa zile nafasi kumi.. Kwa maana kwamba possi amekula nafasi moja kati ya zile kumi za rais,kwahiyo hapa kama bulembo na prof kabudi wakiapa kuwa wabunge bado ibara ya 66(1)(e) itakuwa imekiukwa!
Hapana amekwisha rectify kosa LA kukiuka katiba. Mtu akipoteza sifa ya kuwa mbunge nafasi yake inakuwa wazi na inaweza kujazwa na mamlaka ya uteuzi ikitegemeana ni wa kuteuliwa, kuchaguliwa jimboni au viti maalumu wanawake
 
Unadhani hiyo idadi ya wanawake ndio kavunja katiba ?subiri uone hadi mwisho ndio utoe hizo methali zako.
ningoje nini tena?Utenguzi wa Posi ni uthibitisho tosha kuwa anajaribu kufix makosa yake,hajui tu kuwa anazidi kuongeza makosa.
 
Swali:

Hivi Raisi akiteua mtu kuwa mbunge na baadae mtu huyo akajiuzulu ubunge au kupoteza sifa ya kuwa mbunge,idadi ya wabunge walioteuliwa na Raisi inapungua au inabaki pale pale?
Swali zuri sana hili...3D!
 
Rais hana mamlaka ya kumvua yeyote ubunge; Huu ni mchezo umechezwa baada ya yeye kuchemka kwenye teuzi, hivyo kilichofanyika ni namna ya kupunguza idadi ya wabunge walioteuliwa ili kuleta uwiano kama katiba inavyosema, hivyo Posi atalazimika kujiuzulu ubunge wake!!
Tuangalie ibara hii kwenye katiba..
* Ibara ya 71*

Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-

(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;

(b) ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;

(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;

(d) ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge;

(f) iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa Makamu wa Rais;

(g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge

*lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake*
Ya nadhani kifungu (a) kimeshatimia
 
Ndugu zangu wasalam! Kwa mujibu wa katiba yetu mbovu yenye viraka lukuki(amendments)Rais hana mamlaka ya kutengua uteuzi wa mbunge yeyote hata km alimtea yy,kwa sababu kwa mujibu wa katiba mbunge anaapa mbele ya bunge tukufu la jamhuri ya muungano wa Tanzania na sio rais hivyo mbunge anapoapa anawajibika mbele ya bunge.Rais wetu amevunja katiba hili haliepukiki na tuache siasa za kijinga ndugu zangu watanzania tusiwe wavivu kusoma katiba yetu.
Alivunja Katiba kwa Kuteua Wanaume wengi zaidi, Sasa kwa kuwa huyu Ngosha amejaa hila na ghiliba anataka kupunguza Wale wanaume. Tatizo la huyu Mhalifu mkuu (kuvunja katiba ni Uhalifu) anadhani anaakili kuliko Watanzania wote. By the way hiyo ndio mind set ya criminals wanadhani wanaakili kuliko wote na kuliko systems
 
mihemko yake ndio katiba yetu, acheni kuhoji tuvumilie tu!
 
Back
Top Bottom