Je, Rais ana mamlaka ya Kumvua Mtu "Ubunge"?

Je, Rais ana mamlaka ya Kumvua Mtu "Ubunge"?

Kasome upya hicho kifungu cha 67 (2g) ukielewe vizuri ndio urudi tena kutueleza.
Kwa akili zangu za kidwanzi nazani Raisi awezi. ..kuna watu wawili Rais anaweza kuwateua lakini awezi kuwavua , navyo ni Jaji mkuu na mbunge ...wajuaji watareta vifungu hapa
Ni makamu wa raisi pekee ndie ana uhakika wa kumaliza kipindi chote wengine wote ,ukiondoa wenye nadhifa za kuchaguliwa na wananchi wanawekwa na kuondolewa panapo matakwa ya alie wateua
 
Pamoja na Rais kumteua Mhe. Posi kuwa balozi lakini ubunge wake unabaki pale pale!

Hivyo bado kuna wabunge 6 wa kiume ambao Rais ameteua kinyume cha katiba!!

Katiba imevunjwa huo ndiyo ukweli na hatua za kumwajibisha Rais zinapashwa kuanza kuchukuliwa!!

Rais aliapa kulinda katiba lakini sasa amekiuka! Sheria ni msumeno unakata mbele na nyuma!!!

Ni kipimo kizuri sana kujua kuwa je wapo watu ambao wapo juu ya katiba?
utaiona hii kesi itakavyoishia!
kina Lema wao wakiikosea katiba hamna story wanaanzia ndani kwanza!
 
Rais anayomamlaka ya kumvua Ubunge,Mbunge ambaye amemteua yeye.
Pamoja na kuisoma na kuinakiri na kuiweka hapa jukwaani, bado naweza kusema huelewi ulichokisoma. Ni wapi hapo Katiba imempa uwezo Rais kumvua mtu ubunge aliopewa na Rais? Rais kapewa mamlaka ya kuwateua na kuwatengua watendaji wa Serikali, na si zaidi ya hao...
Mahakama na Bunge ni mihimili isiyo ya serikali. Ndo sababu Rais hawezi kutengua nafasi ya Jaji yeyote hata kama amemteua yeye. Vivyo hivyo kwa Mbunge.
Inatosha kusema tu kuwa Rais ameteleza.
Mbaya zaidi hata njia inayotumika kujisahihisha pia sio sahihi.
Inazidisha matatizo badala ya kuyatatua.
Ni aibu kumteua Mbunge kuwa Balozi.
Nina imani wataalamu wa Sheria na Katiba hawakushirikishwa katika jambo hili.
 
Swali:

Hivi Raisi akiteua mtu kuwa mbunge na baadae mtu huyo akajiuzulu ubunge au kupoteza sifa ya kuwa mbunge,idadi ya wabunge walioteuliwa na Raisi inapungua au inabaki pale pale?
yaani hiyo imestick kama superglue,hata akifa jibu ni kuwa alishateuliwa kuwa mbunge na hivyo nafasi ile haiwezi kujioffset eti ateuliwe mwingine,
nafasi ni kumi,tano wa kiume,tano wa kike
 
Ni wapi hapo Katiba imempa uwezo Rais kumvua mtu ubunge aliopewa na Rais? Rais kapewa mamlaka ya kuwateua na kuwatengua watendaji wa Serikali, na si zaidi ya hao...
Mahakama na Bunge ni mihimili isiyo ya serikali. Ndo sababu Rais hawezi kutengua nafasi ya Jaji yeyote hata kama amemteua yeye. Vivyo hivyo kwa Mbunge.
Inatosha kusema tu kuwa Rais ameteleza.
Mbaya zaidi hata njia inayotumika kujisahihisha pia sio sahihi.
Inazidisha matatizo badala ya kuyatatua.
Ni aibu kumteua Mbunge kuwa Balozi.
Nina imani wataalamu wa Sheria na Katiba hawakushirikishwa katika jambo hili.
 
kama anaweza kumteua why asiweze mtengua, ila haitawezekana kwa mbunge wa kuteuliwa na wananchi maana hawako chini ya mamlaka yake, hao wanaweza wajibishwa na wananchi wake. utaratibu wa kuwajibishwa ndo haujaainishwa kikatiba, ila naamini wananchi wakiogornize wakaenda mahakaman na sababu za kueleweka wanaweza mvua ubunge mbunge wao kama vile raisi anavoweza mvua ubunge mteule wake
Ungekaa kimya ungekuwa umejitendea haki!
 
Mh rais hana mamlaka ya kumvua ubunge mbunge yoyote yule.Kitendo cha rais kumteua dr posi kuwa balozi hakiondoi ubunge wake hadi pale atakapo andika barua mwenyewe kwa hiari yake kujiuzulu nafasi take ya ubunge.

Sasa mh posi nakushauri kataa uteuzi wa balozi ubaki kuwa mbunge, ili heshima ya ubunge iendelee kuwepo na watu wasidhani kuwa na wewe umetumbuliwa.
Mpaka anatangazwa alikuwa ameishakubali Kuwa barozi
 
Pamoja na Rais kumteua Mhe. Posi kuwa balozi lakini ubunge wake unabaki pale pale!

Hivyo bado kuna wabunge 6 wa kiume ambao Rais ameteua kinyume cha katiba!!

Katiba imevunjwa huo ndiyo ukweli na hatua za kumwajibisha Rais zinapashwa kuanza kuchukuliwa!!

Rais aliapa kulinda katiba lakini sasa amekiuka! Sheria ni msumeno unakata mbele na nyuma!!!
Hahaha...tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea, hamjasikia kitu nasema....tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea(Tundu Lissu)
 
Ndugu zangu wasalam! Kwa mujibu wa katiba yetu mbovu yenye viraka lukuki(amendments)Rais hana mamlaka ya kutengua uteuzi wa mbunge yeyote hata km alimtea yy,kwa sababu kwa mujibu wa katiba mbunge anaapa mbele ya bunge tukufu la jamhuri ya muungano wa Tanzania na sio rais hivyo mbunge anapoapa anawajibika mbele ya bunge.Rais wetu amevunja katiba hili haliepukiki na tuache siasa za kijinga ndugu zangu watanzania tusiwe wavivu kusoma katiba yetu.
 
Back
Top Bottom