Je, Rais ana mamlaka ya Kumvua Mtu "Ubunge"?

Je, Rais ana mamlaka ya Kumvua Mtu "Ubunge"?

kama anaweza kumteua why asiweze mtengua, ila haitawezekana kwa mbunge wa kuteuliwa na wananchi maana hawako chini ya mamlaka yake, hao wanaweza wajibishwa na wananchi wake. utaratibu wa kuwajibishwa ndo haujaainishwa kikatiba, ila naamini wananchi wakiogornize wakaenda mahakaman na sababu za kueleweka wanaweza mvua ubunge mbunge wao kama vile raisi anavoweza mvua ubunge mteule wake
kifungu namba ngapi cha sheria?
 
Ukiteuliwa kuwa balozi. Then the public Service Act inasema balozi haruhusiwi kichika nyadhifa yoyote ya kisiasa serikalini. Then automatically Possi anatakiwa kujivua ubunge. Pia katiba katika ibara ya 67 (2)g ambayo inakataza maofisa waandamizi wa serikali kuwa wabunge hivyo possi anapoteza sifa ya kuwa mbunge
 
Ukweli ni kwamba rais anamaamlaka ya kumvua mbunge nafasi na kuchagua mwingine mda wowote maana mbunge hana security of tenure ambayo ni kinga waliyonayo watendaji wakiserekali ambao wenye kinga hio hawawezi fukuzwa pasipo kusikilizwa na kufata utaratibu husika
Kifungu gani cha sheria hicho ?
 
ufafanuzi wako ni kwa kutumia busara, kiufupi ni ufafanuz ambao ni kama vile tunataka kuweka tu mambo vizuri. Ni busara lakini haujafafanua katika lugha ya kisheria kwa maana ya kuonyesha vifungu.
Sidhani kama kuna sheria inayopingana na common sense
 
Salaam Wakuu.

Hongereni kwa mijadala mengi humu na mitandao mengine juu ya Swala la Mh Rais kuteua Wabunge Sita jinsia ya Kiume,na baadae Ndg Abdlallah Posi kupangiwa kazi nyingine kama Balozi.

Baada ya yote hayo, naomba kuuliza swali langu moja hapa. " Je, Rais ana mamlaka ya Kumnyang'anya mtu Ubunge?". Hayo mamlaka/ sheria imeandikwa kwenye Ibara/Kifungu gani?

Napenda kusema natambua kuwa Rais ana mamlaka mazito ya kulivunja Bunge zima, ila sina ninalolifahamu juu ya Kumvua mtu Ubunge wake japo ndiye kamteua.

Wataalamu wa Sheria, tusaidieni katika hili. Je, Rais ana mamlaka ya kumvua Mtu Ubunge? Kama jibu ni ndiyo, je ni Ubunge wa Kuteuliwa yaani viti maalum tu au hata Ubunge wa Uwakilishi Jimboni?
hana
 
Wabunge wa kuchaguliwa na wale wanawake viti maalum wanawajibika kwa vyama vyao vilivyowapa tickiti ya gombea au kuwateua vipi maalum. Wale walioteuliwa na rais wanawajibika kwa Rais. Wananchi watuna mamlaka kwa wabunge kama vile tusivyo nayo kwa Rais. Vyama ndio vinatuamulia nani awe mbunge na nani awe Rais sie kazi yetu ni kuamua tunakipa ridhaa chama kipi na watu wake.
 
Pamoja na Rais kumteua Mhe. Posi kuwa balozi lakini ubunge wake unabaki pale pale!

Hivyo bado kuna wabunge 6 wa kiume ambao Rais ameteua kinyume cha katiba!!

Katiba imevunjwa huo ndiyo ukweli na hatua za kumwajibisha Rais zinapashwa kuanza kuchukuliwa!!

Rais aliapa kulinda katiba lakini sasa amekiuka! Sheria ni msumeno unakata mbele na nyuma!!!
 
Mh rais hana mamlaka ya kumvua ubunge mbunge yoyote yule.Kitendo cha rais kumteua dr posi kuwa balozi hakiondoi ubunge wake hadi pale atakapo andika barua mwenyewe kwa hiari yake kujiuzulu nafasi take ya ubunge.

Sasa mh posi nakushauri kataa uteuzi wa balozi ubaki kuwa mbunge, ili heshima ya ubunge iendelee kuwepo na watu wasidhani kuwa na wewe umetumbuliwa.
 
Back
Top Bottom