Je, Rais ana mamlaka ya Kumvua Mtu "Ubunge"?

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,204
15,198
Salaam Wakuu.

Hongereni kwa mijadala mengi humu na mitandao mengine juu ya Swala la Mh Rais kuteua Wabunge Sita jinsia ya Kiume,na baadae Ndg Abdlallah Posi kupangiwa kazi nyingine kama Balozi.

Baada ya yote hayo, naomba kuuliza swali langu moja hapa. " Je, Rais ana mamlaka ya Kumnyang'anya mtu Ubunge?". Hayo mamlaka/ sheria imeandikwa kwenye Ibara/Kifungu gani?

Napenda kusema natambua kuwa Rais ana mamlaka mazito ya kulivunja Bunge zima, ila sina ninalolifahamu juu ya Kumvua mtu Ubunge wake japo ndiye kamteua.

Wataalamu wa Sheria, tusaidieni katika hili. Je, Rais ana mamlaka ya kumvua Mtu Ubunge? Kama jibu ni ndiyo, je ni Ubunge wa Kuteuliwa yaani viti maalum tu au hata Ubunge wa Uwakilishi Jimboni?
 
kama anaweza kumteua why asiweze mtengua, ila haitawezekana kwa mbunge wa kuteuliwa na wananchi maana hawako chini ya mamlaka yake, hao wanaweza wajibishwa na wananchi wake. utaratibu wa kuwajibishwa ndo haujaainishwa kikatiba, ila naamini wananchi wakiogornize wakaenda mahakaman na sababu za kueleweka wanaweza mvua ubunge mbunge wao kama vile raisi anavoweza mvua ubunge mteule wake
 
Rais anayomamlaka ya kumvua Ubunge,Mbunge ambaye amemteua yeye.
 

Attachments

  • FB_IMG_1484854209570.jpg
    FB_IMG_1484854209570.jpg
    64.1 KB · Views: 114
Kwa akili zangu za kidwanzi nazani Raisi awezi. ..kuna watu wawili Rais anaweza kuwateua lakini awezi kuwavua , navyo ni Jaji mkuu na mbunge ...wajuaji watareta vifungu hapa
Uongo, wateuzi wake wote anao uwezo wa kuwatengua
 
Rais anayomamlaka ya kumvua Ubunge,Mbunge ambaye amemteua yeye.
Mkuu, hii kitu umeweka hapa haina ufafanuzi wa kuwa rais ana mamlakani ya kumvua ubunge mbunge wa kuteuliwa. Nacho juwa mimi, mtu akiteuliwa ubunge (na hapa tunazungumzia mbunge wa kuteuliwa) mara baada ya kuapisha na spika, mbunge anakuwa chini ya spika na spika ndio mwenye mamlaka yote ya mbunge kuwa mbunge au la. Na mbunge mwenyewe anauwezo wa kujiuzulu mwenye kama akitaka hivyo. Sidhani kama rais ana mamlaka tena baada ya mbunge kuapishwa.

Ukumbuke pia, mbunge wa kuteuliwa na mbunge wa kuchaguliwa wana mamlaka sawa wanapokuwa bungeni na hata nje ya bunge.
 
kama anaweza kumteua why asiweze mtengua, ila haitawezekana kwa mbunge wa kuteuliwa na wananchi maana hawako chini ya mamlaka yake, hao wanaweza wajibishwa na wananchi wake. utaratibu wa kuwajibishwa ndo haujaainishwa kikatiba, ila naamini wananchi wakiogornize wakaenda mahakaman na sababu za kueleweka wanaweza mvua ubunge mbunge wao kama vile raisi anavoweza mvua ubunge mteule wake
ufafanuzi wako ni kwa kutumia busara, kiufupi ni ufafanuz ambao ni kama vile tunataka kuweka tu mambo vizuri. Ni busara lakini haujafafanua katika lugha ya kisheria kwa maana ya kuonyesha vifungu.
 
Ukweli ni kwamba rais anamaamlaka ya kumvua mbunge nafasi na kuchagua mwingine mda wowote maana mbunge hana security of tenure ambayo ni kinga waliyonayo watendaji wakiserekali ambao wenye kinga hio hawawezi fukuzwa pasipo kusikilizwa na kufata utaratibu husika
 
Back
Top Bottom