Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,360
- 11,514
Jamaa yangu anaishi Makubuli anasema hawa watu wamerudi kwa kasi kubwa,ari na guvu kubwa sana. Wanaweza pora nyumba mpaka 20 kwa usiku mmoja. Ni vijana wa umri wa miaka 12-30 wanakuwa wengi wakiwa na mapanga ,visu ,magongo na bisibisi. Kiukweli wameuteka mji wa Dar es Salaam. Nadhani kwa hiki kipindi ambacho polisi wapo mapumziko tutapata shida sana. Mpaka wakimaliza likizo Polisi hali itakuwa tete. Tuuombe Mungu sana.
Serikali yetu sikivu yenye kutujali na kutupenda je bado hamjapewa hizi habari? yaani kuna watu washavamiw ana kudhuriwa zaidi ya mara tatu na wakiepeleka taarifa polisi wanawaambia "wewe siyo mtu wa kwanza kushambuliwa na hao vibaka andika maelezo tutafuatilia" inaishia hapo. imekuwa ni jambo la kawaida na polisi haw aamabo tunawalipa mshahara wanaonekana kutoshtushwa kabisa na jambo hili. tunaomba serikali kwa kweli iingilie kati suala hili kwa ajili ya usalama wa wapiga kura wake na wachangia kodi.
Jamani sisi wananchi wote tukiuliwa nchini wakabaki panya road penye yao ninyi viongozi nani atawachangia kodi ambayo ndiyo inawasaidia kuzunguka nchini kwenye helkopta kuhamasisha anuani za makazi? au kwenda kuzinduliwa huko Ulaya na Marekani? Tumsaidie Rais wetu jamani mbona kama kila kitu mmemuachia yeye tu. yeye uzinduzi , yeye kusafiri kujielezea, yeye kila kitu ninyi mnafanya nini?