Serikali inapendekeza Kukusanya kodi za majengo kwa kutumia LUKU, najiuliza tuu, vipi nyumba zisizo na umeme.
Je, zimesamehewa kodi ya majengo?
Kuna mtiririko maalum wa ufanyaji na utekelezaji wa maamuzi ya serikali.
1.Waziri husika hupeleka mapendekezo kwenye baraza la mawaziri baada ya mijadala kati ya watendaji na wadau wa sekta husika.
2. Baraza la mawaziri hukubali au hukataa au hurekebisha. Likikubali tunakuja hatua ya 3. Likikataa basi linaishia huko huko kwa siri kuu. Kwa hiyo kuna mengi huwa yanakataliwa ila kwa kuwa ni siri, hatujui.
3. Waziri husika au atakayeagizwa na baraza la mawaziri hupeleka maamuzi hayo bungeni kupitia taarifa za kawaida za serikali, mswada wa sheria au bajeti kuu kama ilivyokuwa kwa case hii.
4. Bunge linaweza kujadili na kukubali au kurekebisha au kukataa(at least theoretically). Likikubali basi tunaenda hatua ya 5, likikataa linarudi kwa waziri na BLW kufanya mabadiliko.
5. Waziri huandaa kanuni au miongozo ya utekelezaji wa maamuzi hayo.
6. Waziri huweka hadharani kanuni hizo na kuwapa watendaji wakuu wa wizara, idara au taasisi za serikali zinazopaswa kutekeleza maagizo hayo.
7. Watendaji wakuu wa MDAs kila mmoja kwa capacity yake huandika waraka kwa watendaji walioko chini yao na pengine kwa wadau wakuu wa sekta husika kuelezea namna ya utekelezaji wa sheria, miongozo au maamuzi au maagzio hayo ya serikali.
Kwa hiyo hotuba ya bungeni haitekelezwi moja kwa moja kama ilivyo wasilishwa na waziri. Yaweza pia kutekelezwa kama haihitaji muongozo.