Je,nitakuwa nimekosea kufanya hivi?

Beesmom

JF-Expert Member
May 30, 2016
17,202
28,709
Salamu?
Nakumbuka nishawai leta mada kuhusu mwanaume kufanya nae makubaliano ya kuzaa then ndo tuoane....lakin mwenzangu akaja kubadilika na kusema nitoe mimba.

Kiufupi ni kwamba nimelea mtoto amekua ana miaka miwili....sasa ninachoogopa ni siku moja kuja kumpoteza mikononi mwangu huyu mtoto...maana nilisikia watoto wa kiume wakikua ni lazima atamtaka baba yake.

Nitakuwa nimefanya kosa kumzuia huyu mwanangu kumwambia ukweli kwamba bila mimi usingezaliwa coz baba ako alisema nikuue ungali tumbon wiki tatu?

Mi nampenda mwanangu....nimeangaika nae sana sitaki nimpoteze au awe mbali na Mimi...ni bora achukue mama yangu mzazi kuliko kwenda kwa babae ambaye alitukataa.
Ushauri wenu tafadhali
 
Hakuna sababu ya kumficha ili asimjue baba yake, ni haki yake lakini pia usimuumize mtoto kisaikolojia eti baba yake alitaka mimba itolewe...

Wazazi wanaficha mengi saana ili kuwaepusha watoto wao wasiumie kisaikolojia...

Akitaka kumjua baba yake mruhusu, hiyo dhambi ya babake ataibeba mwenyewe. Nafsi yake itamsuta kuona unaruhusu mwanao amtambue ka babake...
 
Usiwe na hofu kwa kitu ambacho bado hakijatokea

Kwani baba wa mtoto bado mnawasiliana?yupo karibu?anafahamu mtoto alizaliwa?

Kama ikitokea ikawa baba akahitaji mtoto sheria zipo

Alafu mbona mi nasikia watoto wa kiume wengi wanapenda zaidi uwepo wa momma
 
Mambo yako na baba yake yanamuhusu nini, mwache aishi maisha yake msipende kuhamisha visasi vyenu kwa watoto
 
Kama unataka Mungu akusamehe dhambi zako za hapa duniani, basi na ww jifunze kusamehe. Achana na Chuki. Ukishindwa kumsamehe binadamu mwenzako usitegemee mungu ataweza kukusamehe ww
Ila daaa,basi tu
 
Hakuna sababu ya kumficha ili asimjue baba yake, ni haki yake lakini pia usimuumize mtoto kisaikolojia eti baba yake alitaka mimba itolewe...

Wazazi wanaficha mengi saana ili kuwaepusha watoto wao wasiumie kisaikolojia...

Akitaka kumjua baba yake mruhusu, hiyo dhambi ya babake ataibeba mwenyewe. Nafsi yake itamsuta kuona unaruhusu mwanao amtambue ka babake...
Aisee,maisha haya.Asante mine
 
Usiwe na hofu kwa kitu ambacho bado hakijatokea

Kwani baba wa mtoto bado mnawasiliana?yupo karibu?anafahamu mtoto alizaliwa?

Kama ikitokea ikawa baba akahitaji mtoto sheria zipo

Alafu mbona mi nasikia watoto wa kiume wengi wanapenda zaidi uwepo wa momma
nilivokataa kuitoa alisusia...alisikia nimejifungua but mpaka Leo haifahamu hata sura ya mwanae.Hashtuki kiufupi
 
Sioni haja ya wewe kuweka uadui kati yake na baba yake. We mlee maana kama si vyema kumjaza mtoto chuki kwa umri mdogo hivyo.
 
Usijidanganye dada angu swala la kumficha mtu babake,, Kwanza lazima ajue hata ukimficha hii dunia haina siri mama na kama unalitambua hilo usiendelee kuharibu uhusiano kati ya baba na mwanae.,,!! Kutomwambia au kumchafua baba bado haifuti historia,, cha msingi huu ndo wakati wako mwafaka wa kuimarisha uhusiano kati ya baba na mtoto kama ilishindkana wakati uko mjamzito..!!!

Mu impanct mwanao roho ya msamaha sio gharama ni bure mamaa.,, Ndo dunia ya leo ilivyo,wengi wana roho za kiuaji ka ya huyo boyfriend wako, unaweza ukamkomalia mwanao ajaze chuki wakat naye cku moja atawakimbia mabinti ukishawajaza vijusi..,,
 
Asante sana ndugu yangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom