Je, niliyestushwa na hii kauli 'tata' ya Naibu Katibu Mkuu CCM Mpogole ni peke yangu tu au tupo wengi? Mama kuwa makini sana!

Mimi nimeambulia hili "Mfariji Mkuu kwa Viongozi wa CCM pamoja na Wanachama ". nilivyoelewa ni kwamba atakuwa comforter in chief wa viongozi na wanachama, ikimaanisha aliyeondoka alikuwa kinyume, yaani alikuwa "demonizer in chief" wa viongozi na wanachama.
Mimba changa
Siyo kwa sababu wewe una mimba changa basi kila mwenye mawazo tofauti na wewe ana mimba changa pia
Ungetuliza mshono usingepata hiyo mimba na kutematema mate hovyo na kujiharishia
 
Unamshauri vibaya mama unataka awaondoe akina Mangula na wenzeka kama alivyofanya JK,karibia CCM imfie mikononi.

JPM ndo alirudisha uhai wa chama hata kama ana mapungufu yake.

Kumtaka mama afanye hivyo humtakii mema mama! Anaweza fanya marekebisho kwa wachache.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mangula abaki ila nimuhimu afanye mabadiliko Tena makubwa hasa kwene sekretariet, pamoja na yoye JPM iliyengeneza mfumo ambao haukuwa na afya Sana Kuna watu ambao waliamini wao ndo wao na wakamfanya yeye Kama mungu mtu kiukweli pamoja na yte ccm chini ya magufuli ilikuwa na simanzi na majonzi kwa walio wengi
 
" Uchaguzi Mkuu halali Kikatiba CCM tutaufanya mwakani 2022 ila huu wa leo ni wa Kuziba tu nafasi na hata Rais Mama Samia akishika hatamu atakuwa ni Mfariji Mkuu kwa Viongozi wa CCM pamoja na Wanachama wote ndani na nje ya nchi "

Ukitulia kabisa, Kuichambua na hata Kuidadavua vyema hii Kauli ya Naibu Katibu Mkuu CCM Ndugu Rodrick Mpogole utagundua kuwa huenda Mama Samia (Rais) anaona anakubalika na wana CCM Waandamizi nyusoni Kwao ila Mioyoni mwao wala hayupo kabisa.

Ushauri pekee (tena wa bure) kabisa ambao nampa Mama ( Rais Samia ) kuwa akipewa tu 'Dhamana' ya Uenyekiti leo na CCM basi 'awafagie' Waandamizi wote waliokuwepo kwani kuna Hatari kubwa ya kwenda nao hadi hiyo mwakani wanaweza wakamdhoofisha na hata Kumuharibia ndani ya Chama.

Mwenyekiti mpya wa CCM (Rais Mama Samia) anatakiwa ajue kuwa CCM anayoipokea sasa ( leo ) ina Mpasuko mkubwa, Majungu na Fitina za chini chini mpaka Usaliti pia Sumu ambayo ilienziwa vyema ndani ya Chama na aliyekuwa Mwenyekiti Taifa ( sasa Hayati ) hivyo asiamini walio karibu nae na aanze na Timu yake (Kikosi chake) ili asikwame.

Kazi yangu kubwa GENTAMYCINE ni kufanya tu Critical Observation juu ya Situation fulani ambayo naiona ina ulakini na Kushauri kwa nia njema tu. Mabadiliko makubwa sana na ya haraka mno yanahitajika katika CCM ya Mwenyekiti Mtarajiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Nawatakia Wajumbe (Wapiga Kura) wote 1,862 (99%) waliopo Ukumbini sasa Kila la Kheri katika Mkutano huu Muhimu na wa Dharula ndani ya Chama (CCM) japo sina uhakika sana kama baada ya Hayati Rais Dkt. Magufuli kutangulia mbele ya Haki CCM iliyopo sasa iko United na kuna Upendo pia.
Kesha wafurusha wote mkuu
 
Wewe umefuata nini hapo na wakati siyo mjumbe?
Woote mnaongea as if mama peke yake ana mvuto kwa wana CCM!

Hivi kati ya mama yenu na hao waandamizi ndani ya #CCM ni nani ana mvuto wa kukiweka chama mahali pake?

Hao kina Nchimbi,Kikwete,Nape,na vurugu zao zingine si ndio hao waliokuwa tayari wamekiuwa chama?

Kuna mambo ndani ya #CCM akiyapindisha sasa hivi itakigharimu chama hicho vibaya sana 2025.

Sio mnaongea tu,utadhani mnaoongelea CHADEMA.

#CCM ni kitu ingine..
Samia apambane tu kurejesha umoja wa kitaifa vyama hupita ila Taifa ni lazima liwr imara na lenye amani bila shaka ccm chini ya JPM pamoja na yte ililikosea Sana Taifa
 
" Uchaguzi Mkuu halali Kikatiba CCM tutaufanya mwakani 2022 ila huu wa leo ni wa Kuziba tu nafasi na hata Rais Mama Samia akishika hatamu atakuwa ni Mfariji Mkuu kwa Viongozi wa CCM pamoja na Wanachama wote ndani na nje ya nchi "

Ukitulia kabisa, Kuichambua na hata Kuidadavua vyema hii Kauli ya Naibu Katibu Mkuu CCM Ndugu Rodrick Mpogole utagundua kuwa huenda Mama Samia (Rais) anaona anakubalika na wana CCM Waandamizi nyusoni Kwao ila Mioyoni mwao wala hayupo kabisa.

Ushauri pekee (tena wa bure) kabisa ambao nampa Mama ( Rais Samia ) kuwa akipewa tu 'Dhamana' ya Uenyekiti leo na CCM basi 'awafagie' Waandamizi wote waliokuwepo kwani kuna Hatari kubwa ya kwenda nao hadi hiyo mwakani wanaweza wakamdhoofisha na hata Kumuharibia ndani ya Chama.

Mwenyekiti mpya wa CCM (Rais Mama Samia) anatakiwa ajue kuwa CCM anayoipokea sasa ( leo ) ina Mpasuko mkubwa, Majungu na Fitina za chini chini mpaka Usaliti pia Sumu ambayo ilienziwa vyema ndani ya Chama na aliyekuwa Mwenyekiti Taifa ( sasa Hayati ) hivyo asiamini walio karibu nae na aanze na Timu yake (Kikosi chake) ili asikwame.

Kazi yangu kubwa GENTAMYCINE ni kufanya tu Critical Observation juu ya Situation fulani ambayo naiona ina ulakini na Kushauri kwa nia njema tu. Mabadiliko makubwa sana na ya haraka mno yanahitajika katika CCM ya Mwenyekiti Mtarajiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Nawatakia Wajumbe (Wapiga Kura) wote 1,862 (99%) waliopo Ukumbini sasa Kila la Kheri katika Mkutano huu Muhimu na wa Dharula ndani ya Chama (CCM) japo sina uhakika sana kama baada ya Hayati Rais Dkt. Magufuli kutangulia mbele ya Haki CCM iliyopo sasa iko United na kuna Upendo pia.

TKO tena kama ilivyokuwa kwa Makamo wa Rais. Yote ni maisha.
 
Acha kujidanganya CCM ni moja wala hawezi kugawanyika
Tatizo kubwa la Hayati alitaka kufanya chama kama mali yake binafsi, kama vile alivyokwisha jimilikisha nchi kuwa ni yake pekee. katika ile process ya kujimilikisha ilibidi kuweka watu wake ambao aliwaaminisha kuwa watakuwa wanufaika wake milele.

Kufa kwake ghafla zaidi ya simanzi kwa wafuasi wake, kumeleta hasira zaidi. Hasira ya kupokonywa tonge kinywani. Japo mama hausiki na kudra ya Mungu kutuondoshea Mwendazake, kuchukua kwake nafasi kuu kumemfanya achukiwe na waliobaki kwa kuwa hakujua mikakati iliyokuwepo kwa manufaa yao.

Tutasikia hoja nyingi zisizo na mashiko dhidi ya mama ili tu kumtoa nje ya reli. Sitostaajabu Muungano pia ukavunjika safari hii ili tu mama asiendelee kuwepo alipo sasa.
 
Mwendazake ametangulia mbele ya hukumu. Alijiamini sana lakini ndiyo hivyo tena. Hakuna ajuaye kesho yake.
 
Back
Top Bottom