Je, niliyestushwa na hii kauli 'tata' ya Naibu Katibu Mkuu CCM Mpogole ni peke yangu tu au tupo wengi? Mama kuwa makini sana!

Kwani uongo?

Huyo Ni rais wa kusimika tu sio wa kupitia sanduku la kura.

Halafu tuko kwenye awamu tano bado huyu kakaimu tu.
Mawazo ya mjinga mmoja asiye jua chochote kuhusu katiba inasema nini ila anajifanya kujua, poleni chuma chenu kimesha liwa na funza huko msitupigie kelele zenu
 
Apange safu yake tuu hata huyo mpogolo anajifariji tuu ikibidi fukuza vinginevyo watakusumbua but najua JK mzee wa mipango atamsaidia kuweka mambo sawa.
 
Unamshauri vibaya mama unataka awaondoe akina Mangula na wenzeka kama alivyofanya JK,karibia CCM imfie mikononi.

JPM ndo alirudisha uhai wa chama hata kama ana mapungufu yake.

Kumtaka mama afanye hivyo humtakii mema mama! Anaweza fanya marekebisho kwa wachache.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkuu naomba nitofautiane na wewe kidogo kuhusu hilo la pili. Ni kweli CCM ilianza kuyumba enzi za JK kwani aliondoa Baraza la ushauri na kupunguza nguvu ya Halmashauri Kuu ya chama ambayo ni chombo pekee kinachotunga sera zitakazotekelezwa na serikali ya CCM. Pili aliingiza kwenye Kamati Kuu ya CCM watu ambao hawakuwa na uzoefu katika uendeshaji wa chama ( party political organisation). Matokeo yake ndiyo hayo ya JK kuona CCM inakufa, akaitwa Kinana, Nape wakashirikiana na Mangula kuokoa jahazi.

Awamu ya Tano CCM ilizidi kudhoofika sana kwa sababu zifuatazo;
1. Halmashauri Kuu ikazidi kupungunzwa nguvu kwa kupunguza idadi kubwa ya wajumbe wake na vikao vyake vikawa ni vya siku moja au mbili tu.
2. Uingizaji wa wanachama kiholela bila kuwasaili kujua kama wanaijua na wanaikubali ITIKADI ya CCM. Mfano ni Polepole na Bashiru na wengine wengi kiasi cha kwamba CCM Maslahi ni wengi zaidi kuliko CCM Asilia.

Kwa kumalizia, CCM kama chama cha siasa kiko hoi bin taabani. Kimepoteza ule moyo wake wa kiitikadi. Ni wakati sahihi wa Mwenyekiti Mpya kuiangalia hali hii kwa makini aanze kukijenga upya chama aondoe mamluki na CCM maslahi wote, aunde Sekretariet mpya iogozwe na makada wazoefu, airudishie nguvu na heshima Halmashauri Kuu na Kuimarisha uongozi na uendeshaji wa chama kutoka ngazi ya Matawi hadi Taifa.
 
Mimi nimeambulia hili "Mfariji Mkuu kwa Viongozi wa CCM pamoja na Wanachama ". nilivyoelewa ni kwamba atakuwa comforter in chief wa viongozi na wanachama, ikimaanisha aliyeondoka alikuwa kinyume, yaani alikuwa "demonizer in chief" wa viongozi na wanachama.
Hahahahah daah
 
Good
 
Mimba changa
 
" Uchaguzi Mkuu halali Kikatiba CCM tutaufanya mwakani 2022 ila huu wa leo ni wa Kuziba tu nafasi na hata Rais Mama Samia akishika hatamu atakuwa ni Mfariji Mkuu kwa Viongozi wa CCM pamoja na Wanachama wote ndani na nje ya nchi "

Ukitulia kabisa, Kuichambua na hata Kuidadavua vyema hii Kauli ya Naibu Katibu Mkuu CCM Ndugu Rodrick Mpogole utagundua kuwa huenda Mama Samia ( Rais ) anaona anakubalika na wana CCM Waandamizi nyusoni Kwao ila Mioyoni mwao wala hayupo kabisa.

Ushauri pekee ( tena wa bure ) kabisa ambao nampa Mama ( Rais Samia ) kuwa akipewa tu 'Dhamana' ya Uenyekiti leo na CCM basi 'awafagie' Waandamizi wote waliokuwepo kwani kuna Hatari kubwa ya kwenda nao hadi hiyo mwakani wanaweza wakamdhoofisha na hata Kumuharibia ndani ya Chama.

Mwenyekiti mpya wa CCM ( Rais Mama Samia ) anatakiwa ajue kuwa CCM anayoipokea sasa ( leo ) ina Mpasuko mkubwa, Majungu na Fitina za chini chini mpaka Usaliti pia Sumu ambayo ilienziwa vyema ndani ya Chama na aliyekuwa Mwenyekiti Taifa ( sasa Hayati ) hivyo asiamini walio karibu nae na aanze na Timu yake ( Kikosi chake ) ili asikwame.

Kazi yangu kubwa GENTAMYCINE ni kufanya tu Critical Observation juu ya Situation fulani ambayo naiona ina ulakini na Kushauri kwa nia njema tu. Mabadiliko makubwa sana na ya haraka mno yanahitajika katika CCM ya Mwenyekiti Mtarajiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Nawatakia Wajumbe ( Wapiga Kura ) wote 1,862 ( 99% ) waliopo Ukumbini sasa Kila la Kheri katika Mkutano huu Muhimu na wa Dharula ndani ya Chama ( CCM ) japo sina uhakika sana kama baada ya Hayati Rais Dkt. Magufuli kutangulia mbele ya Haki CCM iliyopo sasa iko United na kuna Upendo pia.
Mawazo yako at face value.
 
Ndani ya CCM kuna shida.

Anaetakiwa kubaki ni huyu mzee Mangula wengine wote wakuondoa.

Chama kirudi kwa Nchimbi, Nape, January.

Kinyume na hivyo, Mh. Mama Samia ana kwenda kufanyiwa zengwe.
Ramli huwa hazijibu
 
Atakaposuka kikosi chake ataanzisha chuki nyingine ya wazi ambayo sasa kwake nayo itamsumbua kuliko wanaojificha na kusemea pembeni bila madhala kuluko kujitengenezea madhala yeye mwenyewe.
 
Unamshauri vibaya mama unataka awaondoe akina Mangula na wenzeka kama alivyofanya JK,karibia CCM imfie mikononi.

JPM ndo alirudisha uhai wa chama hata kama ana mapungufu yake.

Kumtaka mama afanye hivyo humtakii mema mama! Anaweza fanya marekebisho kwa wachache.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Umenistua aisee. Usiwe unataja taja huyo shetani
 
Woote mnaongea as if mama peke yake ana mvuto kwa wana CCM!

Hivi kati ya mama yenu na hao waandamizi ndani ya #CCM ni nani ana mvuto wa kukiweka chama mahali pake?

Hao kina Nchimbi,Kikwete,Nape,na vurugu zao zingine si ndio hao waliokuwa tayari wamekiuwa chama?

Kuna mambo ndani ya #CCM akiyapindisha sasa hivi itakigharimu chama hicho vibaya sana 2025.

Sio mnaongea tu,utadhani mnaoongelea CHADEMA.

#CCM ni kitu ingine..
 
Mimi nimeambulia hili "Mfariji Mkuu kwa Viongozi wa CCM pamoja na Wanachama". nilivyoelewa ni kwamba atakuwa comforter in chief wa viongozi na wanachama, ikimaanisha aliyeondoka alikuwa kinyume, yaani alikuwa "demonizer in chief" wa viongozi na wanachama.
1619779295743.png
 
Unamshauri vibaya mama unataka awaondoe akina Mangula na wenzeka kama alivyofanya JK,karibia CCM imfie mikononi.

JPM ndo alirudisha uhai wa chama hata kama ana mapungufu yake.

Kumtaka mama afanye hivyo humtakii mema mama! Anaweza fanya marekebisho kwa wachache.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
JPM hakurudisha uhai wa CCM. Alichofanya ni kutumia vyombo vya dola kufanya siasa yeye peke yake na CCM na kuzuia vyama vingine kufanya siasa.

Alizuia vyama vya upinzani kufanya siasa na kuwafanyia viongozi na wanachama wa vyama hivyo kila aina ya hujuma inayoweza kufanywa duniani!
 
Woote mnaongea as if mama peke yake ana mvuto kwa wana CCM!

Hivi kati ya mama yenu na hao waandamizi ndani ya #CCM ni nani ana mvuto wa kukiweka chama mahali pake?

Hao kina Nchimbi,Kikwete,Nape,na vurugu zao zingine si ndio hao waliokuwa tayari wamekiuwa chama?

Kuna mambo ndani ya #CCM akiyapindisha sasa hivi itakigharimu chama hicho vibaya sana 2025.

Sio mnaongea tu,utadhani mnaoongelea CHADEMA.

#CCM ni kitu ingine..
Unaropoka pumba tu!

Ficha chuki zako kwa mama. Yeye ndiye raisi wa JMT na mwenyekiti wa CCM. Watanzania tunampenda. WanaCCM tunampenda!
 
Back
Top Bottom