Je, niliyestushwa na hii kauli 'tata' ya Naibu Katibu Mkuu CCM Mpogole ni peke yangu tu au tupo wengi? Mama kuwa makini sana!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
" Uchaguzi Mkuu halali Kikatiba CCM tutaufanya mwakani 2022 ila huu wa leo ni wa Kuziba tu nafasi na hata Rais Mama Samia akishika hatamu atakuwa ni Mfariji Mkuu kwa Viongozi wa CCM pamoja na Wanachama wote ndani na nje ya nchi "

Ukitulia kabisa, Kuichambua na hata Kuidadavua vyema hii Kauli ya Naibu Katibu Mkuu CCM Ndugu Rodrick Mpogole utagundua kuwa huenda Mama Samia (Rais) anaona anakubalika na wana CCM Waandamizi nyusoni Kwao ila Mioyoni mwao wala hayupo kabisa.

Ushauri pekee (tena wa bure) kabisa ambao nampa Mama ( Rais Samia ) kuwa akipewa tu 'Dhamana' ya Uenyekiti leo na CCM basi 'awafagie' Waandamizi wote waliokuwepo kwani kuna Hatari kubwa ya kwenda nao hadi hiyo mwakani wanaweza wakamdhoofisha na hata Kumuharibia ndani ya Chama.

Mwenyekiti mpya wa CCM (Rais Mama Samia) anatakiwa ajue kuwa CCM anayoipokea sasa ( leo ) ina Mpasuko mkubwa, Majungu na Fitina za chini chini mpaka Usaliti pia Sumu ambayo ilienziwa vyema ndani ya Chama na aliyekuwa Mwenyekiti Taifa ( sasa Hayati ) hivyo asiamini walio karibu nae na aanze na Timu yake (Kikosi chake) ili asikwame.

Kazi yangu kubwa GENTAMYCINE ni kufanya tu Critical Observation juu ya Situation fulani ambayo naiona ina ulakini na Kushauri kwa nia njema tu. Mabadiliko makubwa sana na ya haraka mno yanahitajika katika CCM ya Mwenyekiti Mtarajiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Nawatakia Wajumbe (Wapiga Kura) wote 1,862 (99%) waliopo Ukumbini sasa Kila la Kheri katika Mkutano huu Muhimu na wa Dharula ndani ya Chama (CCM) japo sina uhakika sana kama baada ya Hayati Rais Dkt. Magufuli kutangulia mbele ya Haki CCM iliyopo sasa iko United na kuna Upendo pia.
 
Mimi nimeambulia hili "Mfariji Mkuu kwa Viongozi wa CCM pamoja na Wanachama". nilivyoelewa ni kwamba atakuwa comforter in chief wa viongozi na wanachama, ikimaanisha aliyeondoka alikuwa kinyume, yaani alikuwa "demonizer in chief" wa viongozi na wanachama.
 
Tatizo kubwa la Hayati alitaka kufanya chama kama mali yake binafsi, kama vile alivyokwisha jimilikisha nchi kuwa ni yake pekee. katika ile process ya kujimilikisha ilibidi kuweka watu wake ambao aliwaaminisha kuwa watakuwa wanufaika wake milele.

Kufa kwake ghafla zaidi ya simanzi kwa wafuasi wake, kumeleta hasira zaidi. Hasira ya kupokonywa tonge kinywani. Japo mama hausiki na kudra ya Mungu kutuondoshea Mwendazake, kuchukua kwake nafasi kuu kumemfanya achukiwe na waliobaki kwa kuwa hakujua mikakati iliyokuwepo kwa manufaa yao.

Tutasikia hoja nyingi zisizo na mashiko dhidi ya mama ili tu kumtoa nje ya reli. Sitostaajabu Muungano pia ukavunjika safari hii ili tu mama asiendelee kuwepo alipo sasa.
 
Ndani ya CCM kuna shida.

Anaetakiwa kubaki ni huyu mzee Mangula wengine wote wakuondoa.

Chama kirudi kwa Nchimbi, Nape, January.

Kinyume na hivyo, Mh. Mama Samia ana kwenda kufanyiwa zengwe.
Kiukweli watu wengi wa Magufuli ni wanafiki. Alikuwa anawaweza yeye mwenyewe tu! Akiwaamini kufanya nao kazi basi ajue imekula kwake!
 
Unamshauri vibaya mama unataka awaondoe akina Mangula na wenzeka kama alivyofanya JK,karibia CCM imfie mikononi.

JPM ndo alirudisha uhai wa chama hata kama ana mapungufu yake.

Kumtaka mama afanye hivyo humtakii mema mama! Anaweza fanya marekebisho kwa wachache.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Kwani uongo?

Huyo Ni rais wa kusimika tu sio wa kupitia sanduku la kura.

Halafu tuko kwenye awamu tano bado huyu kakaimu tu.
 
Back
Top Bottom