Kipindi cha uongozi wa Kikwete nchi ilikuwa na mwelekeo wake hali kadhalika kipindi cha Magufuli kulikuwa na mwelekeo mwingine mpya ambao nadhani kila mtu ulimuweka katika mazingira ambayo hakuyazoea
Kipindi cha JK, mafisadi waliogopewa kuguswa kwa sababu ya serikali kuhofia kuwa nchi itayumba iwapo mafisadi wataguswa! Lakini ni kipindi pia ambacho nchi ilishihudia ufisadi mkubwa na ufujaji wa mali za wananchi, huu nao ulikuwa ni mfumo wa aina yake
Tofauti na ilivyokuwa kwa Magufuli, Serikali yake haikuangalia madhara iwapo mafisadi na wahujumu uchumi wakiguswa
Hiyo yote ni kujaribu kuipeleka nchi katika mwelekeo mpya! Na hoja inaanzia hapo!
Kutokana na sababu zinazotelewa kila mara na viongozi wetu mbalimbali ktk Karibu kila idara kuwa wanajenga mifumo iliyoharibiwa!
Maana yake ni kwamba, mifumo iliyoharibiwa na serikali iliyoongozawa na JPM inayo jengwa sasa, bila shaka ni ili mifumo ya enzi ya JK ambayo kila mtanzania wa enzi hizo anaikumbuka vizuri! Ni pamoja na kuruhusu ubabe wa watu waliojiita unanijua mimi? Ama kurejeshwa kwa wale mafisadi ambao ilikuwa ni dhambi kuguswa na kwamba wakiguswa nchi itayumba? Na au uzembe makazini iwe ruksa? Na ama ule mtindo mtu anafuatilia cheti cha mwanaye aambiwe njoo kesho mara mwaka ili tu atoe Rushwa?
Kidiplomasia ya uchumi na uhusiano kimataifa!
Bila ya shaka kila mtu aweza kuelezea kwa namna yake, lakini kwa ujumla wake ukiwalingani hawa wawili, kuna ukweli kwamba, Diplomasia ya kipindi cha uongozi wa Kikwete ulikuwa ni mzuri na kipindi cha JPM haukuwa mzuri sana! Na hapo kunaweza kuwapo na sababu za kwa nini Diplomasia ya JK ilikuwa imara na Diplomasia ya uongozi wa JPM haikuwa imara kama kipindi cha JK
Mifumo ambao JPM aliiharibu inayojengwa sasa ni ipi? Ni pamoja na kukomesha rushwa nchini ambayo ilikuwa imeota kila pahala, kukomesha ufisadi na uzembe makazini ambapo enzi hizo ilikuwa ndio sifa ya kila mtu aliyeko serikalini? Ama ni mifumo ipi iliyoharibiwa inayojaribu kuundwa upya sasa!
Hizo yaweza kuwa ni hisia zangu, lakini nibaki kwenye kwenye hoja ya msingi kwamba, mfumo sahihi na mwelekeo wa matokeo mazuri katika nchi yetu ambao uliokuwepo enzi za uongozi wa JK na ambao ulianzishwa na alitemfuata JPM upi ambao ungeweza kuleta matokeo mazuri?