Mzee Kikwete alikuwa na damu ya Kunguni? (Gundu) hali ilivyo sasa

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,942
4,131
Kipindi cha JK, hadi watoto wa primary waliandamana eti nao wanadai haki yao, wanavyuo, vyama pinzani, mpaka wabadini nao waliandamana kudai haki zao

Inashangaza sana

Nakumbuka 2013 nilikuwa kwenye viunga vya Bagamoyo, na kipindi hiko mgao wa umeme ulikuwa umepamba moto sana kiasi cha wananchi kutaka kugeuza nyaya za umeme kuanikia nguo

Sasa bhana, Tanesco walikuwa wmezoea kukata umeme kila siku za Ijumaa muda wa Ibada za Dini

Nalisikia sauti nyingi kwenye nyumba ya kuabidia zikisema kwa vitisho, Ole wenu Tanesco wiki ijayo mkate umeme, hiyo ofsi yenu haitatosha, tutawachomoa mmoja baada ya mwingine

Mmezoea sana, siku ya Ibada ya wenzetu hamkati muda wao wa Ibada iweje iwe kwetu tu?

Tokea hapo Tanesco ya Bagamoyo, walitii sauti za wananchi

Mambo yalivyo sasa kwenye eneo la Nishati hii, ni sawa tu na kipindi cha JK

Wale wale waliokuwa wakimpigia kelele JK, Leo huwaambii chochote kuhusu uongozi uliopo leo, Umeme siku za Ibada unakatika tu na hakuna kelele, vipaza sauti vya kuitia watu hekaluni mwao, havitumiki sasa, wanatumia midomo yao

Hii inatufundisha nini? Mbona kwa Kikwete walikuwa wakali kama simba? Leo kuna nini na mambo yanaharibika zaidi?

JK alikuwa na damu ya Kunguni au ni nini kinawafurahisha zaidi wananchi wale wale waliokuwa tayari kuandamana kudai umeme kipindi cha JK na sasa huwaambii kitu hata kama mambo yataharibika zaidi

Hili la umeme, kiukweli linachosha sana kuliwaza, mambo mengi sana yanaharibika, biadhara zunadolola, Ibada haziendi sawa n.k
 
Nafurahi sana kuona watu wanalalama kudadadeki maana mijitu haina shukrani.

Tanesco kataa.

Dawasa mwezi wa nne sasa hawana vifaa vya kufungia watu maji....safiiiii

Barabara ya kimara hadi kibaha hadi leo iko vilevile 3 years down the line hata taa za kupunguza giza haziwekwi..na mwendokasi njia zake zinaota nyasi.....saaaafii

Sukari saizi elfu 4 ....saaafi

Kuhudumiwa ofisi za umma siku hizi ni kama unapewa favour....safiiiiii
 
Mwisho wa siku nusu wapoteze madaraka 2015..sasa hivi wamejifunza,wanatunyoosha kbla hata hayo mawazo hayajaja
 
Nafurahi sana kuona watu wanalalama kudadadeki maana mijitu haina shukrani.

Tanesco kataa.

Dawasa mwezi wa nne sasa hawana vifaa vya kufungia watu maji....safiiiii

Barabara ya kimara hadi kibaha hadi leo iko vilevile 3 years down the line hata taa za kupunguza giza haziwekwi..na mwendokasi njia zake zinaota nyasi.....saaaafii

Sukari saizi elfu 4 ....saaafi

Kuhudumiwa ofisi za umma siku hizi ni kama unapewa favour....safiiiiii
Yes mpaka akili ziwakae sawa
 
Back
Top Bottom