Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,230
- 6,471
Habari zenu wadau wa JF siasa.
Niende madani hapo juu.
Jana nilikaa na kufanya maongezi hapa na pale na kada mzoefu ndani ya CCM. Moja ya jambo la kushangaza aliloniambia ni kuwa Magufuli akimaliza muda wake 2025, hawa tunawadhania kuwa wagombea urais hawatagombea.
Nikamuuliza kulikoni? Akasema watajitokeza hao na wengine wengi na watavunja rekodi hata kufika 100 ila mgombea urais CCM 2025 ni Katibu Mkuu wa sasa Dr Bashiru Ally Kakurwa.
Nikamwambia ana uhakika gani? Aksema watu wengi ndani ya chama hasa aliowaleta Rais Magufuli wana mitazamo eti kuwa wagombea wengine ni wanyonyaji na wamejaa tamaa ya Mali na hivyo katibu mkuu ni chaguo kwao kwani inaaminika ni MJAMAA zaidi ya Nyerere.
Kutokana na kuonekana mjamaa anaaminika kuikomboa nchi.
Nikamuuliza mbona siasa za ujamaa za Mwalimu zimetuacha makapuku Bashiru naye si atatupeleka huko? Akadai siasa za Nyerere ni nzuri ila vita vya Iddi Amin au vita vya Kagera 1978 hadi 1979 ndizo zilivuruga na kuharibu maendeleo ya uchumi uliojengwa kijamaa.
Baada ya hapo nikamuuliza kivipi? Akasema vile vita licha ya kugharimu roho za watu pia ziliigharimu Tanzania US dollars million 500 kipindi hicho.
Nilichoka nikaondoka zangu na siamini kama hili litatokea. Kwanza Siasa za nchi hii hazitabiriki na huenda 2025 Dr Bashiru atakuwa chuoni akifundisha na Katibu Mkuu ni Mwananzengo Fulani.