Je, ni kweli mgombea Urais CCM 2025 ni Dr. Bashiru Ally Kakurwa?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
Habari zenu wadau wa JF siasa.

Niende madani hapo juu.
Jana nilikaa na kufanya maongezi hapa na pale na kada mzoefu ndani ya CCM. Moja ya jambo la kushangaza aliloniambia ni kuwa Magufuli akimaliza muda wake 2025, hawa tunawadhania kuwa wagombea urais hawatagombea.

Nikamuuliza kulikoni? Akasema watajitokeza hao na wengine wengi na watavunja rekodi hata kufika 100 ila mgombea urais CCM 2025 ni Katibu Mkuu wa sasa Dr Bashiru Ally Kakurwa.

Nikamwambia ana uhakika gani? Aksema watu wengi ndani ya chama hasa aliowaleta Rais Magufuli wana mitazamo eti kuwa wagombea wengine ni wanyonyaji na wamejaa tamaa ya Mali na hivyo katibu mkuu ni chaguo kwao kwani inaaminika ni MJAMAA zaidi ya Nyerere.

Kutokana na kuonekana mjamaa anaaminika kuikomboa nchi.
Nikamuuliza mbona siasa za ujamaa za Mwalimu zimetuacha makapuku Bashiru naye si atatupeleka huko? Akadai siasa za Nyerere ni nzuri ila vita vya Iddi Amin au vita vya Kagera 1978 hadi 1979 ndizo zilivuruga na kuharibu maendeleo ya uchumi uliojengwa kijamaa.

Baada ya hapo nikamuuliza kivipi? Akasema vile vita licha ya kugharimu roho za watu pia ziliigharimu Tanzania US dollars million 500 kipindi hicho.

Nilichoka nikaondoka zangu na siamini kama hili litatokea. Kwanza Siasa za nchi hii hazitabiriki na huenda 2025 Dr Bashiru atakuwa chuoni akifundisha na Katibu Mkuu ni Mwananzengo Fulani.
 
Hili jukwaa la siasa, usipite nenda majukwaa yenye maisha bora kwa familia yako. Kumbuka tu hata hiyo familia yako bila siasa safi na uongozi bora mambo yatakwenda mrama.
Haya basi kwani Dt.Bushiri akiwa Rais 2025 kuna tatizo kwako?
 
Hakuna ushahidi wa maandishi, video au sauti kuwa Nyerere aliwahi kukataa baadhi ya makabila. Huu ni mkakati wa wenye chuki na jamii hizo kuwakatisha tamaa.
Ni kweli.

Zaidi, Nyerere alipinga ukabila.

Kuna hotuba nyingi alikemea ukabila.

Kuna moja alisema kabisa kwamba mtu hatakiwi kukataliwa urais hata kama ana sifa kwa sababu tu ni Mkara.

Nikataka kujua hao Wakara ni watu gani? Nikaambiwa ni kabila la kanda ya ziwa linalodharaulika sana.

Kwa hiyo Nyerere alikemea ukabila na alijenga umoja wa kitaifa hata kabla ya uhuru. Kwa kweli umoja wa kitaifa ulikuwa ni moja ya masharti ya Tanganyika kupewa uhuru. Nyerere kaacha hotuba na maandishi mengi yanayokemea ukabila.

Nyerere ana makosa yake, lakini hili la kupanda mbegu za ukabila sioni kama ni kosa alilofanya Nyerere. Ukweli ni kwamba Nyerere amefanya kazi kubwa sana kujenga umoja wa kitaifa. Kwenye hili nitamtetea sana tu. Wasiojua historia wasiipindishe kwa kukosa umakini kwao.

Watu wanaofuatilia wanajua hili.

Ona Wakenya wamelitaja.
 
Habari zenu wadau wa JF siasa.
Niende madani hapo juu.
Jana nilikaa na kufanya maongezi hapa na pale na kada mzoefu ndani ya CCM. Moja ya jambo la kushangaza aliloniambia ni kuwa Magufuli akimaliza muda wake 2025, hawa tunawadhania kuwa wagombea urais hawatagombea.
Nikamuuliza kulikoni? Akasema watajitokeza hao na wengine wengi na watavunja rekodi hata kufika 100 ila mgombea urais CCM 2025 ni Katibu Mkuu wa sasa Dr Bashiru Ally Kakurwa.
Nikamwambia ana uhakika gani? Aksema watu wengi ndani ya chama hasa aliowaleta Rais Magufuli wana mitazamo eti kuwa wagombea wengine ni wanyonyaji na wamejaa tamaa ya Mali na hivyo katibu mkuu ni chaguo kwao kwani inaaminika ni MJAMAA zaidi ya Nyerere.
Kutokana na kuonekana mjamaa anaaminika kuikomboa nchi.
Nikamuuliza mbona siasa za ujamaa za Mwalimu zimetuacha makapuku Bashiru naye si atatupeleka huko? Akadai siasa za Nyerere ni nzuri ila vita vya Addi Amin au vita vya Kagera 1978 hadi 1979 ndizo zilivuruga na kuharibu maendeleo ya uchumi uliojengwa kijamaa.
Baada ya hapo nikamuuliza kivipi? Akasema vile vita licha ya kugharimu roho za watu pia ziliigharimu Tanzania US dollars million 500 kipindi hicho.
Nilichoka nikaondoka zangu na siamini kama hili litatokea. Kwanza Siasa za nchi hii hazitabiriki na huenda 2025 Dr Bashiru atakuwa chuoni akifundisha na Katibu Mkuu ni Mwananzengo Fulani.

Kilichotukwamisha mpaka sasa ni ufisadi na sera mbovu za ubinafsishaji na za uchumi chini ya chama kilichotawala mpaka sasa
 
Back
Top Bottom