Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,261
Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CCM, Katibu mkuu kiongozi na sasa mbunge wa kuteuliwa Bashiru Ally aliwahi kunukuliwa akisema watatumia dola sana kubaki madarakani na akaendelea mbele kusema ni uzembe kuondolewa madarakani ukiwa na dola.
Japo kauli hii iliibua mjadala mkali lakini ikitazamwa kwa upana wake ina uhalisia mkubwa sana kwa mifano kadhaa, hembu tazama
Katibu mwenezi wa chama tawala anaweza kupokelewa na kwenda kwenye mkutano wa siasa wa chama chake na watendaji na watumishi wa serikali wa eneo husika, idara mashirika na vitengo mbalimbali na wakawa wanafanya kile kinchoitwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Hakuna chama cha upinzani chenye fursa hiyo.
Katibu mwenezi wa chama tawala anaweza kuwapigia simu mawaziri na wakuu wa mashirika akiwa katika mkutano ya hadhara ya chama wanachama wa chama wakapata fursa ya kuona wanatatuliwa kero zao na kupewa ahadi za kutosha. Hakuna chama cha upinzani chenye fursa hiyo.
Inawezekana pia chama tawala kikawa hakilizamiki kuomba kibali cha kufanya mikutano au maandamano yake mbalimbali kutoka polisi kama inavyovipasasa vyama vyote vya upinzani kufanya hivyo.
Haya ni baadhi ya mambo tu ambayo huenda ndio Bashiru Ally Kakurwa alikuwa akimaanisha ni faida ya kuwa na dola.