Hayawi hayawi sasa yamekuwa, mpango wa kuwawezesha vijana kwa kuwapa ujuzi na mahitaji ya kuwawezesha kuanza shughuli za kilimo unakwenda kubadili hostoria ya Afrika.
Kupitia mpango huu wa BBT, kila kijana anapata fursa ya kuijenga kesho yake iliyo bora. Wakati suala la ajira likiwa changamoto katika nchi zote za Afrika, Rais Samia ameweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuja na muarobaini wa suala la ajira kwa kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo.
Mpaka sasa zimetengwa takribani Hekari 162,492. Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi thabiti wa Rais Samia imejikita katika kuwawezesha wananchi zaidi.
Katika hatua ya kwanza mashamba yametengwa katika Mikoa ifuatayo; Mbeya (Hekari 52,165), Dodoma
(Hekari 20600), Kagera (Hekari 3227) na Kigoma (Hekari 86500). Mpango wa BBT ni endelevu na utafika kila kona.
Sanjari na uwezeshaji huu, serikali inaendelea kutoa pembejeo kwa wakulima wote, msamaha wa kodi kwa malighafi za kilimo, kuiwezesha Bodi ya Nafaka kwa fedha za kutosh, kutafuta masoko ya kimataifa, kuwawezesha Maafisa Ugani nchi nzima, kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa mazao na kudhamini tafiti muhimu kwa sekta ya kilimo.
Tanzania ina ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo takribani Hekta Milioni 13 na nusu, hivyo uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan utakuwa wa kihistoria na wenye kumgusa kila mtanzania moja kwa moja au vinginevyo, hususani vijana.