FAO yavutiwa na BBT, yamsifu Rais Samia kuboresha Kilimo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza sekta ya kilimo na kuboresha mahusiano na mashirikaya kimataifa. Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Dk Qu Dongyu amesema shirika hilo limevutiwa na mradi unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT).

Dk Dongyu alisema hayo alipokutana na kuzungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Makao Makuu ya FAO, Rome nchini Italia.

"FAO tunaunga mkono mradi huu ili Serikali ya Tanzania iweze kutimiza malengo ya kuwainua vijana na wanawake kwenye sekta ya kilimo kama ilivyo moja ya ajenda kwenye mkutano wa FAO wa mwaka 2023," alisema Dk Qu.

Majaliwa yuko nchini Italia akimwakilisha Rais Samia katika Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani (WEF) unaotarajiwa kumalizika leo.

Dk Qu ameahidi kutembelea Tanzania mwakani kujionea maendeleo katika sekta ya kilimo na kupanua wigo wa majadiliano kati ya Tanzania na FAO ili kuendelea kuwezesha zaidi sekta ya kilimo na uchumi wa buluu.

Majaliwa alisema Serikali ya Tanzania imeanza kupanua wigo wa kilimo kutoka cha kutegemea mvua
na kukiwezesha kiwe cha umwagiliaji na imetenga Sh bilioni 900 kufanikisha hilo.

"Kilimo ndio maisha, kilimo ndio chakula, tunataka kujikita zaidi katika kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia mabwawa yetu. Tunataka tujiridhishe kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa kwa kukosa chakula," alisema Majaliwa.
 
Back
Top Bottom