Je ni kweli GPA Kubwa iliniponza!! Nimechemsha au!!

Mkuu,

Kama kweli ww ni msomi mwenye GPA kubwa na umeendelea kama ulivyoadithia basi
usitupotoshe wenzio na wengine wenye nia nzuri ya kufanya/kusoma kwa jitihada kupata marks nzuri,
kwako ww si tu uhaziri bali ndio uliandikiwa kua na maisha hayo. je hujaona mtu akawa na mali kibao then akarudi kua hana kitu?!!

acha kudidimiza watu. ndg zangu tusome tena kwa jitihada kubwa, hiyo ndio funguo ya maisha

Ufunguo wa maisha kwenda wapi!!!.
 
Kaka shukru Mungu kwamba unayo hiyo elimu ya kutosha na unao huo mshahara uanouita mdogo.Kupata GPA kubwa hakukufanyi uwe tajiri wala maskini.Mimi kwa mtazamo wangu ukiwa na kazi ya uhadhiri na bado ukawa maskini ni kama unajitakia vile...uhadhiri ni moja ya ajira chache Tz zenye mshahara wa kueleweka zaidi ya hapo wahadhiri mnakuwa na muda mwingi sana free kuweza kuendesha miradi yako binafsi../.Natamani ningekuwa na hizo GPA nipate kazi ya uhadhiri.Buni miradi itakulipa,kuenedelea kujilinganisha na wenzako kutakuletea pressure bure...
 
Goodrich hujamwelewa!! katika maelezo yake hajasema kama PhD alikuwa na malengo nayo. Alijikuta amefika huko baada ya undergraduate kupata GPA kubwa. maana yake hakuwa na malengo ya hivyo....Yeye alitaka kufanikiwa kwa kupata kazi nzuri ama biashara inayomwingizia kipato kikubwa. soma vizuri maelezo yake utagundua hata kufundisha si kazi aliyoichagua.
 
Unaposema wenzako wako mbali kimaisha unamaanisha nini?

Je, ulipokubali kuingia kwenye uhadhiri ulikuwa na mipango gani kimaisha?

Je, unafahamu kuwa academicians hupata mapato zaidi kwa kupitia grants za tafiti na miradi mbalimbali, je umewahi kuapply grants ngapi? Je, umebuni projects ngapi?

Baada ya kujibu haya maswali jiulize kama cha kulaumu ni GPA, uhadhiri au your own lack of creativity?!!!

Ni sawa lakini si TZ yetu ukilinganisha na nchi zingine nyingi!!. kwenye hilo labda nitoke nje ya nchi, na ndio wengi walivyofanya baada ya kukata tamaa na Maisha na Mambo ya TZ, wengine wanakimbilia siasa.
 
Usidanganyike ndugu. Kama kuna uliyemwacha kakuzidi basi kaiba au kala rushwa. Kwa kiwango ulichonacho ni uvumilivu na kufanya private research na consultance nyingi ili kuongeza kipato. Kwa phd huku haja ya kufuga kuku au kununua daladala.
 
Huyu ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wala hana PHD kama anayo basi ya kwenye mtandao. Maisha na kufahuru wapi na wapi, wangapi hawajasoma kabisa na ni matajiri

Na mvivu maana maprof. siku hizi wanatengeneza pesa nzuri sana kwa kufundisha vyuo mbali mbali

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Pesa nzuri kiasi gani!!. Funguka zaidi kabla hujahitimisha hivyo!.
 
Kama ni msomi uliyekubuhu na kufikia kiwango cha PhD ambacho si wengi walio-bahatika kufikia. Inabidi uwe na ufahamu wa kuwa, fedha na mali sio kila kitu.

Achievement bora zaidi ni kuwa na furaha ya moyoni kuridhika na ukifanyacho. Kama unaona huridhiki na kufundisha fanya utachoona kinakuridhisha satisfaction), lakini, usifikiri kuwa achievement ya usomi ni kipato, ungekuwa unataka kipato ungeachana na kusoma ukajiingiza kwenye biashara, unakumbuka kisa cha Bill Gates?

Fanya unachoona kitakupa wewe "tranquility" au inner self happiness.
 
Ni sawa lakini si TZ yetu ukilinganisha na nchi zingine nyingi!!. kwenye hilo labda nitoke nje ya nchi, na ndio wengi walivyofanya baada ya kukata tamaa na Maisha na Mambo ya TZ, wengine wanakimbilia siasa.

BIG Banned, quite opposite! Ukiwa katika nchi masikini ni rahisi zaidi kupata grants za miradi na tafiti. Wewe umebobea kwenye field gani? Nijulishe ili nikutafutie links za opportunities za kutengeneza mamilioni. Kuna watu kibao all over the world wanatafuta reliable professional partners katika nchi zilizoendelea. Kama uko affiliated na higher learning institution it makes everything easier.
 
GPA = Grade Point Average ukiwa na daraja la kwanza hongera. Wengine tuliondoka na Likikwete na tunapeta maishani.

Tuyaacha mapuuza. Tumia elimu yako na mashahara wako kidogo upatao kuanzisha mradi uliokatikafani yako naamini utafanikiwa.

Yaani umaniacha nacheka mbavu sina wewe baba Mwanaasha!!! Acha uchokozi wewe. Mwenzio nina GPA kali na maisha makali tu na sasa ninasoma ninataka first class ya 4.9!!! Yaani A zote na B plus moja tu nimepata somo moja but hili nilikosa maksi 2.5 nipate A (nimeamua kusoma masters moja of my choice to enhance my areas of expertise). Katika vyote elimu yangu imenisaidia niko mitaani jambo nilipomaliza IDS walinitaka nibaki pale (japo nilisoma idara nyingine si IDS) as researcher na mwalimu. Nikautizame mshahara weee wa 324, 000 basic enzi hizo nikakatimka kufanya private kwa mshahara wa zaidi ya dola 1500 enzi zile na nimeamua kubaki huku huku mitaani tu. Ninachokiona chuo sasa through maongezi na lecturers mbalimbali tatizo ni utitiri wa wanafunzi, mwalimu hana muda wa kutosha wa consultancies and research kama ilivvyokuwa enzi zetu nakumbuka darasa langu tulikuwa wanafunzi 30 tu!! Kweli hata mimi nigekuweko huko ningeshaondoka. Hailipi!!! Omba UN organisations mkuu kule salary dola 7 na kuendelea!!! Mimi naangalia life now!!! At the same time hiyo pension ya wahadhiri ndani ya PPF ni balaa bora wangehamishiwa PSPF!! So sad!
 
.....elimu siyo sawa na utajiri. Na tafiti nyingi zinaonesha, kwa mfano, mwenye elimu ya biashara (MBA) hawezi leta mafanikio ktk kampuni tofauti na wasio kuwa na elimu ya biashara, ni experience ndiyo yenye umuhimu. Kwa hiyo huo muda unaopoteza ukiwa shule wenzako wanapata experience ya kutengeneza pesa, kwa hiyo ukirudi inabidi uanze kujifunza jinsi ya kutengeneza pesa. Ukikubali kujifunza unaweza kuja wapita, ila ukibaki unajiona elimu yako ni bora basi wenzako utawasikia tu!! na hili ndilo huwaponza wasomi wengi, kwa kuiona wao eti wasomi.
 
Nakushukuru sana, umeongeza kitu muhimu sana. Ni ngumu sana mtu kuelewa namaanisha nini. Nadhani soln ni hiyo. kutafuta kazi nyingine inayolipa. Wengine siasa hatuwezi.
 
Nilimaliza chuo miaka kadhaa iliyopita na sasa ni mhadhiri chuo kimoja hapa TZ. Ukweli ni kwamba GPA nzuri (ambayo sasa mi naiita mbaya!) ndio iliyonifanya nishawishiwe na kushawishika kubaki hapo nilipo!, Nikapata nafasi ya kwenda kusoma masters then PhD kwa takriban miaka kama 6 hivi. Tulipomaliza Undergrad kama kawaida watu/classmates tulitawanyika kila mtu kutafuta maisha kwa namna yake. Sasa kwahiyo miaka sita niliyopoteza kwa kusoma, wenzangu walibaki nchini wengine walipata kazi serikalini, wengine kampuni binafsi ambapo huko ni watu wenye vyeo na experience nzuri sana. Ukiachana na hayo ukweli ni kwamba wenzangu wapo mbali sana kimaisha kiasi kwamba nahisi mimi kama vile nilipotea au ile GPA niliyopata ndio iliniponza ingawa kwa wakati ule nilijihisi mi ndio mwenye bahati, lakini naona ni tofauti kabisa hasa nikijilinganisha na wenzangu na hiyo miiaka sita nimefanya maendeleo gani, wenzangu wana mengi sana ambayo mi ndio nafikiria kuanza.

Mbaya zaidi uhadhiri haulipi kabisa, yani ni kutegemea mshahara tu!. Na nikiangalia masenior wangu (Professors etc) hawana maendeleo yoyote, wanalia na njaa tu, wapo wanahangaika na vibiasharabiashara vidogo ambavyo kweli vinachangia kwa wahadhiri wengi kutojiandaa vizuri wanapoingia madarasani kufundisha. Maisha na heshima ya mwalimu wa chuo ni vitu viwili tofauti kabisa (sivyo vile watu wanavyofikiria)!.

Kweli uwalimu ni wito!, lakini kama hauridhiki na unachokipata na hauwezi kujikwamua na maisha magumu na majukumu ambayo unayo kila siku, kweli uwezekano wa kufunza tu ilimradi siku ziende utakuwepo tu miaka yote, sababu utakuwa unatumia muda mwingi kufanya madili mengine nje na kazi ya kufundisha.

Je ni Kweli GPA kubwa iliniponza!! Niache hii kazi nitafute nyingine!!.

mkuu fundisha hata tuition itakulipa.kuna jamaa mmoja anaitwa kamanija a.k.a wagi,a.ka.a son of africa.huyu ni mjasiriamali vibaya,pamoja na kuwa lecturer pale Turdaco akifundisha law,lakini jamaa anapiga tution kuanzia a level mpaka chuo watu wa open university jion pale buguruni malapa na anapiga hela ndeeeeefu kuliko hata huo mshahara anaolipwa huku anatozwa makodi kibaaaaao.ni kujipanga tu kaka.baba yangu mdogo ni prof kuna ndugu yangu mwingine ye ni lecturer wote wapo haposua,but ukilinganisha maisha yao ni tofaut mwenye masters kapiga maendelea mbayaaaaa,yaani kupitia maendeleo ya bwana mdogo dingi mdogo leo hii ndo anstshuka.kwa hiyo mkuu haya mabo ya GpA kubwa au ndogo sio ishu ishu ni wewe mwenyewe umejipangaje,unatumiaje fursa ulizonazo na zinazokuzunguka. Hujaona watoto wa kichaga na kikinga darasa la saba wanapiga biashara china,dubai,korea india na bongo na wanamkwanja mrefu tu? Hyo nayo ni gpa?
 
Yaani umaniacha nacheka mbavu sina wewe baba Mwanaasha!!! Acha uchokozi wewe. Mwenzio nina GPA kali na maisha makali tu na sasa ninasoma ninataka first class ya 4.9!!! Yaani A zote na B plus moja tu nimepata somo moja but hili nilikosa maksi 2.5 nipate A (nimeamua kusoma masters moja of my choice to enhance my areas of expertise). Katika vyote elimu yangu imenisaidia niko mitaani jambo nilipomaliza IDS walinitaka nibaki pale (japo nilisoma idara nyingine si IDS) as researcher na mwalimu. Nikautizame mshahara weee wa 324, 000 basic enzi hizo nikakatimka kufanya private kwa mshahara wa zaidi ya dola 1500 enzi zile na nimeamua kubaki huku huku mitaani tu. Ninachokiona chuo sasa through maongezi na lecturers mbalimbali tatizo ni utitiri wa wanafunzi, mwalimu hana muda wa kutosha wa consultancies and research kama ilivvyokuwa enzi zetu nakumbuka darasa langu tulikuwa wanafunzi 30 tu!! Kweli hata mimi nigekuweko huko ningeshaondoka. Hailipi!!! Omba UN organisations mkuu kule salary dola 7 na kuendelea!!! Mimi naangalia life now!!! At the same time hiyo pension ya wahadhiri ndani ya PPF ni balaa bora wangehamishiwa PSPF!! So sad!

we mhaya au myakyusa? Mbona unajimwambafai kiasi hiki mazeee!
 
.....elimu siyo sawa na utajiri. Na tafiti nyingi zinaonesha, kwa mfano, mwenye elimu ya biashara (MBA) hawezi leta mafanikio ktk kampuni tofauti na wasio kuwa na elimu ya biashara, ni experience ndiyo yenye umuhimu. Kwa hiyo huo muda unaopoteza ukiwa shule wenzako wanapata experience ya kutengeneza pesa, kwa hiyo ukirudi inabidi uanze kujifunza jinsi ya kutengeneza pesa. Ukikubali kujifunza unaweza kuja wapita, ila ukibaki unajiona elimu yako ni bora basi wenzako utawasikia tu!! na hili ndilo huwaponza wasomi wengi, kwa kuiona wao eti wasomi.

na wasomi wengi sio marisk taker/not enterprenuer kwa sababu wao huonza na analysis ya setback kwanza.
 
ama kweli nature ya mtu haibadiliki ht kama amesoma vp..yaani we ukipewa kitengo utaiba mbaya kwa tamaa uliyokua nayo.
 
Uliondika hapa ni ukweli mtu, uhadhiri katika vyuo vyetu ni sifa tu za kujinga, kwa ujumla watu wamechoka sana, sema ile status quo wanajaribu kuimaitain kwa kulazimisha.
Waadhiri wengi wana msongo wa mawazo na work load kubwa, na bado lawama.
 
Back
Top Bottom