Je, ni Akili za Kitaaluma pekee ndizo zinazokufanya uwe mwana Usalama wa Taifa mahiri, au ni zile Akili za Kuzaliwa nazo ( Nature ) tu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,709
109,144
Nimedokezwa kuwa huko CIA na MOSSAD wao Kipaumbele chao kwa wanao wa recruit ni Akili za Kuzaliwa nazo pekee na hizo za Kitaaluma (za Darasani) nenda Katambe nazo kwa Washamba Wenzako huko Kijijini Kwenu.

Na nimedokezwa pia nchi zingine nyingi (hasa Barani Afrika) ila Tanzania haipo Wao ili uwe ni mwana Usalama wa Taifa wanaangalia Taaluma yako kama umeshawahi kupata Sup Chuoni au kama ulipokuwa Darasani ulikuwa unakaa mbele na muulizaji Maswali mzuri na Daftari zako ni Safi na Notes zako zinavutia na uwe na Uwezo mkubwa wa Kukariri Notes za Mwalimu wako (hata kama huzielewi) na Kuzijibia Mitihani ili upate Alama A na B.

Je, ukweli hasa ni upi? Najua hapa JamiiForums mpo /wapo Wabobezi wa Fani husika (tajwa) hivyo watanisaidia Kunifafanulia / Kutufafanulia akina siye tusiojua lolote lile kuhusu mambo / masuala ya Usalama wa Taifa ( Intelligence ) hapa duniani.
 
Akili ni muhimu ndo maana maafisa usalama wa miaka 1995 kurudi nyuma tulichujwa sana

Kwa Sasa kazi Hiyo nshaacha Ila wanaangalia vitu vingi sana

Kuna Afisa usalama unaweza tumwa Kitengo fulan kulingana na wewe ulivyo au ukawa recruited juu kwa juu kwenye nafasi uliyopo labda Banker au mwalimu au dereva ili uchunguze jambo fulan kwa muda fulan Ila hao uwa hawadumu

Ila wengi walitolewa mashuleni vichwa kabisa

Na wengine utulivu silence Yao ya ku contain jambo bila ku leak hapa kuna upimaji wao unavyofanyika
 
Field ya social sciences inaongoza kwa kutoa best spy products duniani ukilinganisha na field ya pure science. Jasusi aliyesoma course za social science mfano public relation ukijaribu kufanya comparison na aliyesoma science ile pure mfano injinia n.k , kwenye scoreboard atakaye kimbiza ni huyu wa social science.
 
Nimedokezwa kuwa huko CIA na MOSSAD wao Kipaumbele chao kwa wanao wa recruit ni Akili za Kuzaliwa nazo pekee na hizo za Kitaaluma (za Darasani) nenda Katambe nazo kwa Washamba Wenzako huko Kijijini Kwenu.

Na nimedokezwa pia nchi zingine nyingi (hasa Barani Afrika) ila Tanzania haipo Wao ili uwe ni mwana Usalama wa Taifa wanaangalia Taaluma yako kama umeshawahi kupata Sup Chuoni au kama ulipokuwa Darasani ulikuwa unakaa mbele na muulizaji Maswali mzuri na Daftari zako ni Safi na Notes zako zinavutia na uwe na Uwezo mkubwa wa Kukariri Notes za Mwalimu wako (hata kama huzielewi) na Kuzijibia Mitihani ili upate Alama A na B.

Je, ukweli hasa ni upi? Najua hapa JamiiForums mpo /wapo Wabobezi wa Fani husika (tajwa) hivyo watanisaidia Kunifafanulia / Kutufafanulia akina siye tusiojua lolote lile kuhusu mambo / masuala ya Usalama wa Taifa ( Intelligence ) hapa duniani.
Mbona kama wewe ni mmoja wao?🙂🙂
 
Back
Top Bottom