ni mjadala mkongwe zaidi duniani, mjadala wa vizazi na vizazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu kwa muktadha wa kiimani
Ni mjadala tata kuhusiana na kile kilichotokea pale Eden na ukweli kuhusu dhambi ya asili....kimsingi ni mjadala usioisha nguvu wala kuchuja! Ulikuwepo upo na utakuwepo! Mjadala wa ngono uzinzi uasherati na majina yake mengi...!
...shetani naye ana dini yake na mojawapo ya ibada zake muhimu ni hili tendo la kufanya ngono hadharani, hili linahusishwa na kile kitendo cha pale Eden, kwamba ile dhambi ya asili ni ngono! Kwenye satanism ngono ina nafasi kubwa sana..naweza kukiri ni zaidi ya asilimia 90! Ibada ya kishetani bila tendo la ngono haijakamilika
mfanano wa kushangaza no kwamba kwenye imani nyingi kama si zote zinazoamini katika Mungu mmoja kitendo cha kuzaa nje ya ndoa ndio dhambi kubwa inayokutenga na imani yako na ili uweze kurudishwa kundini tena kuna ibada maalum na rasmi kwa ajili ya tendo hilo (ibada ya kurudi kundini )
Tafsiri ya dhambi
Ni jambo lolote lile lenye madhara ama kwa mtenda au kwa mtendewa lakini kiimani ni jambo lolote lile linalokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu
...kwenye kanuni za kikristo kumeainishwa dhambi nyingi tu lakini hizi zote hazipewi uzito mkubwa kama ngono! Kwenye imani za wenzetu wengine kitendo cha mwanamke kukutwa amezini bila ndoa adhabu yake ni kupigwa mawe hadi kufa! Mwanaume akiachwa anapeta mitaani na hahesabiwi hatia hata kama alimlazimisha mwanamke husika kufanya naye ngono
hii hali imekuwa ni kama desturi na mapokeo vizazi na vizazi, hata leo hii ni rahisi sana mwanaume kukubalika kwenye mahusiano hata kama ana mtoto tayari kwa mwanamke mwingine kuliko mwanamke ambaye ana mtoto kwa mwanaume mwingine
Baadhi ya imani zinaruhusu ndoa za mitala , lakini kamwe huwezi kukuta mwanamke anachangia wanaume zaidi ya mmoja kihalali
Vyovyote vile iwavyo bado ngono inaonekana ndio dhambi halisi na mwathirika mkubwa akiwa ni mwanamke