Je ngono ndio inayotambulika rasmi kiimani?

Je ngono ndio inayotambulika rasmi kiimani?

Mwanamke anakuwa ni muhanga wa kuadhibiwa pindi anapo bainika kushiriki kitendo cha ngono nje ya ndoa na amekuwa akipewa adhabu kubwa sana kulingana na mwanaume...Huwa naamini enzi hizo wakati wa utungwaji wa adhabu ya makosa mbalimbali palikuwa hakuna ushirikishwaji wa wanawake...Na kiasili viumbe vya kiume vyote hapa duniani tuna wivu uliopitiliza pindi tunaposikia mpenzi wetu ama mke wetu anamahusiano na mwanaume mwingine...Ni ukweli ulio wazi kuwa inatuumizaga mno na si kwetu binadamu tu...Angalia vita kati mbwa dume pindi wanapogombania Mbwa jike...Na hata leo kuna majina mengi mabaya kwa wanawake ambao wako kwenye uhusiano na zaidi ya mwanaume mmoja ili hali majina hayo hayatumiwi kwa wanaume wenye mahusiano na zaidi ya mwanamke mmoja....Mfano...Malaya, Kahaba nk..
 
Na ndiyo dhambi ambayo Mwenyezi Mungu, kupitia vinywa vya Manabii, Mitume, Walimu, mbali mbali, anaitaja ya kuwa anaichukia kweli, na msamaha wake, ni kuna mawili, akusamehe kwa haraka ama achukue muda sana kukusamehe, ( wakati mwengine, anakuacha uteseke na madhara ya hayo tajwa kwenye Maada, ama anakusamehe ila madhara ni juu yako na utakufa nayo).

Nilishajiuliza nami maswali mengi tu kuhusu hili/lo. Ila yote ya yote, bado Mungu, anasamehe kwa wepesi zaidi ukirudi kwake kwa kumaanisha haswa, hapa ina maana unaacha kabisa ngono, zinaa, uzinzi, ulawiti, ufiraji, ufirwaji, na yote yanayoshabihiana na Maada husika hadi ufunge ndoa, ama utulie na mwanandoa mwenzio, kikamilifu mbele za Mungu. Hadi Kifo kiwatenganishe.

Siyo jambo dogo, linahitaji jitihada za hali ya juu, ila wapo wanaoweza kuvumilia.

Ezekieli 24:13-14

Mathayo 5:27-28

Warumi 1:24-27

1Wakorintho 5:1-2

Hiyo ni mifano michache tu kwenye Kitabu Kitakatifu (Biblia), ipo mingi sana mistari na maonyo ya Maada husika.

Ahsante!
 
hivi nani alisema huko Bustan ya Eden Adam na Hawa walifanya kosa la ngono?
 
Kwa hakika sina kwakuwa haikutamkwa neno 'kufanya ngono'
fikra tu bro, lakini ukweli ni kwamba, hawakuwa wamefanya kosa...
kwa maana, Mungu alipomuumba Adam, hakusema Atamuumbia dada au mama au shangazi yake, alimuumba Hawa ili iweje sasa?

verse iko wazi, TUNDA LA MTI WA KATI KATI!!!!!!!.na ngono hapo haina upenyo hapo
 
Kwa hakika sina kwakuwa haikutamkwa neno 'kufanya ngono'
Mwanzo3:6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.”

ukiangalia hiyo aya pale juu, inaonyesha Hawa alianza kwanza kula, kisha baadayen akampelekea na Adam.
SASA KAMA ILIKUWA NI NGONO, ALIANZAJE HAWA KUFANYA NGONO PEKE YAKE KWANZA, KISHA AMPELEKEE NA ADAM HIYO NGONO???😱😱😱
 
Ndio maana nikasema ni mjadala usiokoma vizazi na vizazi
 
hahahah pamekucha sasa bado hajaja kilanga na wengine
 
Kwenye imani za wenzenu wengine kitendo cha mwanamke na mwanamme kukutwa wamezini bila ndoa, adhabu yao ni kupigwa mawe wote wawili mpaka kufa tena baada ya kukamilika kwa ushahidi wa uhakika. Na hukumu hio ikiwa watendaji wamo ndani ya ndoa.
Walokuwa out of ndoa ni kutandikwa bakora mia kila mmoja.
Kama kuna mahali wanatekeleza hukumu hizo kwa kumuhukumu mwanamke pekee basi wanakosea.
Nimemaliza...
 
Thanks my wife sina la kuongeza hapa...zaidi umeniongezea maarifa
 
Kwenye imani za wenzenu wengine kitendo cha mwanamke na mwanamme kukutwa wamezini bila ndoa, adhabu yao ni kupigwa mawe wote wawili mpaka kufa tena baada ya kukamilika kwa ushahidi wa uhakika. Na hukumu hio ikiwa watendaji wamo ndani ya ndoa.
Walokuwa out of ndoa ni kutandikwa bakora mia kila mmoja.
Kama kuna mahali wanatekeleza hukumu hizo kwa kumuhukumu mwanamke pekee basi wanakosea.
Nimemaliza...
Dah, hongera sana Dada!.. ndio raha ya kusoma na kuchunguza ukweli wa mambo hii...
watu tukiwa kama wewe, leo hii tuisingekuwa brainwashed
 
Back
Top Bottom