Uchaguzi 2020 Je, ndani ya CCM kuna watu wamegeuka mashetani katika maumbo ya kibinadamu?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Awali ya yote, mtakaokwazika mtanisamehe tu. Kwa sababu kichwa kikuu cha mada hii imebebwa na maneno magumu na makali kidogo.

Imebidi iwe hivi kwa sababu nimetafuta maneno mbadala ili ujumbe ama maudhui ya ujumbe ninaotaka kila mtu apate, nikakosa.

Pokeeni na twendeni hivyo hivyo kwa sababu ni kweli wapo watu ambao kwa nje sura ni binadamu, lakini ndani ya "nia zao" ni mbwa mwitu wakali, ni mashetani 100%; waongo, wauaji na majambazi.

Hawa ndiyo nimewaita, "THE DEVIL IN HUMAN SHAPE" yaani "SHETANI KATIKA UMBO LA KIBINADAMU"

Hawa siku zote hulazimishwa uongo uwe ukweli kwa yeyote kwa hiari ama kwa lazima so long as wanazo nguvu na mamlaka ya kulazimisha kufanyika hayo.

Ndivyo ilivyo CCM hii ya sasa, they are devils in human shapes.

Kiongozi mkuu wa taasisi yoyote ndiye hubeba taswira (image) nzima ya taasisi hiyo...

Katika level ya familia kama taasisi, baba akiwa ni mlevi, mvuta sigara na mpiga mke, basically uwezekano wa watoto kuwa kama yeye ni 99.99%.

Kwa wakristo na wasomaji wa kitabu kitakatifu cha Neno la Mungu (Biblia) mtanielewa vizuri kwenye hili;

Kwamba, Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani kwa miaka 33.5 tangu kuzaliwa kwake, kukua na huduma yake ya kuhubiri injili ya wokovu duniani alikuwa ni " MUNGU MWENYEWE KATIKA UMBO LA BINADAMU yaani" GOD IN HUMAN SHAPE"

Alitumia njia ya amani na uoendo ili kujifunua kwao (binadamu) ili wamtambue, wapokee ujumbe wake, na kisha waufanyie kazi kivitendo ili ubadilishe mfumo na mtindo wa maisha yao ya mazoea ya dhambi. Lakini wachache sana waliweza kuiona neema hii wakabadilishwa....

Wengi wa Wayahudi walimkataa kabisa hata kumsikia tu achilia mbali kumpokea....

Mara nyingi Yesu Kristo aliwaambia kuwa; hata kama hamwamini kuwa mimi ni mwana wa Mungu na kwamba Mungu yu ndani yangu na bila yeye Mimi siwezi fanya jambo lolote, basi ingalau ziaminini kazi nizitendazo...

Pamoja na "appeal" hili, binadamu baadhi hawakujali, hawakupokea lolote...

Kazi za Yesu Kristo zimeandikwa sana. Ni miujiza isiyoelezeka kwa lugha rahisi. Kufufua watu, kulisha chakula (mikate) mitano tu watu 5,000; kuponya magonjwa sugu mbalimbali, kuwafungua watu wengi toka kwenye vifungo vya ibilisi shetani, kugeuza maji kuwa divai nk nk...

Mamia kwa maelfu ya watu kwa miujiza hii waliamini na kumfuata Yesu Kristo...

Wenye mioyo migumu, wao kwao haya hayakuwa lolote, hayakuwa chochote kubadilisha mitazamo yao na kugeuka toka dhambini....

Pamoja na kuwa Yesu Kristo alikuwa na nguvu za UTAWALA WA KIFALME, nguvu na MAMLAKA YA KI- MUNGU, kamwe hakutumia nguvu na mamlaka yake (ambayo kwa kweli ni makubwa na yasiyo na mwisho) kuwalazimisha watu kumwamini, kumpenda ama "kuunga juhudi" zake...

Hii ni tofauti kabisa na CCM na Mwenyekiti wao chini ya serikali hii....

Tunaambiwa kilaghai na kipropaganda kuwa huyu mtu "alishushwa toka mbinguni kuja kuikomboa Tanzania"...

Tunaambiwa huyu mtu ni " mtakatifu ", hana waa, hana dhambi....tumfuate, tumuunge juhudi....

Tunaambiwa ametenda maajabu na makuu ndani ya miaka minne na usheee sasa, hivyo TUMFUATE na KUUNGA MKONO JUHUDI ZAKE....

Tunaambiwa ndani ya miaka minne na ushee amefanya haya;

å Amejenga reli ya SGR

å Amejenga bwawa la umeme la Stiglers Gorge

å Amenunua ndege za Bombardier na Dreamliner

å Amejenga zahanati na hospitali za kutosha

å Amejenga barabara za lami Tanzania nzima nk nk

Yote haya ni mema kabisa KAMA KWELI YAMEFANYIKA...

Tatizo linakuja la kila mtu kulazimishwa kumwamini, kumkubali na kumpenda na kumtetea mtu huyu kwa sababu ya haya, kwa gharama yoyote...

Imefika wakati sasa nguvu kubwa ya KIJAMBAZI na NJIA ZOTE ZA KIHALIFU zinatumiwa chini ya NGUVU na MAMLAKA yake ya KIFALME kuwalazimisha watu wote wamsifu, wamuamini, wamkubali na kumuunga mkono kuwa amefanya haya....

Hii ni ngumu kwa sababu huku kwetu Shinyanga so far sioni tofauti yoyote positive ya kimaisha na kimazingira kwa watu tangu mwaka 2015 hadi sasa....!!

Hii ikiwa na maana kuwa, yanayosemwa yamefanyika wengine huku hatuyaoni na hayajaleta impact yoyote ktk maisha yetu ya kila siku...

Ndiposa, violence, ujambazi na nguvu kubwa zinatumika kutulazimisha tuamini, tukubali na tumuunge mkono bwana mkubwa huyu....

Yesu akawaambia;

"....mniamini ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba (Mungu) yu ndani yangu; la hamuamini (hivyo), aminini kwa kazi zenyewe...."
(Yoh.14:11)

Kazi anazoziema Yesu ni miujiza aliyofanya ya kufufua watu, kuponya magonjwa sugu kwa neno tu la kinywa chake, kulisha chakula (mikate mitano na vijisamaki kidogo tu) watu 5,000; kubadili maji kuwa divai na miujiza mingine mingi...

Huyu alikuwa, "....GOD IN HUMAN SHAPE....". Lakini hata alipokataliwa, kazi zake kubezwa, watu kutomwamini wala kufuata mafundisho yake, kamwe hakutumia NGUVU na MAMLAKA yake ya ki - MUNGU kuwalazimisha watu wampende, wamshangilie ama kumfuata na ukiwa huna uelekeo ama neutral basi unatekwa, ama unabambikiwa kesi ya uhujumu uchumi ama unapigwa risasi (kuuwawa)...

Sasa leo tuna watu NI MASHETANI KATIKA SURA YA BINADAMU. Bahati mbaya sana hawa watu ndiyo wameshika MAMLAKA ya kifalme....

Wamejivika sura bandia za " MALAIKA WA NURU" kumbe ndani ni mashetani, Ibilisi baba wa uongo, wauaji na majanbazi...

Hawa wanalazimisha TUWAAMINI, TUWAKUBALI, TUWASIFU, TUWAPIGIE MAKOFI na TUWAUNGE MKONO kwa lazima....

Zaidi, soma;

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa ahamasisha Mbowe, Zitto na wengine wanaoikwamisha Serikali 'washughulikiwe'
 
1. Alipopigwa risasi Lisu makada wa CCM walishinda mitandao kushangilia , kupotosha ukweli na kubeza.

2. Alipo uawa mawazo UVCCM na makada wengine wa CCM walibeza na kukejeli sana.

3. Juzi kati hapa bungeni wabunge wa CCM walikua wanahimizana mbunge fulani hivi wa upinzani auawe

4. Amevamiwa na kujeruhiwa Nwenyekiti wa CHADEMA, kuanzia wabunge wa CCM , UVCCM na makada wengine wametumia platforms tofauti kubeza , kukejeli na kupotosha.

Kweli inawezekana shetani yupo kazini huko CCM
 
Nakubali, hata wale wabunge waliokuwa upinzani baada ya kuhamia ccm tu, shetani akawavaa!
... Lijualikali, limegeuka limekuwa shetanlikali!
 
Mm sina chama chochote lakini ukweli ni kuwa Tanzania yngu kuna siasa za kishamba sana na bado tuna safari ndefu

Leo mara eti utaskia sjui Magu aongezwe mda wa Urais akitaka asitake, ukiuliza je tukienda kwenye katiba inasemaje kuhusu hilo? Hawakupi jibu zaidi ya kejeli.

Leo viongozi wa upinzani wanapigwa yaani amani yao ni ndogo ndani ya nchi yao, yaani sisi kwa sisi tunapigana kuumizana na kuuwana kabisa kwa sababu za kisiasa

Dunia ni mapito, usifanye ubaya ukitegemea miaka yako 40 - 50 kwamba haitoisha, kinachofanyika Tz ni ushamba hasa zama hizi
 
CCM ni nyumba ya shetwain aisee...matendo yao yanaendana kabisa!! Naunga mkono hoja!!
 
ccm ni chama cha kigaidi na hii ni serikali ya kishetani
Afu wanadanganyana eti wabadili katiba....unajua usipokuwa makini shetani huyo huyo anaweza kukudumbukiza shimoni kisha akasepa huku akikucheka!!
 
Afu wanadanganyana eti wabadili katiba....unajua usipokuwa makini shetani huyo huyo anaweza kukudumbukiza shimoni kisha akasepa huku akikucheka!!
Ndiko tulikofika baada ya Mh sana LISSU kutabiri dikteta uchwara Sasa ni dikteta kamili
 
1591936162720.png

Wataalamu wa kupita bila kupingwa
 
Back
Top Bottom