Mleta mada, nimesha kusoma akiri yako, yaani wewe hujarizika na huyo msela kutokukuoa hivyo unataka umbane kwa kigezo cha mtoto.
Nakushauri ujipe ujasiri wa kumchukia ghafla ubadili namba zako za simu, kata kabisa mawasiliano naye na lea tu mwanao.
Labda hutujui vizuri wanaume, tulio wengi mtoto huwa si lolote kwetu, hatunaga chungu kihivyo kwakuwa sisi hatubebi mimba wala hatuzai, muhimu kwetu huwa ni mama zetu na watoto huwafikiria tunapokuwa tunaishinao nyumbani.
Ukimpeleka huko ustawi wa jamii atasema kwakuwa mtoto ni mali ya baba na mama basi kila mmoja amgharamikie nusu ya matunzo yake. Hakutakuwa na kisingizio eti wewe huna kazi maadamu ni mtu mzima yakupaswa uwe na shughuri yoyote ile ya kukuingizia kipato.
Zitapigwa hesabu mtoto anatumia shilingi ngapi kwa mwezi ili aishi tena maisha ya kawaida tu na si wewe alafu gharama hizo zitawahusu baba na mama.
Usije shangaa ukawa unatumiwa elfu 20 kwa mwezi.
Nafikiri akili yako inawaza labda unawezakuwa mnaugawana mshahara wake nusu kwa nusu hilo halipo, mshahara ni mali yake na anaruhusiwa kuupangia mambo yake bila mtu yoyote kumwingilia.
Alafu siku nyingine ukitongozwa na mwanaume aliyefanikiwa kimaisha uwe makini sana kwakuwa watu wa aina hii huamini mafanikio yao ndio husababisha mwanamke kuwakubali haraka haraka na ndiyo huwa hivyo, hivyo huwa ni watu wa kuchagua chagua sana sasa were kitendo tu cha kuvuliana naye vyupi basi ukaamini tayari umeshaolewa. Siku nyingine usibebe mimba ya mtu bila kuolewa kwanza.
Ukizidi kumletea msela za kuleta atamkana mtoto na hiyo kesi mtazungushana sana.
Mwisho nakukumbusha tu , hutafanikiwa kumfanya msela aishi unavyotaka wewe. Kitendo cha msela kukomaa na masomo mpaka kufikia hapo maana yake ameshayashinda maisha ya kuamuliwa na mtu kipi cha kufanya isipokuwa mambo yake ya kikazi tu.
Hebu na wewe ongeza bidii kujitafutia pesa zako ili ujiongezee uhuru wa kujiamulia mambo yako.