Mzazi mwenzangu anadai atabadili cheti cha mtoto cha kuzaliwa atoe jina langu kwa kuwa ananichukia

Pleasepast

JF-Expert Member
May 30, 2023
325
454
Habarini za usiku wapendwa

Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza nahitaji msaada wa Mawazo chanya iko hivi kuna mwanamke nilipata naye mtoto lakini kwa bahati mbaya sana tukaja kutengana na sasa kila mtu anaishi kivyake yeye yupo na mtoto.

Kuna wakati mzazi mwenzangu anapata hasira za kuachana anaanza kusema atatengeneza cheti kingine cha kuzaliwa cha mtoto ambacho hataweka jina langu kwa sababu ananichukia sasa.

Wakuu naomba kuuliza hivi hii kitu inawezekana akabadilisha na mtoto akaanza shule na jina jingine huko alipo kwasababu amejificha nae kusiko julikana lakini mwanzo nimeishi na mtoto kama mwaka na miezi 9 na hadi cheti cha mwanzo ndio kilitumika kutengeneza kadi yake ya bima kwa mwajiri wangu.

Sasa hapa naomba kwa wanaojua wanijuze nimfanye nini kabla hajabadilisha au akibadilisha itakuaje hivi kwa kile cheti cha mwanzo.

NB: Hivi visa vipo mitaani kwetu naomba wadau toeni maoni watu wajifunze.
 
""Ishi Nao Kwa Akili""hili fumbo inaweza kuwa Wao wana na akili zaidi yetu,,au sisi tuna akili zaidi yao,,,au wao hawana akili kuzidi Sisi,,au sisi hatuna akili kuzidi wao,,au sisi tuna akili kuzidi wao na wao hawana akili
zaidi Yetu,,au wao Wana akili kuzidi sisi na sisi hatuna hizo akili kuwazidi wao.###TafakariChukuaHatua###HAKI YA MAPENZIII🔔🔔(Kaaang!!Kaaang!!!)
 
Ishi nao kwa akili, kama walikuja wasomali wakapata passport za Tanzania na wakasafiri nazo hadi uingereza, mtoto aliyezaliwa Tanzania atashindwa kubadilishiwa jina na kupewa cheti cha kuzaliwa kingine!?,kama jina lako kwa mtoto ni muhimu sana basi zingatia gharama za ku maintain hilo. Akitokea mwanaume mwingine mzazi mwenzio akamuelewa tena akawa responsible kwa mwanao, Ili kumshikilia kumpa mtoto jina la huyo mwanaume hadi kupata cheti kipya cha kuzaliwa ni kitendo cha siku 5 tu za wiki. Don't underestimate the capability of the abandoned single mother.
 
Ishi nao kwa akili, kama walikuja wasomali wakapata passport za Tanzania na wakasafiri nazo hadi uingereza, mtoto aliyezaliwa Tanzania atashindwa kubadilishiwa jina na kupewa cheti cha kuzaliwa jingine!?,kama jina lako kwa mtoto ni muhimu sana basi zingatia gharama za ku maintain hilo. Akitokea mwanaume mwingine mzazi mwenzio akamuelewa tena akawa responsible kwa mwanao, Ili kumshikilia kumpa mtoto jina la huyo mwanaume hadi kupata cheti kipya cha kuzaliwa ni kitendo cha siku 5 tu za wiki. Don't underestimate the capability of the abandoned single mother.
Hapo sawa angalau wewe umejibu swali husika nashukuru kwa mchango wako japo bado hujafafanua kuhusu cheti cha mwanzo
 
Kama mtoto ni wako unahangaika nini?

Akimbadili jina atakuwa amembadili DNA?

Usihangaike naye, mtoto akikua atakutafuta.
Hujaelewa swali yote hayo nayajua hapa mimi nataka watu wenye uelewa kuhusu jambo kama hili watoe maoni yao na kuhusu kuacha aje akutafute unaweza kuacha tu lakini hapa kinacho angaliwa ni kwa namna gani mtu anaweza kuzuia au ni kwanini hii iwezekane je mamlaka za vyeti haziko makini au shida ni nini
 
Kwanini uhangaike kuzuia wakati hauna huo uwezo?
 
Habarini za usiku wapendwa

Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza nahitaji msaada wa Mawazo chanya iko hivi kuna mwanamke nilipata naye mtoto lakini kwa bahati mbaya sana tukaja kutengana na sasa kila mtu anaishi kivyake yeye yupo na mtoto.

Kuna wakati mzazi mwenzangu anapata hasira za kuachana anaanza kusema atatengeneza cheti kingine cha kuzaliwa cha mtoto ambacho hataweka jina langu kwa sababu ananichukia sasa.

Wakuu naomba kuuliza hivi hii kitu inawezekana akabadilisha na mtoto akaanza shule na jina jingine huko alipo kwasababu amejificha nae kusiko julikana lakini mwanzo nimeishi na mtoto kama mwaka na miezi 9 na hadi cheti cha mwanzo ndio kilitumika kutengeneza kadi yake ya bima kwa mwajiri wangu.

Sasa hapa naomba kwa wanaojua wanijuze nimfanye nini kabla hajabadilisha au akibadilisha itakuaje hivi kwa kile cheti cha mwanzo. NB Hivi visa vipo mitaani kwetu naomba wadau toeni maoni watu wajifunze
Mkuu pole Sana Kwa changamoto hiyo, nianze Kwa kujibu swali la Kwanza, kwamba je anaweza kubadilisha cheti cha kuzaliwa au hapa, jibu NI ndiyo, Kwa sababu anao uwezo wakubadili jina la Baba Kwa kulikana mahakaman au akasingizia hawahi kupata cheti cha kuzaliwa, na anapatiwa cheti kingne Kwa sababu vyeti vya kuzaliwa havina picha na hata akienda kuomba kingne atapata Kwa sababu majina yatakuwa tofauti nacha Kwanza

Pili Kwa maono yangu, huyo mwanamke Kwanza siyo mwanamke sahihi wakufanya naye Maisha, Ni dhahiri hafai anakaa na mtoto wako sehem isiyojulikana.
Tatu, huenda huyo mwanamke anakutikisa kukuona uwezo wako, ila Iman yangu hawez kubadili majina total maana baadaye yatasumbua Hasa mashuleni na kwenye mifumo ya BIMA.

Mwishoni nikutake uwe makini Sana na mwanamke WA Aina hiyo, simamia Msimamo yako kuhusu mtoto na uhusiano wako na yeye kama wazazi

Sent from my Pixel 4 XL using JamiiForums mobile app
 
Hapo sawa angalau wewe umejibu swali husika nashukuru kwa mchango wako japo bado hujafafanua kuhusu cheti cha mwanzo
Ufafanuzi kuhusu cheti cha mwanzo, mifumo yetu bado haipo computerized. Mwanamke anaweza kwenda Rita akadai amepoteza cheti cha kuzaliwa cha mtoto, ataambiwa utaratibu wa kufuata police report etc, atajaza fomu upya akifika sehemu ya majina atabadili jina la mwisho aondoe lako aweke atakalojisikia yeye, wakiwa makini watamuuliza na atatoa sababu na watamkubalia na atapata cheti kipya ndani ya siku 7, na wasipokuwa makini kumuuliza bado atapata cheti kipya ndani ya siku 7. Hakuna sheria inayomzuia mama kubadilisha jina la mtoto na kubadilisha cheti. Inaruhusiwa. Tena kama hajaandikishwa shule ni rahisi zaidi. Pia kisheria hata ukiwa mtu mzima unaruhusiwa kubadilisha jina mojawapo kwenye process ni kwenda kuapa mahakamani, ila watu wanakwepaga usumbufu sababu ya jina kusambaa kwenye vyeti,vitambulisho nk. USHAURI:, Kama hutaki mama wa mwanao abadili jina lake njia rahisi ni moja tu, tuma ela ya matumizi kila mwezi hata kama ni ndogo, hata akiolewa na mtu mwingine hawezi kubadili, vinginevyo awe na asili ya ushetani.
 
Shukrani sana hii ni elimu tosha kabisa.
 
Mkuu pole Sana Kwa changamoto hiyo, nianze Kwa kujibu swali la Kwanza, kwamba je anaweza kubadilisha cheti cha kuzaliwa au hapa, jibu NI ndiyo, Kwa sababu anao uwezo wakubadili jina la Baba Kwa kulikana mahakaman au akasingizia hawahi kupata cheti cha kuzaliwa, na anapatiwa cheti kingne Kwa sababu vyeti vya kuzaliwa havina picha na hata akienda kuomba kingne atapata Kwa sababu majina yatakuwa tofauti nacha Kwanza

Pili Kwa maono yangu, huyo mwanamke Kwanza siyo mwanamke sahihi wakufanya naye Maisha, Ni dhahiri hafai anakaa na mtoto wako sehem isiyojulikana.
Tatu, huenda huyo mwanamke anakutikisa kukuona uwezo wako, ila Iman yangu hawez kubadili majina total maana baadaye yatasumbua Hasa mashuleni na kwenye mifumo ya BIMA.

Mwishoni nikutake uwe makini Sana na mwanamke WA Aina hiyo, simamia Msimamo yako kuhusu mtoto na uhusiano wako na yeye kama wazazi

Sent from my Pixel 4 XL using JamiiForums mobile app
Safi kabisa napenda watu waelewa kama wewe mkuu unajibu maswali husika na elimu inaenda kwa jamii na ndio hadhi ya JF inaonekana nashukuru kwa mchango wako watu watajifunza na kuhusu uyo mwanamke ni dhahiri kuwa hafai kukaa na mwanaume na ndio maana ameachwa sasa pole ni kwa atakae shikishwa.
 
Kaa ukijua kwamba siri ya baba halisi wa mtoto anaijua mama mzazi.

Damu nzito kuliko jina. Tulia kama ni wako utajua mbeleni.

Kama we unamaindisha jina Lako kutumika ata kama mtoto si damu yako hapo sawa.

Child support unatoa lakini, isije ikawa unamtegea mzazi mwenzio malezi halafu unataka jina Lako liwekwe kwenye cheti
 
Back
Top Bottom