Je, mwanaume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,904
2,000
Marital Rape: Je, Mume anaweza kumbaka mke wake?

Ni ukweli unaokubalika ya kwamba Mume na Mke katika zama hizi za kisasa wako sawa kama ‘partners na kila mmoja akiwa na haki iliyo kamili kuhusiana na miili yao.

Sheria za hapo mwanzo (Old Laws) ziliweza kumlinda mume kutokana na mashtaka ya ' kumbaka mke wake. Sheria hizi zimefutwa kabisa katika maeneo mataifa mengi humu duniani mfano Mume anaweza kushtakiwa kwa kumbaka mke wake katika nchi kama Norway, Sweden, Denmark, Canada, majimbo mengi ya Marekani, Australia, Israel na iliyokuwa Urusi.

Tanzania kwa mujibu wa sheria za makosa ya kujamiiana, Mume anaweza kushitakiwa kwa kosa la kumbaka mke kama mmetengana (SOSPA 1998)

Yote niliyoelezea hapo juu kuhusu usawa yameainishwa vizuri na katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania (Bill of Rights- Sura 13) Kuhusu binadamu wote ni sawa.

Swali langu: Kulingana na maambukizo ya magonjwa yasiyotiba, Je kuna haja ya kufanya mabadiliko ya kisheria na kuweka kifungu kinachosema mume anaweza kumbaka mkewe?

Shadow.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,297
2,000
Mambo ya mahusiano ya unyumba yanafafanuliwa na Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971. Mume hawezi kumbaka mkewe. Kwa Tanzania, mwili wa mkeo ni halali yako kuutumia unavyopenda na unapo penda.

Kwa Islamic Sharia, ukimwacha mke kwa talaka moja au mbili, yaani Talaka Rejea. Ukimbaka ni sawa na kumrejea, ile talaka inafutika na anarejea kuendelea na ndoa yenu.

Japo haikuelezwa bayana na sheria yetu ya Makosa ya Kujamiiana. Wanaharakati wa Mtandao wa Jinsia (wengi wameachika ama ndio waliowaoa waume zao) walidhamiria kifungu cha mume kumbaka mkewe kiwepo lakini wanasheria wakakipinga kwa vile sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 hijabatilishwa na inasisitiza mume hawezi kumbaka mkewe.

Mmoja wa wanasheria mahiri wa Sheria ya Familia, Prof. Palamagamba Kabudi, amekiri mapungufu hayo na mengine mengi kwenye sheria yetu ya ndoa, lakini pia amesema hata mabadiliko yakija, 'itakuwa ni aibu kwa mwanamke wa kiafrika kusimama mahakamani na kudai amebakwa na mumewe'.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,944
2,000
Je Mume anaweza kumuua mkewe?
Je Mume anaweza kumchapa vibao mkewe?
Je Mume anaweza kumtukana mkewe?
Je mume anaweza kumfukuza mkewe?
Je Mume anaweza kumtumikisha mkewe?
Je Mume anaweza kuacha kuwa mume?

Tunauliza uwezo? Jibu ndiyo anaweza! Na kama swali ni kubaka ndiyo lakini kubaka ni kosa la jinai! So, kama mume anaweza kumbaka mkewe kwa sababu ni mke ina maana kuwa tunakubaliana na hoja kwamba mume anaweza kufanya kosa la jinai dhidi ya mke wake! Sasa huu ni uwezo au udhaifu?
 
Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,904
2,000
Mzee Mwanakijiji,
Kwa hiyo mwanakijiji unathibitisha ya kwamba kuna haja ya kuwa na madadiliko katika sheria zetu ili ziweze kuakisi sheria mama ( Katiba) kwamba binadamu wote ni sawa?

Kwamba wanawake wana uhuru wa kuamua kuhusu miili yao na kuachana na dhana ya sheria ya mwingereza ( Common Law) kwamba kiapo cha kanisani au kwa imamu ni makubaliano ya kudumu na mume haihitaji kuomba bali kujichumia hilo tunda hata kama ni bila ya ridhaa ya mke wake?

Naomba niweke wazi hapa kwamba nazungumzia sheria ya makosa ya jinai ( Penal Code as amended by SOSPA-1998) na si mahusiano katika ndoa( Marriage Act-1971).

Shadow.
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,474
2,000
Ayo mambo huko huko Ulaya apa bongo in practise mke ni kama personal belonging kwa watu wengi which is not good.
 
Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,736
2,000

Swali langu: Kulingana na maambukizo ya magonjwa yasiyotiba, Je kuna haja ya kufanya mabadiliko ya kisheria na kuweka kifungu kinachosema mume anaweza kumbaka mkewe?

Shadow.
...Nadhani hapo magonjwa yasotibikika ni kama UKIMWI.

..."When it is the person you have entrusted your life to who rapes you, it isn't just physical or sexual assault, it is a betrayal of the very core of your marriage, of your person, of your trust."

...ipo haja ya kupitisha sheria hiyo, kwani hapo ni kumuambukiza UKIMWI kwa makusudi.
 
Mwana wa Mungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2008
1,004
1,195
Ninao uelewa mkubwa kuhusu hili...

Mume hawezi kumbaka mkewe hata siku moja, isipokuwa kama mume na mke wametengana(separation) ndio inasemekana kuwa atakuwa amebakwa. Yaani, kuna wakati wanandoa wanaweza kushindana, wakaenda kuomba separation decree, ambayo mara nyingi haizidi miaka mitatu kwasababu inaweza kusababisha divorce,

Wakiwa kwenye separation kama hiyo inayotambulika kisheria, mume akimlazimisha mke kufanya tendo la ndoa ni sawa na kubaka na ni kosa la jinai, lakini kama hakuna separation wala divorce, mume anaweza kumlazimisha tu mkewe hata kama yuko mwezini au anaumwa na hakuna kosa lolote.

Siwezi kuongelea kiundani sana, wala siwezi kuongea kwa lugha ya kisheria hapa au kuweka vifungu na kesi zilizowahi kuamulia kama mfano, lakini ukweli ndio huo. hiyo analysis aliyoweka Mwanakijiji ni potofu kabisa, nafikiri Mwanakijiji aendelee kwenye field yake, sijui ya nini, hapo alipoeleza amechemka sana. Awaachie wenye field ya sheria waeleza hilo jambo. We don't need kulazimisha mambo, yamewekwa wazi na sheria, na haiwezi kubadilika labda bunge lifanye badiliko hilo.
 
Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,704
0
Sheria zote za kijinga kama hii ya mwanamume kuweza kushtakiwa kwa kumbaka mkewe ni matunda ya upumbavu wetu. Kinyemela matapeli ya nchi za magharibi yame tushawishi kuingiza sheria zenye nia ya kuvunja familia na sisi kama wendawazimu tume zikumbatia bila kujua nia hasa ya sheria hizo.

Sio siri tena kwamba divorce rates are extremely high kwa sababu ya mambo mengi ambayo tumeingiziwa kinyemela na kwamba kila mtu aliyeko kwenye ndoa leo anatamani kutoka! Hivi wewe utajisikiaaje una mtaka mkeo, halafu anakuambia sitaki, na wewe you are unable to do anything kwa vile unaogopa kwenda jela? It's an extrermely terrible situation to be in. Nadhani the next thing utakachokifikiria ni kutoka kwenye ndoa hiyo, no matter what!

Marital Rape Je Mume anaweza kumbaka mke wake?

Ni ukweli unaokubalika ya kwamba Mume na Mke katika zama hizi za kisasa wako sawa kama partners na kila mmoja akiwa na haki iliyo kamili kuhusiana na mihili yao.

Sheria za hapo mwanzo (Old Laws) ziliweza kumlinda mume kutukana na mashtaka ya kumbaka mke wake. Sheria hizi zimefutwa kabisa katika maeneo mataifa mengi humu duniani mfano Mume anaweza kustakiwa kwa kumbaka mke wake katika nchi kama Norway, Sweden, Denmark, Canada, majimbo mengi ya marekani, Australia, Israel na iliyokuwa Urusi.

Tanzania kwa mujibu wa sheria za makosa ya kujamiaana, Mume anaweza kushitakiwa kwa kosa la kumbaka mkeo kama mmetengana(SOSPA 1998)
Yote niliyoelezea hapo juu kuhusu usawa yamehainishwa vizuri na katiba ya Jam. ya Muungano ya Tanzania (Bill of Rights- Sura 13) Kuhusu binadamu wote ni sawa.

Swali langu: Kulingana na maambukizo ya magonjwa yasiyotiba, Je kuna haja ya kufanya mabadiliko ya kisheria na kuweka kifungu kinachosema mume anaweza kumbaka mkewe?

Shadow.
 
Babylon

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
1,338
1,195
Hapa namnukuu Pasco kwa kile alicho kisema eti katika dini ya kislam ukimwacha mke na kumuingilia hapo inakuwa umemrejea huo ni uongo ambao haufai au ni chuki za kidini kwani katika dini ya Kislam pindi mke ukisha mpa taka anakuwa sio mkeo tena na huruhusiwi kumuingia na ukifanya hivyo ni kufanya kosa la zinaa nakuomba uwe mkweli na uwaelimshe ya ukweli wale ambao hawajuwi nini kilichokuwemo katika uislam na ndoa
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,297
2,000
Hapa namnukuu Pasco kwa kile alicho kisema eti katika dini ya kislam ukimwacha mke na kumuingilia hapo inakuwa umemrejea huo ni uongo ambao haufai au ni chuki za kidini kwani katika dini ya Kislam pindi mke ukisha mpa taka anakuwa sio mkeo ena na huruhusiwi kumuingia na ukifanya hivyo ni kufanya kosa la zina nakuomba uwe mkweli na uwaelimshe ya ukweli wale ambao hawajuwi nini kilichokuwemo katika uwislam na ndowa
Ndugu yangu Babylon, chuki za kidini wapi. Nimezungumzia Talaka Rejea, ukimbaka mtalaka wako ndio umemrejea. Labda kama ni Talaka Tatu ndipo dini ya Kiislamu haikuruhusu kumrejea mpaka aolewe tena na mwanamume mwingine na aachike kwa Talaka Tatu ndipo unaweza sio kumrejea, bali kumuoa tena.
Babylon, na hii chuki?.
.
 
Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,904
2,000
Ndugu yangu Babylon, chuki za kidini wapi. Nimezungumzia Talaka Rejea, ukimbaka mtalaka wako ndio umemrejea. Labda kama ni Talaka Tatu ndipo dini ya Kiislamu haikuruhusu kumrejea mpaka aolewe tena na mwanamume mwingine na aachike kwa Talaka Tatu ndipo unaweza sio kumrejea, bali kumuoa tena.
Babylon, na hii chuki?.
.
Ndugu yangu Pasco, mimi naona hapo akikupeleka polisi unaweza kuanza kunyemelewa na kuta za keko. Tuwe makini katika hili. Kama mdau aliyesema hapo juu sheria ya kujamiaana ya mwaka 1998 inasema mume anaweza kumbaka mkewe baada ya kutengana. Angalia tusije tukapeleka ujumbe tata kwa wanajamii.

Shadow.
 
Violet

Member
Nov 17, 2008
99
0
Rape ni nini?
Kuna nchi nyingine ni kule kumgangania mtu mpaka akakubali ingawa msimamo wake wa kwanza ulikuwa NO. Hata kama baadae alienjoy nakufurahia. Kuna kijana alifungwa miaka 4, ingawa msichana ndio alikuwa anamfuatafuata, culture tofauti, akadhani labda anapendwa kumbe mwenzie alikuwa anataka urafiki tuu.

Kuwaelezea wazazi wake wakaita polisi. Kama TZ itabadilisha sheria, itategemea sana sana wata define vipi RAPE. Wengi wetu tunadhani ile ya kubaka mtu humjui, kutumia physical nguvu. Kuhusu kubaka MKE, sio lazima muwe mmetengana, ukiambiwa this night NO ni No, ila tatizo ya situation ya mke na mme ni kuthibitisha. Ndio mana watu wengi hawarepoti.
 
X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,640
1,250
Ndugu yangu Babylon, chuki za kidini wapi. Nimezungumzia Talaka Rejea, ukimbaka mtalaka wako ndio umemrejea. Labda kama ni Talaka Tatu ndipo dini ya Kiislamu haikuruhusu kumrejea mpaka aolewe tena na mwanamume mwingine na aachike kwa Talaka Tatu ndipo unaweza sio kumrejea, bali kumuoa tena.
Babylon, na hii chuki?.
.
Pasco! Icho unachokizungumza hakipo kwenye Uislam. Jaribu kuwa makini unapozungumza mambo ya kisheria. Usipoteze umma tafadhali.
Kama jambo hulifahamu bora kuuliza kwanza kuliko kuendelea kubisha usicho kifahamu na kukijuwa vema.

Kama kweli wewe mjuzi wa SHARIA za KIISLAM tufahamishe maana ya mwanamke kuachwa "Taraka tatu, pamoja na hizo taraka rejea zako."

Ndugu yetu hapa amekujibu vizuri sana, ila kwa sababu umejiandaa kiubishi ubishi, bado utaendelea kubisha tu, hata kama jambo si kweli.
Hapa namnukuu Pasco kwa kile alicho kisema eti katika dini ya kislam ukimwacha mke na kumuingilia hapo inakuwa umemrejea huo ni uongo ambao haufai au ni chuki za kidini kwani katika dini ya Kislam pindi mke ukisha mpa taka anakuwa sio mkeo ena na huruhusiwi kumuingia na ukifanya hivyo ni kufanya kosa la zina nakuomba uwe mkweli na uwaelimshe ya ukweli wale ambao hawajuwi nini kilichokuwemo katika uwislam na ndowa
 
Mwana wa Mungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2008
1,004
1,195
Jamanieee, nendeni kule website ya bunge, mkadownload " The Law of Marriage Act 1971",

Mkiisoma, hakuna maswali tena. Pia angalieni "Sexual Offences Special provisions Act ya mwaka 1998, inaongelea mambo ya kubakabaka hayo. Sheria ile imeongea kwa lugha ya kueleweka tu, hamna lugha ya kisheria sana. Kule mtapata na mambo mengine kama kumwingilia mke kinyume na maumbile kama ni kosa kubwa sana, pia mwanamume anayemruhusu mume mwenzie amuingilie na yule anayemuingilia pia (mashoga na walawiti) pia kuna adhabu zake kali sana hapa.

Hivi tukiona kina anti anti mtaani hapa, hasa tunavyosikia huko Tanga, Zanzibar na maeneo ya Dsm na Pwani wanaoamua kuwa mashoga au wanaowaingilia wake zao au wanawake wowote wale kinyume na maumbile, au wanaowalawiti wanaume wenzao kwa kuamua au kutokuamua, kuna adhabu zake kule SOSPA.

Asanteni.
 
MwM,

Mjadala hapa nispecific kuhusu suala la 'je mume anaweza kumbaka mkewe?" Je kuna haja ya kuibadili sheria zaidi na kuruhusu mke kuwa anatoa 'consent' kila anapoombwa unyumba?

Zingatia ya kwamba kwa tafsiri ya haraka haraka sheria ya Tanzania inasema mke ukubali kwa jumla kuhusiana na tendo la ndoa (consent) siku ya kufunga ndoa na itabadilika pale tu atakapokuwa ametengana na mumewe au kuachana (soma sheria ya makosa ya kujaamiiana -SOSPA 1998).

Shadow.
 
Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,901
1,225
Siku moja katika mazungumzo na rafiki yangu ambaye ni mbumbumbu wa sheria kama mimi , alinidokozea kwamba katika sheria ya makosa ya kujamiiana Tz ni makosa kwa mume kumbaka mke wake. Kwa wale wenye uelewa wa sheria naomba wanisaidie ufafanuzi wa yafuatayo ili nisije nikajikuta naenda jela bia kufahamu:-

1. Ni kweli kuna hiyo sheria inayomkataza mume kumbaka mke wake?
2. Ni kweli mume anaweza kumbaka mke wake?
3. Ni matendo au viashiria vipi vinavyookuwepo kuonyesha mume kambaka mke wake?
4. Je kuna uwezekano wa mke kumbaka mume wake?
5. Kama huo uwezekano upo, sheria inasemaje? Na ni zipi haki za mume aliyebakwa?

Nawasilisha.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom