Je, mwanaume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,285
2,000
Ulichoandika ni kweli kabisa.
Wabunge wetu[vyama vyote], hivi sasa tunapigana na gender violence na moja ya udhalilishaji mkubwa kwa wake zetu ni hili la kulazimisha tendo la ndoa hata kama mke hataki. Ukweli uliodhahiri ni kwamba hili kosa moja kubwa ambalo linaonekana kama la kawaida.
Hadi sasa ,Ghana,India,Indonesia,Jordan,Lesotho,Nigeria,Oman,Singapore, Sri lanka na Tanzania ndiyo nchi pekee zilizohalalisha kitendo hiki.
Wabunge kina mama, huu ndiyo wakati wenu wa kulisimamia hili [bila kujali itikadi] hadi hii sheria ya kishenzi iondolewe.
Mwanamke anaolewa ili afanywe sasa kama hataki au hajisikii kufanywa anafanya nini kwangu.Kama ni mke wangu atakua na excuse siku akiwa period tu hizo sababu nyingine hazina mashiko kwasababu je namimi mwanaume nisipojisikia kufanya naye mwaka mzima kutakua na ndoa hapo.Kumbuka mwanaume asipokua na uwezo wakumwingilia mkewe mke anaweza kuomba talaka.Kwa tafsiri hiyo hakuna kubakana mke na mume vinginevyo kuwe na mgogoro ambao kimsingi lazima wawe mbali mbali sio ndani ya nyumba yenye paa moja.Mambo mengine ya wazungu tuwaachie wenyewe.
 

Mgjd

JF-Expert Member
Feb 19, 2012
454
195
Kwanini uolewe wakati hutaki kufanya tendo la ndoa?
Kukubali kuolewa ni sawa ni kuhalalisha tendo la ndoa, haya mambo ya kuiga iga mambo ya western countries kuna muda inabidi tuwe makini

Sent using Jamii Forums mobile app
Eh, mwanamke aweza kukataa kumpa haki ya tendo la ndoa mumewe b8la sababu muhimu??? . Vinginevyo mpaka inafikia kubaka , hapo inaonekana kuna ukatili unaendelea kati yao..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

shuve

JF-Expert Member
Oct 11, 2012
314
250
Eh, mwanamke aweza kukataa kumpa haki ya tendo la ndoa mumewe b8la sababu muhimu??? . Vinginevyo mpaka inafikia kubaka , hapo inaonekana kuna ukatili unaendelea kati yao..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanamke anapo olewa inamaana ameridhia(consent) kufanya tendo la ndoa mda wowote labda Kama ni mgonjwa anaweza kukataa ila la sivyo hawezi kukataa na akikataa basi ni refusal consummation na ina weza kuwa sababisha separation mpaka divorce.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Johsal

Senior Member
Oct 23, 2014
158
250
Na vipi kuhusu....
1. Mwanamke lets say ana umri mkubwa akamlazimisha kijana mdogo kufanya nae mapenzi kwa nguvu (inatokea kwa wadada wa kazi na watoto wa kiume) akitishia kumpiga?

2. au kumnyima mshahara in case huyo mwanaume anakua ameajiriwa na huyo mwanamke.

Hii unaiwekaje mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kamdudu

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
552
500
Siku moja katika mazungumzo na rafiki yangu ambaye ni mbumbumbu wa sheria kama mimi , alinidokozea kwamba katika sheria ya makosa ya kujamiiana Tz ni makosa kwa mume kumbaka mke wake. Kwa wale wenye uelewa wa sheria naomba wanisaidie ufafanuzi wa yafuatayo ili nisije nikajikuta naenda jela bia kufahamu:-

1. Ni kweli kuna hiyo sheria inayomkataza mume kumbaka mke wake?
2. Ni kweli mume anaweza kumbaka mke wake?
3. Ni matendo au viashiria vipi vinavyookuwepo kuonyesha mume kambaka mke wake?
4. Je kuna uwezekano wa mke kumbaka mume wake?
5. Kama huo uwezekano upo, sheria inasemaje? Na ni zipi haki za mume aliyebakwa?

Nawasilisha.
ukikubali kuolewa sharti ulale bila nguo...
kwani maana ya kuoana ni nini ???
 

Masasaa

JF-Expert Member
Oct 23, 2015
452
500
MwM,

Mjadala hapa nispecific kuhusu suala la 'je mume anaweza kumbaka mkewe?" Je kuna haja ya kuibadili sheria zaidi na kuruhusu mke kuwa anatoa 'consent' kila anapoombwa unyumba?

Zingatia ya kwamba kwa tafsiri ya haraka haraka sheria ya Tanzania inasema mke ukubali kwa jumla kuhusiana na tendo la ndoa (consent) siku ya kufunga ndoa na itabadilika pale tu atakapokuwa ametengana na mumewe au kuachana (soma sheria ya makosa ya kujaamiiana -SOSPA 1998).

Shadow.
Hivi consent hapa ni ya mwanamke tu? Je mke hawezi mbaka mumewe? It should be both parties i think

Stay home, stay safe
Corona kills
 
Jun 27, 2019
8
45
Pasco! Icho unachokizungumza hakipo kwenye Uislam. Jaribu kuwa makini unapozungumza mambo ya kisheria. Usipoteze umma tafadhali.
Kama jambo hulifahamu bora kuuliza kwanza kuliko kuendelea kubisha usicho kifahamu na kukijuwa vema.

Kama kweli wewe mjuzi wa SHARIA za KIISLAM tufahamishe maana ya mwanamke kuachwa "Taraka tatu, pamoja na hizo taraka rejea zako."

Ndugu yetu hapa amekujibu vizuri sana, ila kwa sababu umejiandaa kiubishi ubishi, bado utaendelea kubisha tu, hata kama jambo si kweli.
Ndugu mbona mbishi sana na uislamu wako uchwala

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Babu Kingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
418
250
Ni kweli kuna hiyo sheria inayomkataza mume kumbaka mke wake?
KUNA MAMBO MENGINE YA KUTUNGA MWANADAM YANAPASUA KICHWA. MKE ULIPOMUOA MKAFUNGA NDOA ALISHAJUA ANACHOFUATA KWA MUME, NA MUME AMESHAHALALISHIWA TOKA SIKU HIYO ON WARDS... SASA KUBAKA KUNAKUJAJE???
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom