Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,577
- 5,265
Asante mkuu kwa kujibu!
Kwanza kabla ya kutoa hoja zangu, namimi niseme kitu!
Unajua mkuu, haya mambo ukiyajadili bila kuegamia upande wowote yanaleta raha sana. Kwa kweli kwangu mimi ni burudani tosha hii ninapoona watu kila hoja inayotolewa lazima ihojiwe. Safi sana na huu ndio u great thinker, hakuna kukubali kirahisi rahisi.
Sasa niende kwenye hoja!
Hili la kwanza unalozungumzia, ni kuwa kadiri ya wanaoamini Mungu, ni kuwa Mungu hana mwanzo wala mwisho, maana yake ni wa milele. Yaani kabla ya kuumba hata kitu kumoja, tayari alishakuwepo kwa kipindi Infinity kurudi nyuma. Sasa atuwezi tukasema kipindi infinity ni muda gani kwa kutaja kwa namba!! Yaani ni muda usiotamatika!!. Ona ilivyongumu ku visualize!!
Hoja yako ya pili, mkuu kadiri ya imani yako ni kuwa Mungu ni chanzo cha vitu vyooote. Sasa hapa pia tutahitaji utuelezee, Je, chanzo cha chanzo hicho ni kipi!?
Ndio, kila chanzo kina chanzo, angalia mfano huu, labda tuseme Chanzo cha kifo cha John Doe ni ajali, chanzo cha ajalu hiyo ni mwendo kasi wa dereva, chanzo cha mwendo kasi huo ni kulewa, chanzo cha ulevi wa dereva ni stress, chanzo cha stress, ni usaliti wa mkewe, chanzo cha usaliti wa mkewe ni... chanzo chanzo chanzompaka mwisho, na kujirudia rudia humohumo
.
Mambo haya yanafurahisha sana!!
Shida iliyopo mkuu ni kwamba sio ya kwamba muda hautamkiki bali ni muda usiojulikana na hii yote ni kutokana na namna binadamu tumeishia kutambua/ kukadiria muda baada ya kuwepo kwa ulimwengu na vilivyomo ndani ya ulimwengu. Hatuna uwezo wa kurudi nyuma kabla ya ulimwengu kuwepo na kutambua muda. Hata wanasayansi wanakadiria umri wa universe kwa kutumia reference ya tukio la bing bang, hawana uwezo wa kujua muda kabla ya tukio la bing bang. Kwahiyo kutojua muda uliotumika kabla hakutaweza kupata jibu la kile alichokuwa akikifanya ni kipi kwasababu inawezekana kumepishana sekunde tu mathalani.
Hoja ya pili ni kwamba ni kweli kwa mujibu wa mawazo yangu; Mungu maana yake ni chanzo cha uwepo wa vyote vilivyopo ulimwenguni. Yawezekana na yeye akawa na chanzo au asiwe na chanzo. kama atakuwa na chanzo basi hicho chanzo chake yeye kitakuwa na neno lingine kutofautisha kati yao. Uwezo wa binadamu umeishia kutambua ya kwamba chanzo/kisababishi cha ulimwengu na vilivyopo ulimwenguni linatumika neno Mungu. Je wewe waona ni kipi kilichosababisha uwepo wa vyote vilivyopo ulimwenguni?


