Je, Mungu ana sura ya mwanadamu?

Je, Mungu ana sura ya mwanadamu?

kiufupi MUNGU hana umbile la aina yoyote,si mtu,si mnyama,si upepo Wala si chochote.
Ila YUPO.

Anaweza kujibadilisha kwa mapenzi yake kuwa chochote kile au kutumia chochote kile kutimiza yaliyo mapenzi yake. Mungu ni muweza wa yote kwa mapenzi na matakwa yake. Kwa mfano alikuwa anashuka kama wingu la uwepo wa Mungu katika hema ya kukutania ya Wana wa Israeli. Alimtokea Musa pale Mlimani Sinai kama Moto katika kichaka, uko hapo?!
 
Kama ndio hivyo basi ni sahihi nikisema unaabudu usichokijua!
hapana .kwa Mimi muislam namjua mungu kupitia kwenye quran.na sina Shaka nae .maana dalili za uwepo wake zinaonekana.yupo vipi hapo anajua mwenyewe.
 
Anaweza kujibadilisha kwa mapenzi yake kuwa chochote kile au kutumia chochote kile kutimiza yaliyo mapenzi yake. Mungu ni muweza wa yote kwa mapenzi na matakwa yake. Kwa mfano alikuwa anashuka kama wingu la uwepo wa Mungu katika hema ya kukutania ya Wana wa Israeli. Alimtokea Musa pale Mlimani Sinai kama Moto katika kichaka, uko hapo?!
Kwa hyo huo Moto uliomtokea Musa ndo MUNGU?
 
Kwa hyo huo Moto uliomtokea Musa ndo MUNGU?

MUNGU muweza wa yote kwa mapenzi yake akamtokea Musa akiwa kama muujiza wa moto usio unguza kichaka pale Mlimani Sinai, wakati huo Musa alikuwa akichunga kondoo wa mkwewe Jethro. Kutoka sura ya 3 aya ya1 mpaka ya 6.
 
Acha uongo na Ujanja ujanja! Mtu huyo ni Bwana Yesu ndiye aliye mtokea katika maono/vision Yohana Mbatizaji akiwa kifungoni kisiwani Patmo. Na Yesu alishamwambia Petro hapo kabla ya kwamba nikitaka Yohana hata kufa mpaka nitakapo rudi mara ya pili. Yohana mwanafunzi aliyependwa sana na Bwana Yesu hakufa mpaka alipofunuliwa mambo ya siku za mwisho za kurudi kwa Bwana Yesu yatakavyo kuwa na akayasimulia na yanaishi kati yetu leo mpaka Yesu atakapo rudi.

Kwenye Biblia kuna umbo la mwanadamu ambalo Adam na Eva waliumbwa nalo ambalo ni ule mwili usio haribika. Na ulikuja kugeuka kuwa huu unao haribika baada ya anguko la dhambi pale bustani ya Eden na hukumu ilikuwa hii, "ulikuwa umavumbi na utarudi kuwa mavumbi." Tukifufuliwa kutoka wafu ile siku ya mwisho tutavaa ule usio haribika na kufanana na Mungu.

Lakini kwa nini kuhangaika kote huko kuijua sura ya Mungu. Bwana Yesu alikuwa hapa duniani akaishi kati ya wanadamu akiwa ni Mwanadamu kweli na vilevile Mungu kweli. Shetani anawachanganya wanadamu kwa hila yake kuu tu. Lakini kusema ukweli Mungu kaweka sura yake wazi hapo Mwanzo 1:28.

Kuweni makini sana na dini zinazo taka kupindisha ukweli wa Neno la Mungu maana niza shetani na ndiyo sifa kuu ya shetani baba wa uongo wote. Ampotoshe mwanadamu ili asiwe pekee yake jehanamu. Na kwa hili kafanikiwa kweli kweli anawapeleka kwa mabilioni huko jehanamu.
Hapo kwenye red umechanganya mambo.
Yohana Mbatizaji hakuwahi kufungwa kunako gereza la Patmo. Aliyefungwa kisiwani Patmo ni Yohana ndugu yake Yakobo - watoto wa Mzee mvuvi aitwaye Zebedayo. Yohana huyu ndiye mwandishi wa kitabu cha Ufunuo.
 
MUNGU muweza wa yote kwa mapenzi yake akamtokea Musa akiwa kama muujiza wa moto usio unguza kichaka pale Mlimani Sinai, wakati huo Musa alikuwa akichunga kondoo wa mkwewe Jethro. Kutoka sura ya 3 aya ya1 mpaka ya 6.
Mungu alimtokea mussa wakati anarudi kutoka nchi ya madian kurudi misri.
Sio wakati anachunga mifuko.hapo alikuwa amemaliza hyo kazi na kupewa mke .
 
MUNGU muweza wa yote kwa mapenzi yake akamtokea Musa akiwa kama muujiza wa moto usio unguza kichaka pale Mlimani Sinai, wakati huo Musa alikuwa akichunga kondoo wa mkwewe Jethro. Kutoka sura ya 3 aya ya1 mpaka ya 6.
Kuhusu mungu kugeuka moto.kuna mashaka.
Ila kila upande una kubali Musa aliongea na mungu.katika mlima Sinai.
Na hata mussa mwenyewe hakumuona mungu.
 
Mwanzo 1:26 Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa SURA yetu.
Nawakaribisha wadau kwa mjadala na kufundishana.
Mungu hayuko sehemu nyingine yuko ndani yako. You can be God or Satan. You can be David or Solomon, ni choice tu.
 
Hapo kwenye red umechanganya mambo.
Yohana Mbatizaji hakuwahi kufungwa kunako gereza la Patmo. Aliyefungwa kisiwani Patmo ni Yohana ndugu yake Yakobo - watoto wa Mzee mvuvi aitwaye Zebedayo. Yohana huyu ndiye mwandishi wa kitabu cha Ufunuo.

Si kumbuki kuandika neno Mbatizaji hata angalia reference za mbele za jina niloendelea kulitumia. Wewe msahihishaji/mhujumu maandishi yangu ulitakiwa ujue yuko Yohana na James ndugu wana wa Zebedayo wanafunzi wa Yesu. Yohana Mbatizaji hakuwahi kuwa mwanafunzi wa Yesu alikuwa ni sauti ya mtu aliae nyikani akitengeneza mapito ya Bwana Yesu na Roho wa Eliya alikuwa ndani yake. Na mapito yanayo ongelewa hapa usije ukafikiria ni Mabarabara kama haya aliotuachia JPM na wenzake walio tangulia, hata siyo. Bali alifanya ubatizo wa toba ya dhambi kwa Wayahudi ndio yale maneno yake tubuni mumgeukie Mungu wenu, mkaziache dhambi zenu...' Narudia tena kwa kusisitiza, sikumbuki kuandika neno Mbatizaji inawezekani ni uhuni wa shetani vilevile, bali na ijulikane kwa watu wote kwamba tulisha mshinda kupitia Bwana Yesu. Yeye na vikaragosi wake wote.
 
Kuhusu mungu kugeuka moto.kuna mashaka.
Ila kila upande una kubali Musa aliongea na mungu.katika mlima Sinai.
Na hata mussa mwenyewe hakumuona mungu.

Hakumuona kwa umbo lipi? Maana anajidhihirisha kwa maumbo mbalimbali. Bwana Yesu akiwa hapa duniani alikuwa ni Mungu katika mwili wa Mwanadamu. Na Bwana Yesu kwa Maneno Yake Mwenyewe aliwambia wanafunzi/wafuasi wake, "Aliye niona mimi amemuona Baba Yangu na akaongezea kama Baba alivyo ndani yangu na Mimi Ndani Yake na ninyi ndivyo mlivyo ndani yangu...." Hiyo statement ya Musa ni too general to... na imefungwa na mazingira iliyo ongelewa.
 
Mungu alimtokea mussa wakati anarudi kutoka nchi ya madian kurudi misri.
Sio wakati anachunga mifuko.hapo alikuwa amemaliza hyo kazi na kupewa mke .

Angalia vizuri usomaji wako wa Biblia
usisome ili kupata hoja za kuukosoa Ukristo na Mungu wa dini hiyo, ambaye ni Mungu wa Mbinguni muuamba mbingu, dunia, bahari na vyote vilivyomo ndani yake vizijazavyo, vinavyoonekana na visivyo onekana, uwe na uhakika kamwe hautabaki salama. Soma ili uelewe na upate neema ya kukombolewa kupitia imani kwa Bwana Yesu Kristo wa Nazareti aliye Hai maana neema hiyo ni ya bure tu.

Mungu alimwambia Musa ukitoka Misri utarudi na wana Waisraeli wakombolewa mniabudu hapa katika huu mlima. Na ndio hii unayongelea hapa ambayo ni mara ya pili aliporudi kutoka Misri inaonesha utii wa Musa na ule unabii wa Mungu kutimilizwa.
 
Angalia vizuri usomaji wako wa Biblia
usisome ili kupata hoja za kuukosoa ukristo na Mungu wa dini hiyo, ambaye ni Mungu wa Mbinguni muuamba mbingu, dunia, bahari na vyote vilivyomo ndani yake vizijazavyo, vinavyoonekana na visivyo onekana, uwe na uhakika kamwe hautabaki salama. Soma ili uelewa na upate neema ya kukombolewa kupitia imani maana neema hiyo ni ya bure tu.

Mungu alimwambia Musa ukitoka Misri utarudi na wana Waisraeli wakombolewa mniabudu hapa katika huu mlima. Na ndio hii unayongelea hapa ambayo ni mara ya pili aliporudi kutoka Misri inaonesha utii wa Musa na ule unabii wa Mungu kutimilizwa.
Unaweza ukaniambia Musa alikuwa ni dini gani
 
Hujambo!

2 Wakorintho 4:16
"Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku."

Na ndio alichomaanisha, na tumfanye mtu kwa mfano wetu na sura yetu.. Yaani huo utu wa ndani.. au kwa kiswahili cha moja kwa moja inafaa useme NA TUIFANYE ROHO (Maana huo ndio mfano kamili wa Mungu, na hiyo ndio sura/muonekano wake)..

Muonekano huu wa ndani, upo sawa kwa kila mwanadamu licha ya kutofautiana sura (wapo wenye sura pana, nyembamba, za duara, mchongoko, n.k) umbo, kimo, n.k

Utu wa nje ni huu mwili wa ndani, huu unachakaa na kuchoka na utabaki hapahapa duniani.

Utu wa ndani ni ROHO ZETU, hizi zitaishi milele, aidha kwenye Moto wa milele kwa zile roho ambazo zilikataa kumtii Muumbaji, au mbinguni kwa zile Roho zilizomtii Mungu.

Kiufupi Sana, mwanadamu nafsi iliyo hai, inaundwa na Mwili wa nyama (Utu wa nje/Unaoonekana) na Roho (Utu wa ndani/Usionekana kwa macho ya Mwilini.)
Hivi baada ya Mungu kusema " Tumfanye mtu kwa mfano wetu" alichokifanya/ kitengeneza au kiumba ni ROHO au ni MWILI?
Kama alitengeneza Mwili basi ndiyo mfano wao na kama alichotengeneza ni Roho basi ndiyo mfano wao.
 
Mwanzo 1:26
"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."

Kwanza kabisa, Mungu anaonekana anazungumza na mtu/watu ambao wanafanana maumbile na muonekano wao.. (Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; )

Hebu jiulize duniani tupo watu wangapi? Maelfu ya mamilioni bila shaka, na sote tunatofautiana sura zetu.. SWALI, Je Mungu Kama alimfanya mwanadamu kwa mfano wake, kwa sura yake kwanini wanadamu tunatofautiana?

Ili kupata JIBU la swali hili lazima tujiulize wanadamu WANAFANANA kitu gani? - Sura (Hapana), Maumbo (Hapana), Fikra (Hapana), Je kipi haswa wanafana Basi? Bila shaka ni ROHO.. Kila mwanadamu ana Roho, na hii ndio inawapa ufanano wanadamu.

Hivyo Basi, tumeomana wanadamu wanafana Roho.. bila shaka huu ndio mfano wa Mungu, hii ndio sura/muonekano wa Mungu.

Sasa Basi, tutizame Maandiko matakatifu yanasemaje, Mungu ana muonekano upi?

Kwa pamoja, sote tunaotamani kupata jibu la swali hili tuangalie kile kitabu cha mwanzo, ile sura ya kwanza ule mstari wa pili..

Mwanzo 1:2
"Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji."

Basi kumbe Maandiko matakatifu yanasema kuwa Mungu ni ROHO, Hapa sasa tunaona ya kuwa mfano wa Mungu na sura ya Mungu ndani yetu ni ROHO ZETU.
Hoja yako ina nguvu mno, na ninaamini kuwa Wanaaadamu wote wameunganishwa na roho, na ndio maana Roho huweza kuwasimamia na kuwaona popote pale walipo....ni roho pekee ndio aliyonayo mwanadamu ambayo viumbe wengine hawana..
 
Asante.

Ni kweli Yohana kipindi hiki alikuwa katika kisiwa cha patmo, na kuwa katika Roho alikomaanisha ni HALI YA KUWA KARIBU NA MUNGU, KUWA KATIKA USAFI, UCHAJI NA UTAUWA WA KIWANGO CHA JUU KIROHO, mtu akiwa katika hali hii tunasema yupo katika ulimwengu wa roho, ulimwengu ambao Mungu (Ambaye ni ROHO kamili) huwasiliana/kuzungumza na wanae kiroho... Hivyo Basi Yohana akiwa katika Roho, alipata kumuona huyo mtu mfano wa mwanadamu.. Pengine angekua katika hali ya mwili asingeweza kumuona.

Je mtu huyu alikua ni nani? Jibu liko hapa chini...

Ufunuo wa Yohana 1:17-18
"Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu."

Mtu huyo ili tumjue hebu tuangalie sifa zake, kimuonekano na zile alizotaja kwa maneno yake kama ilivyosikika kwa masikio na kuandikwa kwa mikono ya Yohana..

Mtu huyu kwanza, Anamuambia Yohana USIOGOPE... Hii ina maana Yeye Hana Hofu (Ameishinda hofu), Tujiulize ni mwanadamu gani hana hofu? Bila shaka yule hakuwa mwanadamu na ndio maana Yohana alisema aliona mtu, mfano wa mwanadamu.

Sifa ya pili, MIMI NI WA KWANZA NA WA MWISHO (ALPHA AND OMEGA), Je ni mwanadamu gani ambaye ni alpha and Omega? Hayupo.. Basi huyu hakuwa mwanadamu Bali ni mtu mfano wa mwanadamu..

Sifa ya tatu, ALIYE HAI, NAMI NALIKUWA NIMEKUFA... Huyu Bwana mkubwa bila shaka yeye ndiye MASIHA, Mwamba wa miamba, Alpha and Omega, Asiye na Hofu.

Sifa ya Nne, Yuko hai hata milele na milele.. Huyu ndiye MFALME wetu Yesu Kristo wa Nazareth.

Sifa ya tano, NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI NA ZA KUZIMU.. Hapa ndipo anapojitambulisha kwa UMUHIMU WA KULE KUFA NA KUFUFUKA KWAKE SIKU YA TATU... Yesu alikufa, Akazikwa AKASHUKA KATIKA WAFU, Huko alienda Kumnyang'anya shetani Mamlaka na Umiliki wa hizo funguo.

Basi bila shaka, Yohana akiwa katika ulimwengu wa roho alionana na kuongea na YESU KRISTO WA NAZARETH, BWANA WA MABWANA, MFALME WA WAFALME, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI, AKETIYE KUUME KWA MUNGU BABA, MWENYE USHIRIKA PAMOJA NASI KUPITIA ROHO MTAKATIFU, AMBAYE KWAKE TWAPATA UZIMA WA MILELE NA TUMAINI LA UHAI WETU..

Bila shaka nimejibu/Nimeeleza ulichotaka, Kama sivo ULIZA TENA.
Na hii ni hoja nzuri inayothibitisha kuwa Yesu alikuwepo kabla ya Ulimwengu kuumbwa, yaani kwa lugha za kidunia, kabla ya hata Bing Bang..
 
Kwanza na declair interest mimi ni Mkristo na nitatumia Biblia, maandiko mbalimbali ya kikristo, wanatheolojia mbalimbali, maono mbalimbali ya kikristo na yangu Binafsi kuhusu Mungu na kufanana na mwanadamu/Mtu.

NENO: MWANZO 1:26-28 Mungu anasema na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu. Hapa aliongea na watoto wake wa kimbingu kabla ya uumbaji wa mwanadamu. Wana aliokuwa anaongea nao ni viumbe wa kiroho yaani malaika, maserafi, makerubi n.k. Ukisoma Biblia watumishi wa Mungu waliowahi Kutana na malaika walikuwa na sura (Image) na maumbo ya kibinadamu(Image) na sio wanyama.

Watumishi wa Mungu manabii na mitume waliobahatika kumuona Mungu alijifunua kwao kama (Image) mtu/mwanadamu Toka Isaya, Daniel tena alimuona "kama mzee wa siku" hadi Nabii Yohana walimuona "mmoja aliye mfano wa Mwanadamu"(Image)

Hata mimi binafsi nishawahi muona "mmoja aliye mfano wa Mwanadamu (Image)

Kwa hiyo, Mungu anafanania (Image) mwanadamu na hii ipo wazi kwani kabla ya anguko la mwanadamu. Mwanadamu alikuwa mtawala wa dunia na Mungu alimpa atawale kama ambavyo yeye anatawala Mbinguni na hata mwanaye wa pekee a.k.a mwana wa Mmiliki alikuja na kukaa duniani kwa Image kama mwanadamu.
Kuna vitu unachanganya, mkuu na kuna vitu upo sahihi
 
Hivi baada ya Mungu kusema " Tumfanye mtu kwa mfano wetu" alichokifanya/ kitengeneza au kiumba ni ROHO au ni MWILI?
Kama alitengeneza Mwili basi ndiyo mfano wao na kama alichotengeneza ni Roho basi ndiyo mfano wao.

Jibu liko hapo Mwanzo Sura ya 2 aya ya 7.
 
Mungu hafananishwi na mwanadamu bali labda afananishwe na mtu(roho) maana mtu anaishi ndani ya mwanadamu(ni roho) spiriti..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom