Je, Mungu ana sura ya mwanadamu?

Je, Mungu ana sura ya mwanadamu?

Tofauti ni uelewa

Mwanzo 1:26-27
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”.


Kwa mfano wetu ni kusema utu na tabia mienendo.

Mungu alimuumba mwanadamu akampa pumzi, akili, maarifa nk na kumpa majukumu ya kutawala na kuendeleza uumbaji wa vitu duniani. Na ndio maana wanadamu wote tunapata kibali cha kuzaliwa tunatakiwa kuishi kwa kufanya na kukamilisha kile Mungu alichokusudia kwetu mwisho tuondoke.

Na uumbaji katika ulimwengu huu unaendelea kwa wanadamu kutumia karama/vipaji akili na maarifa waliyogaiwa na Mungu. Sasa hivi mwanadamu nae anaumba machines mbalimbali na robots kufanya kile anachokitaka yeye. Na anaziprogram hizo machines na roborts kufanya tuu yale aliyoagiza yeye na sio vinginevyo; kama vile wanadamu tulivyokua programmed na Mungu kupitia maandiko matakatifu ya imani zetu

Je, tunaweza kusema gari linalofanya safari na kubeba mizigo kwa niaba ya mwanadamu au machines, au robots mbalimbali zina kichwa, macho, miguu na moyo kama alivyo mwanadamu??

Hujaelezea kwa Sura yetu
 
Kwanza na declair interest mimi ni Mkristo na nitatumia Biblia, maandiko mbalimbali ya kikristo, wanatheolojia mbalimbali, maono mbalimbali ya kikristo na yangu Binafsi kuhusu Mungu na kufanana na mwanadamu/Mtu.

NENO: MWANZO 1:26-28 Mungu anasema na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu. Hapa aliongea na watoto wake wa kimbingu kabla ya uumbaji wa mwanadamu. Wana aliokuwa anaongea nao ni viumbe wa kiroho yaani malaika, maserafi, makerubi n.k. Ukisoma Biblia watumishi wa Mungu waliowahi Kutana na malaika walikuwa na sura (Image) na maumbo ya kibinadamu(Image) na sio wanyama.

Watumishi wa Mungu manabii na mitume waliobahatika kumuona Mungu alijifunua kwao kama (Image) mtu/mwanadamu Toka Isaya, Daniel tena alimuona "kama mzee wa siku" hadi Nabii Yohana walimuona "mmoja aliye mfano wa Mwanadamu"(Image)

Hata mimi binafsi nishawahi muona "mmoja aliye mfano wa Mwanadamu (Image)

Kwa hiyo, Mungu anafanania (Image) mwanadamu na hii ipo wazi kwani kabla ya anguko la mwanadamu. Mwanadamu alikuwa mtawala wa dunia na Mungu alimpa atawale kama ambavyo yeye anatawala Mbinguni na hata mwanaye wa pekee a.k.a mwana wa Mmiliki alikuja na kukaa duniani kwa Image kama mwanadamu.
Ni lini Mwenyezi Mungu aliwapa malaika/maserafi/makerubi uwezo wa kushirikiana naye (Mungu) katika kuumba/kufanya?
 
Kwanza na declair interest mimi ni Mkristo na nitatumia Biblia, maandiko mbalimbali ya kikristo, wanatheolojia mbalimbali, maono mbalimbali ya kikristo na yangu Binafsi kuhusu Mungu na kufanana na mwanadamu/Mtu.

NENO: MWANZO 1:26-28 Mungu anasema na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu. Hapa aliongea na watoto wake wa kimbingu kabla ya uumbaji wa mwanadamu. Wana aliokuwa anaongea nao ni viumbe wa kiroho yaani malaika, maserafi, makerubi n.k. Ukisoma Biblia watumishi wa Mungu waliowahi Kutana na malaika walikuwa na sura (Image) na maumbo ya kibinadamu(Image) na sio wanyama.

Watumishi wa Mungu manabii na mitume waliobahatika kumuona Mungu alijifunua kwao kama (Image) mtu/mwanadamu Toka Isaya, Daniel tena alimuona "kama mzee wa siku" hadi Nabii Yohana walimuona "mmoja aliye mfano wa Mwanadamu"(Image)

Hata mimi binafsi nishawahi muona "mmoja aliye mfano wa Mwanadamu (Image)

Kwa hiyo, Mungu anafanania (Image) mwanadamu na hii ipo wazi kwani kabla ya anguko la mwanadamu. Mwanadamu alikuwa mtawala wa dunia na Mungu alimpa atawale kama ambavyo yeye anatawala Mbinguni na hata mwanaye wa pekee a.k.a mwana wa Mmiliki alikuja na kukaa duniani kwa Image kama mwanadamu.
[emoji736][emoji736][emoji736]
 
Asante.

Ni kweli Yohana kipindi hiki alikuwa katika kisiwa cha patmo, na kuwa katika Roho alikomaanisha ni HALI YA KUWA KARIBU NA MUNGU, KUWA KATIKA USAFI, UCHAJI NA UTAUWA WA KIWANGO CHA JUU KIROHO, mtu akiwa katika hali hii tunasema yupo katika ulimwengu wa roho, ulimwengu ambao Mungu (Ambaye ni ROHO kamili) huwasiliana/kuzungumza na wanae kiroho... Hivyo Basi Yohana akiwa katika Roho, alipata kumuona huyo mtu mfano wa mwanadamu.. Pengine angekua katika hali ya mwili asingeweza kumuona.

Je mtu huyu alikua ni nani? Jibu liko hapa chini...

Ufunuo wa Yohana 1:17-18
"Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu."

Mtu huyo ili tumjue hebu tuangalie sifa zake, kimuonekano na zile alizotaja kwa maneno yake kama ilivyosikika kwa masikio na kuandikwa kwa mikono ya Yohana..

Mtu huyu kwanza, Anamuambia Yohana USIOGOPE... Hii ina maana Yeye Hana Hofu (Ameishinda hofu), Tujiulize ni mwanadamu gani hana hofu? Bila shaka yule hakuwa mwanadamu na ndio maana Yohana alisema aliona mtu, mfano wa mwanadamu.

Sifa ya pili, MIMI NI WA KWANZA NA WA MWISHO (ALPHA AND OMEGA), Je ni mwanadamu gani ambaye ni alpha and Omega? Hayupo.. Basi huyu hakuwa mwanadamu Bali ni mtu mfano wa mwanadamu..

Sifa ya tatu, ALIYE HAI, NAMI NALIKUWA NIMEKUFA... Huyu Bwana mkubwa bila shaka yeye ndiye MASIHA, Mwamba wa miamba, Alpha and Omega, Asiye na Hofu.

Sifa ya Nne, Yuko hai hata milele na milele.. Huyu ndiye MFALME wetu Yesu Kristo wa Nazareth.

Sifa ya tano, NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI NA ZA KUZIMU.. Hapa ndipo anapojitambulisha kwa UMUHIMU WA KULE KUFA NA KUFUFUKA KWAKE SIKU YA TATU... Yesu alikufa, Akazikwa AKASHUKA KATIKA WAFU, Huko alienda Kumnyang'anya shetani Mamlaka na Umiliki wa hizo funguo.

Basi bila shaka, Yohana akiwa katika ulimwengu wa roho alionana na kuongea na YESU KRISTO WA NAZARETH, BWANA WA MABWANA, MFALME WA WAFALME, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI, AKETIYE KUUME KWA MUNGU BABA, MWENYE USHIRIKA PAMOJA NASI KUPITIA ROHO MTAKATIFU, AMBAYE KWAKE TWAPATA UZIMA WA MILELE NA TUMAINI LA UHAI WETU..

Bila shaka nimejibu/Nimeeleza ulichotaka, Kama sivo ULIZA TENA.

Acha uongo na Ujanja ujanja! Mtu huyo ni Bwana Yesu ndiye aliye mtokea katika maono/vision Yohana Mbatizaji akiwa kifungoni kisiwani Patmo. Na Yesu alishamwambia Petro hapo kabla ya kwamba nikitaka Yohana hata kufa mpaka nitakapo rudi mara ya pili. Yohana mwanafunzi aliyependwa sana na Bwana Yesu hakufa mpaka alipofunuliwa mambo ya siku za mwisho za kurudi kwa Bwana Yesu yatakavyo kuwa na akayasimulia na yanaishi kati yetu leo mpaka Yesu atakapo rudi.

Kwenye Biblia kuna umbo la mwanadamu ambalo Adam na Eva waliumbwa nalo ambalo ni ule mwili usio haribika. Na ulikuja kugeuka kuwa huu unao haribika baada ya anguko la dhambi pale bustani ya Eden na hukumu ilikuwa hii, "ulikuwa umavumbi na utarudi kuwa mavumbi." Tukifufuliwa kutoka wafu ile siku ya mwisho tutavaa ule usio haribika na kufanana na Mungu.

Lakini kwa nini kuhangaika kote huko kuijua sura ya Mungu. Bwana Yesu alikuwa hapa duniani akaishi kati ya wanadamu akiwa ni Mwanadamu kweli na vilevile Mungu kweli. Shetani anawachanganya wanadamu kwa hila yake kuu tu. Lakini kusema ukweli Mungu kaweka sura yake wazi hapo Mwanzo 1:28.

Kuweni makini sana na dini zinazo taka kupindisha ukweli wa Neno la Mungu maana niza shetani na ndiyo sifa kuu ya shetani baba wa uongo wote. Ampotoshe mwanadamu ili asiwe pekee yake jehanamu. Na kwa hili kafanikiwa kweli kweli anawapeleka kwa mabilioni huko jehanamu.
 
Kwa hiyo tofauti ni kwamba quran ipo katika lugha ya kiarabu na injili na torati zipo katika lugha za mataifa tofauti, swali ni je una uhakika gani kwamba torati na injili zenye lugha asilia hazipo?
Pili kusoma quran koran kwa lugha ya kiarabu sio hoja, hoja ni je unailewa?

Soma hapo Matendo ya Mitume sura ya 2 mistari/aya za 1 mpaka 13. Habari kuu ni kuja/ kuteremshwa kwa Roho Mtakatifu aka Roho wa Mungu kutoka Mbinguni kuja hapa duniani kwa wanafunzi/ wafuasi wa Bwana Yesu ili aishinao kama Msaidizi na Mfariji wa karibu. Hii ilikuwa ni ahadi ya Bwana Yesu kwao kabla ya kuteswa, kufa, kufufuka, kukaa kati yao kwa siku arobaini na kupaa kurudi mbinguni. Waliipata hiyo Neema Kuu na ahadi kutimia siku kumi tu baada ya Bwana Yesu kupaa. Hawa walinena kwa lugha mpya kushuhudia Matendo Makuu ya Mungu kwa wanadamu. Kumbuka hawa walikuwa ni wayahudi lakini wakinena kwa lugha za mataifa yote ya dunia hii.
Kwa sababu na namna iyo hiyo walioandika Biblia sisi Wakristo tunaamini kupitia Roho wa Mungu kwamba walioongozwa na Roho Mtakatifu.

Mungu wa Biblia yaani Mungu wa Mbinguni sio wa lugha moja. Na alionesha uwezo huo pale kwenye mnara wa Babeli. Huwezi kuwapiga watu wako kwa pigo la kuchanganya lugha/ndimi zao ili baadaye usiwe na uwezo wa kuwasikia na kuwasiliana nao kwa lugha hizo. Bali uwe na uwezo wa eti lugha moja kati ya hizo maelfu, kiarabu chaa!

Na ieleweke kwa wasomaji wote ya kuwa Matendo ya Mitume waweza kuyaita pia ni Matendo ya Roho wa Mungu yalivyo jidhirisha/ Manifestion kwa wanafunzi wa Yesu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom