Mkuu yohana alikuwa katika roho na akaona mtu mfano wa mwanadamu, unaweza ukaelezea hiyo;
Ufunuo wa Yohana : 1 : 13 - na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
via
OneLink.To
Asante.
Ni kweli Yohana kipindi hiki alikuwa katika kisiwa cha patmo, na kuwa katika Roho alikomaanisha ni HALI YA KUWA KARIBU NA MUNGU, KUWA KATIKA USAFI, UCHAJI NA UTAUWA WA KIWANGO CHA JUU KIROHO, mtu akiwa katika hali hii tunasema yupo katika ulimwengu wa roho, ulimwengu ambao Mungu (Ambaye ni ROHO kamili) huwasiliana/kuzungumza na wanae kiroho... Hivyo Basi Yohana akiwa katika Roho, alipata kumuona huyo mtu mfano wa mwanadamu.. Pengine angekua katika hali ya mwili asingeweza kumuona.
Je mtu huyu alikua ni nani? Jibu liko hapa chini...
Ufunuo wa Yohana 1:17-18
"Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu."
Mtu huyo ili tumjue hebu tuangalie sifa zake, kimuonekano na zile alizotaja kwa maneno yake kama ilivyosikika kwa masikio na kuandikwa kwa mikono ya Yohana..
Mtu huyu kwanza, Anamuambia Yohana USIOGOPE... Hii ina maana Yeye Hana Hofu (Ameishinda hofu), Tujiulize ni mwanadamu gani hana hofu? Bila shaka yule hakuwa mwanadamu na ndio maana Yohana alisema aliona mtu, mfano wa mwanadamu.
Sifa ya pili, MIMI NI WA KWANZA NA WA MWISHO (ALPHA AND OMEGA), Je ni mwanadamu gani ambaye ni alpha and Omega? Hayupo.. Basi huyu hakuwa mwanadamu Bali ni mtu mfano wa mwanadamu..
Sifa ya tatu, ALIYE HAI, NAMI NALIKUWA NIMEKUFA... Huyu Bwana mkubwa bila shaka yeye ndiye MASIHA, Mwamba wa miamba, Alpha and Omega, Asiye na Hofu.
Sifa ya Nne, Yuko hai hata milele na milele.. Huyu ndiye MFALME wetu Yesu Kristo wa Nazareth.
Sifa ya tano, NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI NA ZA KUZIMU.. Hapa ndipo anapojitambulisha kwa UMUHIMU WA KULE KUFA NA KUFUFUKA KWAKE SIKU YA TATU... Yesu alikufa, Akazikwa AKASHUKA KATIKA WAFU, Huko alienda Kumnyang'anya shetani Mamlaka na Umiliki wa hizo funguo.
Basi bila shaka, Yohana akiwa katika ulimwengu wa roho alionana na kuongea na YESU KRISTO WA NAZARETH, BWANA WA MABWANA, MFALME WA WAFALME, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI, AKETIYE KUUME KWA MUNGU BABA, MWENYE USHIRIKA PAMOJA NASI KUPITIA ROHO MTAKATIFU, AMBAYE KWAKE TWAPATA UZIMA WA MILELE NA TUMAINI LA UHAI WETU..
Bila shaka nimejibu/Nimeeleza ulichotaka, Kama sivo ULIZA TENA.