Je, Mungu ana sura ya mwanadamu?

Je, Mungu ana sura ya mwanadamu?

Hahahahah.

Nakukaribisha Sana Mkuu, ila uandishi Kama huu hata shetani huwezi kumshinda, maana anaijua vema Biblia Takatifu.

Rudia tena kwa kuongezea vifungu mbalimbali vya kusapoti maelezo yako, ukifanya hivyo INAKUWA RAHISI HATA KWA YULE AMBAYE SI MWAMINI KUELEWA na KUAMINI.
Haya hongera na kuwa na siku njema maana naona unashindana.
 
Haya hongera na kuwa na siku njema maana naona unashindana.
Kwanini unasema ninashindana?

Bila shaka unahisi unao ushindani ndani yako... Mimi naongea kwa faida ya wote.

Ukiweka vifungu kwanza unaweka uzito kwenye maelezo yako (Unaepusha zile blah blah) lakini pia Unawafanya wasio amini waamini, na mwisho inaonyesha namna gani uko kwenye njia sahihi kiimani.

Hatushindani, hata Kama wewe unaona au unahisi hivyo.
 
HII QUR AN LEO HII AJE MTU KUTOKA POPOTE DUNIANI ATAKUSOMEA QUR AN HII HII TUNAYOISOMA TZ

KITU AMBACHO HUWEZI KUKIPATA KWENYE INJILI AMA TORATI YA LEO KILA TAIFA KIVYAKE KITABU KILICHOBAKI SALAMA NI QUR AN PEKE YAKE

Kwa hiyo tofauti ni kwamba quran ipo katika lugha ya kiarabu na injili na torati zipo katika lugha za mataifa tofauti, swali ni je una uhakika gani kwamba torati na injili zenye lugha asilia hazipo?
Pili kusoma quran koran kwa lugha ya kiarabu sio hoja, hoja ni je unailewa?
 
Mwanzo 1:26 Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa SURA yetu.
Nawakaribisha wadau kwa mjadala na kufundishana.
Swali zuri.
Ila nadhani umeuliza hivyo kwa Mujibu kama inavyoelezwa katika kitabu Biblia.
Yaani Torati, Zaburi na Injiri.
Wabudha, Wahindu na hata Waislamu hili swali haliwahusu kabisa.
Vitabu vyao havisemi kama ulivyo nukuu hilo andiko la hoja yako ya msingi.
Swali ninawahusu Wayahudi na Wakristo pekee.

Narudi kuchangia mada.
 
Kusema maneno hayo haikuwa na maana kuwa binadamu tuliumbwa kwa kufanana na Mungu bali hapa kilichomaanishwa ni ule uwezo wa kutambua mema na mabaya
 
ni kweli Mungu alituumba wanadamu kwa mfano(utukufu) wake. Kwanini? ili akatawale vilivyomo duniani ~(Dominion), km yy atawalivyo kila kitu. Lakini mwanadamu anabaki kweny nafasi ya utawala(mamlaka) endapo tu atabaki kweny kuumbwa kwa mfano/sura/utukufu wa Mungu! Sura ya Mungu ndiyo ile waliokua nayo adam na hawa bustanini Eden,shetani aljua siri hii ndio maana akapenyeza dhambi ili kuondoa utukufu wa Mungu ndani yetu,kwa lugha nyingine dhambi inaleta sura mpya ya mtu ktk ulimwengu wa roho! uktaka kuendlea kubaki na sura ya Mungu ni mpaka pale utakapomkiri yeye na kuenenda ktk neno lake. Wote tumepungukiwa utukufu wa Mungu
 
HII QUR AN LEO HII AJE MTU KUTOKA POPOTE DUNIANI ATAKUSOMEA QUR AN HII HII TUNAYOISOMA TZ

KITU AMBACHO HUWEZI KUKIPATA KWENYE INJILI AMA TORATI YA LEO KILA TAIFA KIVYAKE KITABU KILICHOBAKI SALAMA NI QUR AN PEKE YAKE
Unaongea kama illiterate hujajibu swali!!

Umeulizwa iweje kitabu kipya kitumike kupima kitabu kikongwe zaidi yake??

And not vice versa?

Hafu ni nani kakuambia biblia zinatifautiana

Scripts ni hizohizo hakuna mabadiliko tofauti zinakuja kwenye translations

Unaona quaran iko uniform sababu mnatumia kwenye original language

Ila ukitafsiri tofauti lazima zije kutokana na weakness ya baadhi ya lugha katika kutoa maelezo fulani, ndiomaana kwa wasomj wa biblia kama kuna sehemu kwenye lugha mahalia inaleta utata unaangali je kwenye latin,au hebrew ilitumikaje na ilimaanisha nini
 
Mwanzo 1:26 Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa SURA yetu.
Nawakaribisha wadau kwa mjadala na kufundishana.
Kwa Imani ya KIISLAM na kwa kufuata mafundisho ya Quran
MUNGU ni Moja, hana mshirika, hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hafanani na kitu chochote
Huo ndio msimamo wa waaaislam kumuhusu Mungu
 
Kwa Imani ya KIISLAM na kwa kufuata mafundisho ya Quran
MUNGU ni Moja, hana mshirika, hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hafanani na kitu chochote
Huo ndio msimamo wa waaaislam kumuhusu Mungu

Mkuu koran inaposema hafanani na kitu chochote tafsiri yake ni kwamba mnaabudu msichokijua
 
Kama mshapata kujua sura yake, basi naombeni mnijuze kwenye hiyo sura yake, race yake ni ipi?
 
Sura vs uso

Tofautisha
Kwamba kuna uwezekano akawa na kimoja hapo?

Una maanisha hana uso?
Tofauti ni nini?
Tofauti ni uelewa

Mwanzo 1:26-27
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”.


Kwa mfano wetu ni kusema utu na tabia mienendo.

Mungu alimuumba mwanadamu akampa pumzi, akili, maarifa nk na kumpa majukumu ya kutawala na kuendeleza uumbaji wa vitu duniani. Na ndio maana wanadamu wote tunapata kibali cha kuzaliwa tunatakiwa kuishi kwa kufanya na kukamilisha kile Mungu alichokusudia kwetu mwisho tuondoke.

Na uumbaji katika ulimwengu huu unaendelea kwa wanadamu kutumia karama/vipaji akili na maarifa waliyogaiwa na Mungu. Sasa hivi mwanadamu nae anaumba machines mbalimbali na robots kufanya kile anachokitaka yeye. Na anaziprogram hizo machines na roborts kufanya tuu yale aliyoagiza yeye na sio vinginevyo; kama vile wanadamu tulivyokua programmed na Mungu kupitia maandiko matakatifu ya imani zetu

Je, tunaweza kusema gari linalofanya safari na kubeba mizigo kwa niaba ya mwanadamu au machines, au robots mbalimbali zina kichwa, macho, miguu na moyo kama alivyo mwanadamu??
 
Mungu ni Roho kamili haba mwili.
(Mwanzo 1:2)

Aliposema tumfanye mtu kwa mfano wetu, na sura yetu. Alimaanisha mfano wa yeye (ROHO), na ndio maana licha ya wanadamu kutofautiana kimwili sote tunafanana na MUNGU kwa Roho.

Hivyo mfanano wa sisi na Mungu ni ROHO ZETU.
Lakin hapo haoo huwa tunaskia kwamba huyu ana roho mbaya huyu ana roho nzuri..Sasa hata roho mbona binadam tunatofautiana??
 
Lakin hapo haoo huwa tunaskia kwamba huyu ana roho mbaya huyu ana roho nzuri..Sasa hata roho mbona binadam tunatofautiana??

Unajua machines zimetengenezwa na binadamu? Ulishawahi fanya kazi na machines tofauti tofauti zikakupa matokeo ambayo hukutegemea? Ulishawahi endesha gari break zikafail ukaumia au gari ikaumia na kuumiza? Ulishawahi sikia ndege imeanguka na kuteketea?

Hayo yote ndio sawa na roho nzuri vs mbaya kwa binadamu. Unaposhindwa kufuata maelekezo ndipo unapoharibu
 
Unajua machines zimetengenezwa na binadamu? Ulishawahi fanya kazi na machines tofauti tofauti zikakupa matokeo ambayo hukutegemea? Ulishawahi endesha gari break zikafail ukaumia au gari ikaumia na kuumiza? Ulishawahi sikia ndege imeanguka na kuteketea?

Hayo yote ndio sawa na roho nzuri vs mbaya kwa binadamu. Unaposhindwa kufuata maelekezo ndipo unapoharibu
Namalizia kuandaa script ya kukutongoza uwe demu wangu
 
Mwanzo 1:26
"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."

Kwanza kabisa, Mungu anaonekana anazungumza na mtu/watu ambao wanafanana maumbile na muonekano wao.. (Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; )

Hebu jiulize duniani tupo watu wangapi? Maelfu ya mamilioni bila shaka, na sote tunatofautiana sura zetu.. SWALI, Je Mungu Kama alimfanya mwanadamu kwa mfano wake, kwa sura yake kwanini wanadamu tunatofautiana?

Ili kupata JIBU la swali hili lazima tujiulize wanadamu WANAFANANA kitu gani? - Sura (Hapana), Maumbo (Hapana), Fikra (Hapana), Je kipi haswa wanafana Basi? Bila shaka ni ROHO.. Kila mwanadamu ana Roho, na hii ndio inawapa ufanano wanadamu.

Hivyo Basi, tumeomana wanadamu wanafana Roho.. bila shaka huu ndio mfano wa Mungu, hii ndio sura/muonekano wa Mungu.

Sasa Basi, tutizame Maandiko matakatifu yanasemaje, Mungu ana muonekano upi?

Kwa pamoja, sote tunaotamani kupata jibu la swali hili tuangalie kile kitabu cha mwanzo, ile sura ya kwanza ule mstari wa pili..

Mwanzo 1:2
"Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji."

Basi kumbe Maandiko matakatifu yanasema kuwa Mungu ni ROHO, Hapa sasa tunaona ya kuwa mfano wa Mungu na sura ya Mungu ndani yetu ni ROHO ZETU.
sura siyo roho mkuu,hapo wangetoa neno kwa sura yetu wakaweka kwa roho yetu Ila ndo hivyo walioandika washajichanganya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom