Je, Mungu aliumba dunia kwa miaka Elfu 6?

Je, Mungu aliumba dunia kwa miaka Elfu 6?

Wewe ndiye utalaanika muda sio mrefu, omba msamaha mapema.

Huyo Mirza Ghulam Ahmad (as), naapa kwa yule Allah ambaye maisha yangu yapo mikononi mwake, huyo ni nabii wake, Allah kamtuma kuja kuwaunganisha Waisilamu wote na kuifanya Islamu itamalaki dunia nzima, huyo Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad (as) ni nabii mfuasi aliyetabiriwa na kipenzi chetu Mtukufu wa daraja Mtume Muhammad (saw) kufika katika zama hizi, kejeli dhidi yake ni kujitafutia laana kubwa, na nilipata kukuonya kwamba kwa wewe kuendelea kumtusi na kumkejeli Hadhrat Ahmad (as) NI WEWE PEKEE KATIKA HII DUNIA UTABAKI KUWA SALAMA, wapo watu wenye nguvu kubwa walijaribu lakini Allah aliwaangamiza kwa fedheha kubwa na jumuiya ya waisilamu wa Ahmadiyya inazidi kupeta, kila mwaka wanajiunga malaki ya watu na jumuiya hii ndiyo jumuiya inayokuwa kwa kasi kubwa kuliko jumuiya za dini zote duniani.

Rai yangu ya upendo kwako ni hii:--

---Acha matusi na kejeli kwani huo sio Uisilamu.
---Allah pekee ndiye anayetujua undani wetu zaidi ya sisi tunavyojijua.
---Allah ndiye mjuzi wa kila kitu, naye anamjua vyema Hadhrat Ahmad (as) kuliko mimi na wewe.
----Fanya hichi kitu: amka usiku na swali swala ya Tahajjud kwa unyenyekevu, kwa kumlilia Allah ili akuonyeshe UKWELI au UONGO wa Hadhrat Mirza, mimi ninakuambia Hadhrat Mirza ni nabii mkweli lakini mimi ni nani mbele ya kauli ya Allah atakapokujibu pale utakapomuomba kujua uhakika kuhusu Hadhrat Ahmad (as)??, ndugu yangu ninakusihi fanya Swala ya Tahajjud hata kwa siku kadhaa umuombe Allah kwa unyenyekevu bila ya kuwa na hisia ya kejeli dhidi ya Hadhrat Ahmad (as), naapa Wallahi Allah atakuonyesha ukweli.

Unaposwali sala ya Tahajjudi achana kabisa na maneno ya uongo ya kashfa yaliyotungwa na wapinzani wa Hadhrat Ahmad (as), wewe jikite wewe mwenyewe mbele ya Allah kuomba ili akuonyeshe ukweli katika njia anayoijua yeye mwenyewe.

Ni matumaini yangu kwamba utashika njia hii ya maombi ili kujua ukweli.

Na Allah akubariki, Alhamdulillah.
Mkuu ni hivi kila nambii na mtume alikuja na maajabu yake je ? Kwa nyie ahmadiya mirtha gulam alikuja na maajabu gani?
 
Mwanzo 1 3
Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

Mwanzo 1 4
Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.

Mwanzo 1 5
Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.
 
Mwanzo 1 13
Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.

Mwanzo 1 14
Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;

Mwanzo 1 15
tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.

Mwanzo 1 16
Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.

Mwanzo 1 17
Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi
 
Kama mungu hana mwanzo Wala mwisho basi mungu hawez ishi ndani ya muda coz muda Ni kipimo Cha chanzo na ukomo
 
Ufafanuzi:-

Neno "siku" lililotumika katika uumbaji wa Mungu kwa ajili ya dunia na mbingu lina maana ya wakati/kipindi na hivyo inakuwa Mungu aliumba ulimwengu katika nyakati 6 (6 periods) na sio maana yake kwamba Mungu aliumba ulimwengu kwa siku zetu hizi za saa 24 (days) za kupambazuka na kuchwea kwa jua.

Kwasababu "siku" kwa Mungu ni miaka yetu 1000, soma (22:47) Qur'an na pengine ni miaka yetu 50,000, soma (70:4), Qur'an.
Kwhyo ile dhan ya ikawa ikawa jion, ikawa asubuhi ni geresha sio? Au ilikuwa inachukua miak 500 mchana na miaka500 usiku?
 
Kwhyo ile dhan ya ikawa ikawa jion, ikawa asubuhi ni geresha sio? Au ilikuwa inachukua miak 500 mchana na miaka500 usiku?

Nakupa kazi, hebu iandike hiyo sehmu ya kitabu cha mwanza (anza na aya sura ya kwanza) hadi aya kadhaa ili tupate picha ya hicho unachosema, ujue hapa tunazungumzia juu ya kumbwa kwa ulimwengu kabla ya vitu vingine havijawekwa kama Nuru nk,
 
Mungu aliumba kwa siku, yaani,24hrs,ndio maana biblia unasema, ikawa mchana,ikawa asubuhi.
 
Kama siku moja ya malaika kwenda kwa mwenyezi mungu ni sawa na miaka 50,000 ya kwetu hapa duniani ,
Kwa ninavyofahamu mimi ni hivi.

Malaika wanapotumia siku moja kwenda mbinguni,basi lau na sisi tuseme tuende huko mbingumi basi tutatumia miaka hiyo 50,000 na sio siku moja kama malaika,kwa sababu malaika ana uwezo mkubwa aliopewa na Allah wa kusafiri umbali mrefu mnoo.

Sasa kwa kuwa sisi hatujapewa huo uwezo basi maana yake tutatumia miaka hiyo 50,000 kwenda mbinguni kwa sababu uwezo wetu dhaifu,lakini umbali huu ambao sisi tungesafiri kwa miaka hiyo 50000 basi malaika mwemye uwezo wake wa kipekee hutumia siku moja tu.

Ni sawa na mimi natumia IST kwenda mwanza kutoka dar natumia siku mbili,mwingine anatumia ndege kutoka pale pale dar kwenda mwanza anatumia saa moja.

Hii maana yake ni kuwa
Saa moja ya NDEGE from dar to mwanza = masaa 24 ya IST kutoka dar to mwanza.

Kinachotofautisha IST na NDEGE katika ufikaji wa baina ya point zile zile ni uwezo tu baaasi.
 
Mkuu kwanza niseme jibu lako halijaniridhisha na sijaleta swali kinyume labda twende taratibu kisha tutarudi kwenys swali langu la awali.
Nikunukuu kwanza

"Kadhalika katika sura ya 70 bado inaelezea mlinganyo wa tukio la malaika kwenda kwa na ukisoma fasiri za Qur'aan zimeelezea maana ya hii aya kama ilivyokuja, kwa kuonyesha siku moja wanayotumia Malaika kwenda juu kwa Allah, ni sawa miaka wlfu 50 yetu sisi" mwisho wa kunukuu.

Kwa niivyoelewa nukuu hiyo hapo juu ni kwamba

1.Malaika wanatumia siku mojs kwenda kwa mwenyezi mungu (S.W) .

2.Siku moja wanayotumia wao kwenda kwa mwenyezi mungu ni sawa na miaka 50,000 kwetu sisi.

Sasa labda nikufafanulie kwa nilivyoelewa mimi na mfano wangu utaegemea zaidi aya inayosema miaka 1000 badala ya 50,000.

Ni kwamba kama malaika ataondoka duniani mwaka 1020(A.D) ina maana atafika kwa mwenyezi mungu mwaka huu wa 2020(A.D) kwake yeye ataona ametumia siku moja pekee na wakatu sisi imepita miaka 1000 tangia ameondoka duniani .
(Nipo tayari kurekebishwa kama nitakuwa nimeelewa vibaya).

Na pia ningeomba uelezee nukuu yako .
Hiyo aya ina maanisha hivi: Mwendokasi wa Malaika wa siku 1 kwenda mbinguni kasi yake ukiibadili kwa sisi binadamu itatugharimu hiyo miaka elfu kufika mbinguni.

Ni sawa sawa na kusema kutoka Ubungo-Posta wao wanatumia lisaa limoja (1). Ila sisi tunatumia masaa (10). Kwa hiyo wao wakienda mara 10 watatumia masaa 10. Ila sisi tukienda mara 10 tutatumia masaa 100.
 
Sawa kabisa kumbe imeongelea umbali ,sasa ndugu yangu hakunielewa hata nilivyojaribu kumuuliza kama ni umbali ndiyo umeongelewa .
 
Kwa ninavyofahamu mimi ni hivi.

Malaika wanapotumia siku moja kwenda mbinguni,basi lau na sisi tuseme tuende huko mbingumi basi tutatumia miaka hiyo 50,000 na sio siku moja kama malaika,kwa sababu malaika ana uwezo mkubwa aliopewa na Allah wa kusafiri umbali mrefu mnoo.

Sasa kwa kuwa sisi hatujapewa huo uwezo basi maana yake tutatumia miaka hiyo 50,000 kwenda mbinguni kwa sababu uwezo wetu dhaifu,lakini umbali huu ambao sisi tungesafiri kwa miaka hiyo 50000 basi malaika mwemye uwezo wake wa kipekee hutumia siku moja tu.

Ni sawa na mimi natumia IST kwenda mwanza kutoka dar natumia siku mbili,mwingine anatumia ndege kutoka pale pale dar kwenda mwanza anatumia saa moja.

Hii maana yake ni kuwa
Saa moja ya NDEGE from dar to mwanza = masaa 24 ya IST kutoka dar to mwanza.

Kinachotofautisha IST na NDEGE katika ufikaji wa baina ya point zile zile ni uwezo tu baaasi.
Mmeelezea vizuri kinachomata ni spidi na umbali na ndo nilichokuwa najaribu kumuelewesha mkuu jurjani.
 
Ujawahi kusikia watu wamesoma vitabu vya dini halafu wakajitoa mhanga kuua wenzao?
Hiyo hofu wewe umeijuaje,umeitoa wap, kama sio kwenye vtabu ambavyo ww unasema vimeandikwa na binadam? Maana walisoma wakajua makatazo ya Mungu na ghadhabu zake ndio wakaja kukuambia wewe nawe ukaelewa ukapata hofu
 
Mwanzo 1 13
Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.

Mwanzo 1 14
Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;

Mwanzo 1 15
tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.

Mwanzo 1 16
Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.

Mwanzo 1 17
Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi
Hizo siku zilihesabiwa katika hali gani mkuu kidunia au kimbinguni?
 
Back
Top Bottom