Je, Mungu aliumba dunia kwa miaka Elfu 6?

Swali langu lipo hapa, huu ufafanuzi wa nyakati umeutoa wapi ? Maana ingekuwa hivyo Allah au mtume wa Allah angetumia tamko hilo baada yake ametumia mlinganyo sahali na uko wazi zaidi. Sababu tamko nyakati hutumika kama vile tutumiapo tamko majira.

Kadhalika inabaki kuwa siku moja kwake Allah ni sawa na miaka elfu au aya iliposema miaka 50,000 hii miaka ilienda sambamba na tukio la malaika.

Allah anasema katika sura hiyo ya 22 (Hajj) aya ya 47 :

48. Na wanakuhimiza ulete adhabu, lakini Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na ahadi yake kabisa. Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi. (al Hajj :47)

Kwa minajili hiyo,swali langu la tamko "Nyakati" hatulioni katika aya zaidi tunaona ule mlinganyo wa siku moja ya Allah ni kama miaka elfu, tunayohesabu sisi.

Kadhalika katika sura ya 70 bado inaelezea mlinganyo wa tukio la malaika kwenda kwa na ukisoma fasiri za Qur'aan zimeelezea maana ya hii aya kama ilivyokuja, kwa kuonyesha siku moja wanayotumia Malaika kwenda juu kwa Allah, ni sawa miaka wlfu 50 yetu sisi.
Ninauliza swali hili nikitaka ufumbuzi zaidi na ufahamu zaidi na sipo kupinga au kukosoa .

Swali.
Kama siku moja ya malaika kwenda kwa mwenyezi mungu ni sawa na miaka 50,000 ya kwetu hapa duniani ,na tangia mtume muhammad (S.A.W) apokee wahay ni miaka 1400+ iliyopita , na malaika aliyekuwa anamshushia wahyi ni huyo huyo jibril (A.S) , je? Hauoni kwamba ilitakiwa jibril (A.S) awe ameshusha aya moja pekee kama miaka 50,000 hapa duniani bado haijafika ili kukamilisha ile siku moja ni sawa na miaka 50,000 kwa mwenyezi mungu.

Kwa maana kushusha aya moja pekee itachukua miaka 50,000 ya hapa duniani kwend ka mwenyezi mungu ( S.W) itachukua pia miaka 50,000 na kurudi na aya tena ni miaka 50,000.

Kwa maana hiyo mpaka hivi sasa ilitakiwa jibril (A.S) awe njiani akielekea kuchukua aya ya pili.

Au aya hiyo hapo haihusiani na kushuka kwa wahyi?
 
Unaposema imepotoshwa. Nitakuuliza swali umejuaje na wewe marejeo yako ni yapi juu ya jambo hilo ? Lakini, je imepotoshwa kimaana au matini ?
Unakubaliana na mdau hapo kua dhana ya kuran haijaacha kitu ni uwongo uliowekwa na watu tu?
 
Wewe mbona umeshindwa kuthibitisha uwepo wako wa kesho kwa ithibati ya leo. Yaani usilete kauli za kitoto ya kuwa kesho utakuwepo pasi na kututhibitishia kuwepo kwako kesho.
Kesho ipi unayoizungumzia hapa, ni leo ambayo ambayo jana ilikua kesho?
 
Kwanza ungenieleza leo usiku utapitiwa na usigizi saa ngapi?

Na kuamka kesho saa ngp??

Halafu uje tubet..
Nimelala saa 23:30 nimeamka saa 06:30

Kesho gani hapo unaizungumzia?
 
Nimelala saa 23:30 nimeamka saa 06:30

Kesho gani hapo unaizungumzia?
Utakumbuka muda uliopofumba macho kulala,,lakini hutokumbuka ni muda gani usingizi ulikupitia,,

MUNGU hutufisha na kutufufuwa kila siku..

Hakuna mwenye ujanja wa kujuwa usingizi ulimpitia muda gani,,,,na utaamka saa ngapi,,
.usijidanganye mkuu.

Zote hizo ni sifa yake Muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.
 
Naona tutazunguka hapa bila muafaka.

Wewe ni mjuzi wa kiswahili na bila shaka utakuwa umenielewa niliposema "nyakati" sambamba na "siku"---- siku ya Mungu ni tofauti na siku zetu za 24 hours, sasa vyovyote utakavyoziita lakini kuna utofauti ndiyo maana nikatumia nyakati (periods/vipindi) kwa ajili ya siku ya Mungu, lengo ni kuonyesha utofauti tu kati ya siku zetu za kupambazuka na kuchwa kwa jua na siku za Mungu.

kosa lako ni hapo unapolazimisha tamko Nyakati litumike kuwasikisha siku, wakati siku ni siku imeshabainishwa tayari. Ni sawa useme juma moja kina vipindi saba, kisha ukasema hivyo vipindi ni siku saba. Tutakuuliza hiki ni Kiswahili cha wapi ?

Unachotakiwa kufanya hasa unapo zungumzia aya na hadithi tumia maneno yale yale yaliyotumika sababu yapo. Huko kwingine lazima ukosee kama ulivyokosea hapa. Nyakati huwa ni sehemu ya muda fulani na hasa hutumika katika mwaka, yaani huwa tunasikia ikisemwa "Nyakati za joto au nyakati za usiku" na mfano wake.
 
Ninauliza swali hili nikitaka ufumbuzi zaidi na ufahamu zaidi na sipo kupinga au kukosoa .

Swali.
Kama siku moja ya malaika kwenda kwa mwenyezi mungu ni sawa na miaka 50,000 ya kwetu hapa duniani ,na tangia mtume muhammad (S.A.W) apokee wahay ni miaka 1400+ iliyopita , na malaika aliyekuwa anamshushia wahyi ni huyo huyo jibril (A.S) , je? Hauoni kwamba ilitakiwa jibril (A.S) awe ameshusha aya moja pekee kama miaka 50,000 hapa duniani bado haijafika ili kukamilisha ile siku moja ni sawa na miaka 50,000 kwa mwenyezi mungu.

Kwa maana kushusha aya moja pekee itachukua miaka 50,000 ya hapa duniani kwend ka mwenyezi mungu ( S.W) itachukua pia miaka 50,000 na kurudi na aya tena ni miaka 50,000.

Kwa maana hiyo mpaka hivi sasa ilitakiwa jibril (A.S) awe njiani akielekea kuchukua aya ya pili.

Au aya hiyo hapo haihusiani na kushuka kwa wahyi?
Hii ni hesabu rahisi sana. Kwa maana hiyo ni kuwa Jibril ameshaimaliza kazi yake zamani sana. Jiulize kama siju moja ya Allah ni miaka elfu kwetu sisi, maana yake yake kwao muda wetu ni sehemu ndogo sana, yaani hata kitendo cha kupepesa macho kwao ni muda mwingi kwa munasaba wa miaka elfu kwetu sisi.

Yaani ni sawa na tuseme Treni ya Umeme yenye mwendokasi wa 280km/h mathalani kufika Mwanza, ila ni zaidi ya muda huo kwa basi, je kwa mwendo huo wa Treni kwa kutoka hapo Station kufika kimara, bila shaka ni muda mchache sana kwa kutumia Treni.

Ulichokosea wewe ni kulileta swali kinyume na maandiko yalivyo.
 
Unakubaliana na mdau hapo kua dhana ya kuran haijaacha kitu ni uwongo uliowekwa na watu tu?

Sikubaliani nae sababu ya kuwa Qur'aan si kitabu cha Sayansi wala si kitabu cha siasa za kishetani, bali ni muongozo kwa watu na kwa wale wanao mcha Allah.

Tunaposema hakijaacha kitu, kwa maana katika muongozo wa kuyaendea mambo yoyote yale. Ila hukuti katika Qur'aan habari za ujenzi au kilimo. Ila inakupa muongozo juu ya kuyaendea mambo kwa uzuri. Hii ndiyo maana ya kuwa haijaacha kitu. Qur'aan ukiisoma imetupe muongozo wa namna ya kuhakiki habari na mfano wake.
 
Kesho ipi unayoizungumzia hapa, ni leo ambayo ambayo jana ilikua kesho?
Ile ambayo ni hii leo. Tunaposema hakuna aijuaye kesho ni kuwa hakuna anaeweza kuleta ithibati ya hakika ya leo akiwa jana. Ndiyo maana husemwa watu wanatabiri ila hawana ithibati. Ukiona imetokea ujue hujathubitisha bali umebahatisha.
 
kosa lako ni hapo unapolazimisha tamko Nyakati litumike kuwasikisha siku, wakati siku ni siku imeshabainishwa tayari. Ni sawa useme juma moja kina vipindi saba, kisha ukasema hivyo vipindi ni siku saba. Tutakuuliza hiki ni Kiswahili cha wapi ?

Unachotakiwa kufanya hasa unapo zungumzia aya na hadithi tumia maneno yale yale yaliyotumika sababu yapo. Huko kwingine lazima ukosee kama ulivyokosea hapa. Nyakati huwa ni sehemu ya muda fulani na hasa hutumika katika mwaka, yaani huwa tunasikia ikisemwa "Nyakati za joto au nyakati za usiku" na mfano wake.

Wewe sijui ni mtu wa wapi??!!.

Kuna siku za aina mbili, siku ya saa 24 na siku ambayo ni sawa na miaka 1000 au 50,000, ili kutofautisha kati ya siku za saa 24 tulizozoea na siku za miaka 1000 na 50,000, hizo nikaziita nyakati au vipindi (periods), mfano unaposema nyakati za joto hiyo ni sawa na kusema vipindi vya joto au mtu anaposema vipindi vya masomo na kila kipindi kina dk 30.

Ninachotaka kusema ni hiki ili kuonyesha utofauti wa siku ya saa 24 na siku ya miaka 1000 au 50,000, ni lazima siku hizo ziainishwe kuonyesha utofauti ndiyo maana nikatumia neno nyakati na hata ningeweza kutumia neno vipindi.

Itakuwa ni ujinga neno siku liwe na maana ya saa 24 hapo hapo neno hilo hilo liwe ni sawa na miaka 1000 au 50,000 bila ufafanuzi, hivyo nilichofanya mimi ni ufafanuzi tu ili kurahisisha fikra za watu ambao wengi hudhani kwamba Mungu aliumba ulimwengu kwa siku sita za saa 24, na siku ya 7 akapumzika kitu ambacho baadhi ya waumini wa dini fulani nao siku ya 7 ya saa 24 huwa wanapumzika kana kwamba Mungu huwa anachoka kama wao.

Nyakati za joto, Nyakati sita za uumbaji wa ulimwengu, vipindi sita vya uumbaji wa ulimwengu, the six periods of creation of the universe.

Ni ufafanuzi tu kuondoa utata.
 
Wewe unajua kila kitu kilichopo hapa duniani na mbinguni na unajua jinsi vinavyoishi???.
Hizi habari za mbinguni unaweza kuzielezea in fact tuzijadili wote?
Electromagnetic waves around us, how do they exist around us???

Wewe unaweza kuona kila kitu au unaweza kusikia kila sauti??

Mungu yupo katika medium nyingine ambapo macho yetu hayawezi kumuona na umbo lake ni unique na anazo sifa exceptional ndiyo maana akakuumba mwanaume bila "hiyari yako" na sio mwanamke au sio panya.

Mimi nimekuuliza huyo mungu kabla ya kuumba hivi vitu alikua akiishi wapi sasa Hizo electromagnetic waves zimeingiaje kwenye swali hilo?

Mi sijauliza umbo la mungu

Mi nimeuliza wapi alikua akiishi mungu

Kama ambavyo saizi unaweza ukajibu kua yuko mbingu ya saba, nataka unijibu kabla hajaumba hiyo mbingu ya saba alikua anaishi wapi?
 
Utakumbuka muda uliopofumba macho kulala,,lakini hutokumbuka ni muda gani usingizi ulikupitia,,

MUNGU hutufisha na kutufufuwa kila siku..

Hakuna mwenye ujanja wa kujuwa usingizi ulimpitia muda gani,,,,na utaamka saa ngapi,,
.usijidanganye mkuu.

Zote hizo ni sifa yake Muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.
Mzee mbona unaniwekea mawazo yako kichwani mwangu?

Unajuaje hayo yote ilihali wewe sio mimi?
 
Sikubaliani nae sababu ya kuwa Qur'aan si kitabu cha Sayansi wala si kitabu cha siasa za kishetani, bali ni muongozo kwa watu na kwa wale wanao mcha Allah.

Tunaposema hakijaacha kitu, kwa maana katika muongozo wa kuyaendea mambo yoyote yale. Ila hukuti katika Qur'aan habari za ujenzi au kilimo. Ila inakupa muongozo juu ya kuyaendea mambo kwa uzuri. Hii ndiyo maana ya kuwa haijaacha kitu. Qur'aan ukiisoma imetupe muongozo wa namna ya kuhakiki habari na mfano wake.
Nafurahi sana kuona namna ambavyo mna chalenjiana wenyewe kwa wenyewe.

Sasa nataka unisaidie kuniambia ni wapi mungu alikua akiishi kabla ya hapo alipo saizi?
 
Hizi habari za mbinguni unaweza kuzielezea in fact tuzijadili wote?

Mimi nimekuuliza huyo mungu kabla ya kuumba hivi vitu alikua akiishi wapi sasa Hizo electromagnetic waves zimeingiaje kwenye swali hilo?

Mi sijauliza umbo la mungu

Mi nimeuliza wapi alikua akiishi mungu

Kama ambavyo saizi unaweza ukajibu kua yuko mbingu ya saba, nataka unijibu kabla hajaumba hiyo mbingu ya saba alikua anaishi wapi?

Nani kasema Mungu yupo mbingu ya 7 ???.

Put aside God, Counter question is this, je wewe unajua vitu vyote jinsi vinavyoishi???

Pia je wewe unajua namna "intelligent signals" zinavyo exist around us ??

Je wewe unaweza kuona kitu chochote kilichopo mbele yako in the day light???

Je wewe unaweza kusikia kila sauti ???.

Hayo ni maswali ya kujiuliza kwanza kabla ya kuanza kutafuta Maisha ya
Mungu, perception juu ya mazingira ya maisha yako tu yanakushinda iweje urukie kutaka kujua Maisha katika "realm" ya Mungu??!!

Kwanza leo umeshakula??
 
Wewe sijui ni mtu wa wapi??!!.

Kuna siku za aina mbili, siku ya saa 24 na siku ambayo ni sawa na miaka 1000 au 50,000, ili kutofautisha kati ya siku za saa 24 tulizozoea na siku za miaka 1000 na 50,000, hizo nikaziita nyakati au vipindi (periods), mfano unaposema nyakati za joto hiyo ni sawa na kusema vipindi vya joto au mtu anaposema vipindi vya masomo na kila kipindi kina dk 30.

Ninachotaka kusema ni hiki ili kuonyesha utofauti wa siku ya saa 24 na siku ya miaka 1000 au 50,000, ni lazima siku hizo ziainishwe kuonyesha utofauti ndiyo maana nikatumia neno nyakati na hata ningeweza kutumia neno vipindi.

Itakuwa ni ujinga neno siku liwe na maana ya saa 24 hapo hapo neno hilo hilo liwe ni sawa na miaka 1000 au 50,000 bila ufafanuzi, hivyo nilichofanya mimi ni ufafanuzi tu ili kurahisisha fikra za watu ambao wengi hudhani kwamba Mungu aliumba ulimwengu kwa siku sita za saa 24, na siku ya 7 akapumzika kitu ambacho baadhi ya waumini wa dini fulani nao siku ya 7 ya saa 24 huwa wanapumzika kana kwamba Mungu huwa anachoka kama wao.

Nyakati za joto, Nyakati sita za uumbaji wa ulimwengu, vipindi sita vya uumbaji wa ulimwengu, the six periods of creation of the universe.

Ni ufafanuzi tu kuondoa utata.
Hakuna nyakati sita za uumbaji, hili ni lako na tumekuachia wewe na ni uongo wa wazi.

Tangu dunia inaumbwa hakuna mtu aliyesema "Nyakati sita",Qur'aan fasafa mno, lingekuwa tamko hilo ni muafaka lingetumika. Kwahiyo unapolitumia lazima tu upotoshe maana. Lakini vilevile sisi Waswahili hstulitumii hivyo tamko hilo.

Hakuna ujinga hapo wa tamko siku ya masaa 24 na siku ya miaks 1000 huo ni mlinganyo tu, ndiyo maana kitabu kitukufu kimelitumia tamko hilo. Sasa wewe mwnye uelewa mdogo na mpotoshaji maana yako hsina asili.

Ama tukiliangalia tamko vipindi nalo halikai hapi, sababu nyakati huwa ni chini ya siku au sehemu ya mwaka, ndiyo maana kwa ufasafa Allah akatumia hivyo hivyo siku.
 
Back
Top Bottom