Kiujumla swala la Uumbaji, yakiwemo na maswali Mengi ya dini, ni maswali ya kifalsafa.
Kwa uelewa wangu, Muda sio tu relative, bali binadamu tumeweka na kujiwekea hesabu ya Muda ili tuishi kimpangilio.
Ila kiuhalisia hakunaga mwanzo na mwisho, ila upo mwanzo wa Jambo na mwisho wa japo, mwanzo na mwisho wa tukio, nk.
Mwanzo wa Maisha na mwisho wa Maisha, ya kiumbe au tukio.
Kuna dhana ya Mungu Hana mwanzo Wala mwisho. Mimi ni Muumini wa hiyo dhana.
Kama ana mwanzo na mwisho hiyo hawezi kuwa Mungu. Labda mmoja wa miungu" demigod/ or Idols"
Ila Mungu aliye mmoja hapaswi kuwa na mwanzo wala kuwa na mwisho wa existence yake.
Vinginevyo ni Bora kusema hakuna Mungu.
Biblia ilivyoandikwa imeandikwa na mwanadamu. Kuanzia ikiwa ni kitabu kimoja kimoja, kabla havija kusanywa na kuwa kitabu kimoja.
Enzi za Musa akiwa na vitabu vya Sheria/torati. Huo ndio ulikua mwanzo wa biblia.
Simulizi za Uumbaji zilianza kwenye vitabu vya Musa, kwenye kitabu cha Mwanzo. Fikiria kwa teknolojia, Maendeleo,Elimu, na Uelewa wa watu wa kipindi Cha Musa, Miaka mingi kabla ya Yesu, maana yake Zaidi ya Miaka elfu mbili iliyopita. Kungekuwa na namna gani Bora ya kuwaelezea watu wa kipindi hicho juu ya Uumbaji zaidi ya jinsi Musa alivyowaelezea kwenye kitabu cha Mwanzo.
Bila shaka namba rahisi kwa uelewa wa watu wa kipindi kile, ilikua lazima Musa avunje Zama za Uumbaji kwa kusema siku ili aweze kueleweka.
Ila siamini Kama kweli Uumbaji ulifanyika ndani ya siku sita, yaani masaa 24×6. Kama tunavyoelewa Sasa. Au Kama ambavyo yamekuwepo siku zote.
Nakubaliana na aliyesema hizo siku sita zilikua nyakati ambazo pengine ni Miaka Bilioni Moja, kwa kila wakati.
Sasa fikiria kwa kipindi Cha Musa hata neno Bilioni lilikuwepo?
Maana hata ukiangalia msamiati ulioo yesha namba kubwa iliotumika kwenye biblia ni elfu.
Sana sana wakitakuonyesha ni zaidi ya elfu litatumika neno maelfu kwa maelfu. Na lilitumika kwenye kuonyesha idadi ya vitu au watu.
Sasa achana na Hesabu hiyo rahisi.
Embu, fikiria Musa angepewa ufunuo wa Uumbaji kwa namna ambayo Leo hii sayansi inauelewa. Yaani Ile process yoote ya Evolution Kama sayansi inavyozidi kugundua Leo hii, ndio Musa angelielewa Hilo kipindi hicho.
Angemuelezea Nani ambaye angemuelewa. Na ingefaa nini kwenye kuwafanya watu aliokua akiwaongoza( waizraeli) waweze kumcha Mungu?
Hivyo naamini Maelezo ya Uumbaji Kama yalivyo kwenye kitabu cha Mwanzo Ni Simple Version ya Uumbaji, ambayo lengo lake lilikua ni watu wa kipindi hicho waweze kuelewa Mungu yupo na ndio chanzo Cha vyote vilivyoumbwa, hivyo wanapaswa kumcha yeye.