Leta maandiko mkuu kila mtu asome na kuchangia mada hii ndo maana ya JF
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app
Mwanzo 1
1
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2
Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
### Kinachosemwa hapa kwenye haya mafungu mawili; Mungu hakukifanya ndani ya hizi siku sita(6) za uumbaji zinazoongelewa hapa; bali alikuwa ameshakifanya miaka mingi nyuma na ambayo haijasemwa ni lini
###Kilichofanyika kwenye siku sita (6) zinazoongelewa hapa, ni kile kinachosemwa kuanzia fungu la tatu (3) na kuendelea. Kwa hiyo basi; kwenye siku sita (6) zinazoongelewa hapa, Mungu hakuumba Mbingu na Nchi bali alikuwa tayari ameshaziumba kabla; miaka mingi nyuma ambayo hautelezwi kuwa ni lini
###Mbali na haya; kama unayachugnuza maandiko vizuri, unaweza kugundua kuwa Adam na Hawa si binadamu wa kwanza kuwahi kuwepo duniani, bali Mungu aliwahi kuumba watu huko nyuma kabla ya maisha ya Adamu na Eva isispokuwa kwenye siku hizi sita (6) binadamu wa kwanza kuumba walikuwa ni Adam na Hawa
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. 5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku.
Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. 7Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. 8Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. 10Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. 12Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 13Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.
14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili ya kuonesha majira, siku na miaka; 15tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. 16Mungu akaumba mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi 18na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 19Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.
20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na viumbe vyenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. 21Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 22Mungu akavibariki, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. 23Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. 25Mungu akaumba aina zote za wanyama wa porini na wa kufugwa na viumbe vyote vitambaavyo juu ya nchi; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 2