Bahati mbaya katika historia ya Taifa hili itabaki kuwa hivyo katika historia kwa vizazi vijavyo kuwa katika muhula wa pili wa utawala wa awamu yatano serikali iliongozwa bila ya muhimili wa tatu ambao ni Bunge.
Itasomeka hivyo kuwa kulikuwa hakuna Bunge kabisaaa bali lilikuwepo baraza liliundwa ili kuwakilisha kikundi cha watu walio shika dola na kutawala kwa mabavu kwa kutumia nguvu na sio kwa ridhaa ya wananchi.
Itasomeka kuwa baraza hilo liliundwa kuwakilisha kikundi hicho cha washika dola ili kutunga na kuidhinisha sheria sheria za kidhalimu na ukandamizaji kwa maslahi badala ya kuwakilisha wananchi kwa maslahi ya ustawi wa Taifa.
Historia hiyo ita thibitishwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo nakala za magazeti picha mnato na video zikiknyesha viongozi waandamizi wa kikundi hicho wakiuambia umma jinsi gani watakavyoitumia dola kubaki madarakani.
Huku wengine wakiwathibishia wananchi kuwa hata wasipochagua CCM itashinda tu, na kubwa zaidi ni uvunjwaji na usiginaji wa katiba jambo ambalo pia litatumika kama kumbukumbu rejea katika mitaala ya elimu ya juu, si hapa Tanzania bali pia nchi jirani zinazofanana na sisi kimfumo.
Uthibitisho wa uvunjwaji wa katiba huo of corse ukiachilia mbali mambo kadhaa ya nyuma lakini kubwa ni kuwaingiza bungeni kina Dada 19 watakao endelea kujulukana kama COVID 19 ambao hawakuwa na sifa zakua wabunge kwa sababu hawakuwa na chama wanachokiwakilisha.
DOA JEUSI KATIKATI YA SHUKA JEUPE KWENYE UTAWALA WA JIWE ITABAKI KUWA HIVYO DAIMA DUMU