Je, Mtanzania, una imani Bunge linaloendelea Dodoma?

Je, Mtanzania, una imani Bunge linaloendelea Dodoma?

Sina haja na hilo Bunge hata kidogo. Bunge lenyewe linaongozwa na wagonjwa wa akili!!!
 
Inasemekana kwamba hata ambaye amenyimwa macho basi angalau anapewa uwezo wa kunusa na kupapasa, hanyimwi vyote.

Ukweli niliouona (maana macho ninayo) ni kwamba wananchi wengi wamelipuuza na kulidharau kabisa bunge jipya linaloendelea Mjini Dodoma, wadau hawana habari nalo wala hawataki hata kufuatilia yanayojiri, taarifa zinaonyesha kwamba namna wabunge hao walivyopatikana na namna uchaguzi wa 2020 ulivyoendeshwa ndio sababu kubwa ya wananchi kulipuuza bunge hili.

Hawaoni kama wabunge walioingizwa bungeni kwa mbeleko ya chuma huku wengine wakiingizwa ndani ya bunge bila kuwakilisha chama chochote cha siasa kama Katiba ya nchi inavyotaka, kuna mashaka mazito kama wabunge hawa wa kutengeneza maabara wanaweza kuhoji masuala ya msingi , kwa ujumla wananchi wameamua kujitenga na bunge hili japo juhudi za kulitangaza zimekuwa kubwa mno !

Nakulilia Tanzania .
Bila shaka umetumia neno "wananchi" ukimaanisha wana Chadema maana unaona ni aibu siku hizi kujiita MWANACHADEMA!
 
Hakuna bunge pale ni kikundi furani chenye mamlaka ambacho kipo kazi maalumu
 
Hujui kitu
Kweli sijui ila nami nilichangia kumtoa jirani yangu na aliyekuwa Mwenyekiti wangu wa Mtaa hapa Mwanza Jiji Ndugu Mwakiaba, hasa pale nilipomwona mke wake akitembea huku akilia katika mitaa ya Kata ya Mkolani akiomba achangiwe ili mmewe na jirani yangu asifungwe!
 
Hicho ni kikao cha Kamati Kuu ya Ma CCM Nitafatilia ikiwa kuna Tangazo la TANZIA
Naunga mkono hoja, hilo siyo bunge halali, mkuu wao anasema walimu wafundishe masomo matano
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hao ni wajumbe walioteuliwa na Magufuli, lakini haijulikani ni kwaajili ya kufanya kazi gani.

Hawatuhusu. Wanachoongea hakituhusu. Nimesoma hapa JF kuwa baadhi wameanza kujadili namna ya kumwongezea muda wa Urais aliyewateua.

Japo sijui kama ni lazima wajumbe hao wajadili hilo la kumwongezea muda wake wa Urais. Akitaka, si anatangaza tu kuwa yeye ni Rais wa maisha na ikawa? Mbona aliagiza wakurugenzi wasiwatangaze wapinzani kuwa wabunge hata kama wamechaguliwa na wananchi, na ikawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati mbaya katika historia ya Taifa hili itabaki kuwa hivyo katika historia kwa vizazi vijavyo kuwa katika muhula wa pili wa utawala wa awamu yatano serikali iliongozwa bila ya muhimili wa tatu ambao ni Bunge.

Itasomeka hivyo kuwa kulikuwa hakuna Bunge kabisaaa bali lilikuwepo baraza liliundwa ili kuwakilisha kikundi cha watu walio shika dola na kutawala kwa mabavu kwa kutumia nguvu na sio kwa ridhaa ya wananchi.

Itasomeka kuwa baraza hilo liliundwa kuwakilisha kikundi hicho cha washika dola ili kutunga na kuidhinisha sheria sheria za kidhalimu na ukandamizaji kwa maslahi badala ya kuwakilisha wananchi kwa maslahi ya ustawi wa Taifa.

Historia hiyo ita thibitishwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo nakala za magazeti picha mnato na video zikiknyesha viongozi waandamizi wa kikundi hicho wakiuambia umma jinsi gani watakavyoitumia dola kubaki madarakani.

Huku wengine wakiwathibishia wananchi kuwa hata wasipochagua CCM itashinda tu, na kubwa zaidi ni uvunjwaji na usiginaji wa katiba jambo ambalo pia litatumika kama kumbukumbu rejea katika mitaala ya elimu ya juu, si hapa Tanzania bali pia nchi jirani zinazofanana na sisi kimfumo.

Uthibitisho wa uvunjwaji wa katiba huo of corse ukiachilia mbali mambo kadhaa ya nyuma lakini kubwa ni kuwaingiza bungeni kina Dada 19 watakao endelea kujulukana kama COVID 19 ambao hawakuwa na sifa zakua wabunge kwa sababu hawakuwa na chama wanachokiwakilisha.

DOA JEUSI KATIKATI YA SHUKA JEUPE KWENYE UTAWALA WA JIWE ITABAKI KUWA HIVYO DAIMA DUMU
Awamu ya tatu itatajwa kama kipindi cha giza katika historia ya nchi yetu. Ni sawa na Wajerumani na mataifa ya Ulaya yanavyoukumbuka utawala wa Hitler. Mengi machafu yaliyofichika, yatakuja kuwekwa wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom