Kuna Umuhimu Kamati Za Bunge Kuendeshwa Live, Mfumo Uliopo Unaruhusu Ushawishi Mbaya!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Nimeshangaa utitiri wa matangazo ya iftal huko bungeni Dodoma kwa sasa!

Na ndio maana nikaanza kufikiria na kutafakari kinachoendelea hukohuko Bungeni kwa sasa!
Kuhusiana na ripoti ya CAG. Inayohusu ufisadi wa ma-trilioni ya shilingi za walipa kodi wa nchi hii.

Kwa sababu,huko kwenye kamati za kibunge!
ndiko hasa ambako wahusika wanaitwa na kujieleza rasmi. Hatua kwa hatua bila chenga!
Kitendo cha kuwa faragha,kinatoa nafasi kubwa ya michezo michafu kutendeka,ikiwemo wajumbe wa kamati husika kupewa milungula na watuhumiwa,kisha kuweza kushawishika na hatimae kupelekea kuupindisha ukweli halisi kwa manufaa yao binafsi.Na hivyo kuvuruga muenendo wa kupatikana ukweli kwa wahusika kuweza kuadhibiwa kutokana na maovu yao.

Hainiingii akilini,Kamati zenye kuchunguza mambo yanayohusu ubadhirifu wa ma-trilioni ya shilingi za walipa kodi.

Halafu wanakabidhiwa wajumbe wachache wa kamati,tena ambao nao pia,baadhi yao kwa asilimia kubwa.
Uadilifu wao ni wa kutiliwa mashaka,tukizingatia hata ile namna walivyopatikana kimashaka madlshaka kupitia wajumbe wenye njaa kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita 2020 ndani ya CCM yenyewe.

Tena woote wakiwa ni walewale wa chama tawala,ambacho pia ni chama tuhumiwa?

Wakiwa wamefunikwa na ushungi au kilemba cha wenyeviti wa kamati hizo,ambao ni wabunge wa upinzani wasiotambulika rasmi na upinzani wenyewe?

Kwamba wajumbe wa kamati hizo,ni wale wabunge ambao wengi wao hawaijui hatma yao pale itakapofika 2025!

Halafu unawakabidhi jambo zito kama hili la ufisadi wa kutisha,tena wakiwa faragha na watuhumiwa?

Wakati hawana uhakika kwa hata 30% kwamba watarudi bungeni tena!
Hii ni kama wanapewa fursa rasmi ya kujitafutia utajiri na pensheni za maisha mapya huko uraiani.

Ndio maana tunaona matangazo ya iftal yamekuwa mengi bungeni kule Dodoma!
Ikiwa ni kiashiria cha Iftal kutumika ili kupata ukaribu na baadhi ya wajumbe,ili kuanza ushawishi kuelekea mchakato wa uchambuzi wa ripoti ya CAG.

Hivi tujiulize,Kwani ikiwa live mahojiano ya kamati,kutakuwa na madhara gani kwa serikali na kwa watanzania kwa ujumla?

Mbona wenzetu Kenya,haya mambo hufanyika live na kufanikiwa?
Je sisi tunakwama wapi?

Ndio tunajua kwamba
sio watumishi wote wa serikali wanahusika na ubadhirifu huo ,bali kuna wahuni wachache ndani ya serikali wanaichafua serikali nzima kwa tamaa zao na kwa manufaa yao binafsi..

Ambao wameunda ushirika wa kimfumo(Cartel) na kuendesha genge kuu la ufisadi ndani ya serikali yetu.kutokana na mfumo mbaya tulioukumbatia,wa uendeshaji wa serikali yetu(State Capture).

Sasa hawa tungependa bunge kutoa nafasi ili washughurikiwe kwa uwazi na ukweli.
Ili pasiwepo na biashara ya kulindana,ikumbukwe tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu 2025,ni vyema kufika huko,na Serikali na chama vikiwa visafi!
Kama kweli CCM ina nia njema na wananchi wa taifa letu.

Na kama hoja za serikali zitakuwa dhaifu kama CAG alivyoripoti ni vyema ikaundwa kamati teule ya bunge yenye wazalendo na wanamuogopa "Mwenyezi Mungu" wachunguze tuhuma hizo,ili kuleta tumaini kwa watanzania na walipa kodi na Tozo wa nchi yetu.

Ni maoni yangu binafsi ila tusahihishane pale tunapopeana mawazo mbadala kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Nawatakia Asubuhi Njema!
 
Kamati ziwe live? Bunge lenyewe halitakiwi kuwa live, sababu wananchi wanatakiwa kuchapa kazi sio kutazama Bunge
Au umeshaanza kusaliti mawazo ya JPM, mwana Sukuma Gang mwenzangu?
 
Mimi sio mwana Sukuma Gang maana ni kitu hewa,ni jina hewa lililotengenezwa na Mafisadi ili kumpumbaza malkia na hatimae wanapiga pesa!
 
Inawezekanaje hii kutokuwa rushwa!!???
Leo kuna Iftar imeandaliwa na PM hapa Dom, na kesho bajeti ya PM inapitishwa!!!
 
Wakati dhalimu anazuia bunge live na kusema watu wafanye kazi na sio kuangalia bunge,mliona ni bonge la kiongozi. Kisha akaamua kunajisi uchaguzi ili ajaze wezi wenzake wa CCM, mlikuwa mnasema anakubalika. Sasa hivi bunge la majizi ya kura tumelipuuza kisha ndio unataka lionyeshwe live.

Ukitaka kufuatilia hilo bunge la majizi ya kura nenda huko huko bungeni, au ombeni chanel 10 ionyeshe ili nyie Makada wa CCM muwe mnfuatilia hivyo vikao vya CCM ndani ya bunge.
 
Wana shida sana sana, hakuna kitu cha maana watafanya
 
Halafu yule Mbunge mwenye kibaraghashia hajui kuwa anal stimulation inaleta orgasm haraka anataka ati Wabunge wapimwe tigo zao kama ziko intact.

Nimeshangazwa sana na Bunge hili lililojaa Mambumbumbu wengi.
 
Kuna mbunge akasema kuwa wachekiwe marinda Kama jeshini ,duu ama kweli shibe inalewesha na kutoa akili
 
Wakati dhalimu anazuia bunge live na kusema watu wafanye kazi na sio kuangalia bunge,mliona ni bonge la kiongozi. Kisha akaamua kunajisi uchaguzi ili ajaze wezi wenzake wa CCM, mlikuwa mnasema anakubalika. Sasa hivi bunge la majizi ya kura tumelipuuza kisha ndio unataka lionyeshwe live.

Ukitaka kufuatilia hilo bunge la majizi ya kura nenda huko huko bungeni, au ombeni chanel 10 ionyeshe ili nyie Makada wa CCM muwe mnfuatilia hivyo vikao vya CCM ndani ya bunge.
Wakati ule kulikuwa na wahuni wenu cha**dema huko bungeni,kulikuwa hakuna tija zaidi ya matusi ya kihuni bungeni.
Halafu wewe endelea kugombana na kaburi wakati sisi tunaangalia mbele yetu!

Hatukuwepo wakati ukitumbuliwa!
 
Mnaanza kutia akili sasa.
Wakati lile shetani lenu linanajisi uchaguzi na kufungia bunge live mlishangilia sana eti anakubalika.
Haya ndo matokeo ya kunajisi uchaguzi
 
Nimeshangaa utitiri wa matangazo ya iftal huko bungeni Dodoma kwa sasa!

Na ndio maana nikaanza kufikiria na kutafakari kinachoendelea hukohuko Bungeni kwa sasa!
Kuhusiana na ripoti ya CAG. Inayohusu ufisadi wa ma-trilioni ya shilingi za walipa kodi wa nchi hii.

Kwa sababu,huko kwenye kamati za kibunge!
ndiko hasa ambako wahusika wanaitwa na kujieleza rasmi. Hatua kwa hatua bila chenga!
Kitendo cha kuwa faragha,kinatoa nafasi kubwa ya michezo michafu kutendeka,ikiwemo wajumbe wa kamati husika kupewa milungula na watuhumiwa,kisha kuweza kushawishika na hatimae kupelekea kuupindisha ukweli halisi kwa manufaa yao binafsi.Na hivyo kuvuruga muenendo wa kupatikana ukweli kwa wahusika kuweza kuadhibiwa kutokana na maovu yao.

Hainiingii akilini,Kamati zenye kuchunguza mambo yanayohusu ubadhirifu wa ma-trilioni ya shilingi za walipa kodi.

Halafu wanakabidhiwa wajumbe wachache wa kamati,tena ambao nao pia,baadhi yao kwa asilimia kubwa.
Uadilifu wao ni wa kutiliwa mashaka,tukizingatia hata ile namna walivyopatikana kimashaka madlshaka kupitia wajumbe wenye njaa kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita 2020 ndani ya CCM yenyewe.

Tena woote wakiwa ni walewale wa chama tawala,ambacho pia ni chama tuhumiwa?

Wakiwa wamefunikwa na ushungi au kilemba cha wenyeviti wa kamati hizo,ambao ni wabunge wa upinzani wasiotambulika rasmi na upinzani wenyewe?

Kwamba wajumbe wa kamati hizo,ni wale wabunge ambao wengi wao hawaijui hatma yao pale itakapofika 2025!

Halafu unawakabidhi jambo zito kama hili la ufisadi wa kutisha,tena wakiwa faragha na watuhumiwa?

Wakati hawana uhakika kwa hata 30% kwamba watarudi bungeni tena!
Hii ni kama wanapewa fursa rasmi ya kujitafutia utajiri na pensheni za maisha mapya huko uraiani.

Ndio maana tunaona matangazo ya iftal yamekuwa mengi bungeni kule Dodoma!
Ikiwa ni kiashiria cha Iftal kutumika ili kupata ukaribu na baadhi ya wajumbe,ili kuanza ushawishi kuelekea mchakato wa uchambuzi wa ripoti ya CAG.

Hivi tujiulize,Kwani ikiwa live mahojiano ya kamati,kutakuwa na madhara gani kwa serikali na kwa watanzania kwa ujumla?

Mbona wenzetu Kenya,haya mambo hufanyika live na kufanikiwa?
Je sisi tunakwama wapi?

Ndio tunajua kwamba
sio watumishi wote wa serikali wanahusika na ubadhirifu huo ,bali kuna wahuni wachache ndani ya serikali wanaichafua serikali nzima kwa tamaa zao na kwa manufaa yao binafsi..

Ambao wameunda ushirika wa kimfumo(Cartel) na kuendesha genge kuu la ufisadi ndani ya serikali yetu.kutokana na mfumo mbaya tulioukumbatia,wa uendeshaji wa serikali yetu(State Capture).

Sasa hawa tungependa bunge kutoa nafasi ili washughurikiwe kwa uwazi na ukweli.
Ili pasiwepo na biashara ya kulindana,ikumbukwe tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu 2025,ni vyema kufika huko,na Serikali na chama vikiwa visafi!
Kama kweli CCM ina nia njema na wananchi wa taifa letu.

Na kama hoja za serikali zitakuwa dhaifu kama CAG alivyoripoti ni vyema ikaundwa kamati teule ya bunge yenye wazalendo na wanamuogopa "Mwenyezi Mungu" wachunguze tuhuma hizo,ili kuleta tumaini kwa watanzania na walipa kodi na Tozo wa nchi yetu.

Ni maoni yangu binafsi ila tusahihishane pale tunapopeana mawazo mbadala kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Nawatakia Asubuhi Njema!
Naunga mkono hoja kama mleta mada ulilaani Bunge kuwa gizani Tangu 2016.
 
Back
Top Bottom