Je, Msajili Hazina anaihujumu CCM?

Achukibesi

JF-Expert Member
Dec 3, 2012
234
77
Kama tunavyojua, mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu na katika mchakato huo, Watanzania wote huwa na haki sawa ya kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuchagua au kuomba kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali zinazogombewa.

Katika Uchaguzi wa mwaka huu, kumetokea kuvunjwa kwa rekodi ya kujitokeza kwa wagombea wengi katika mchakato wa awali wa kupata wagombea hasa katika Chama cha Mapinduzi baada ya makundi mbalimbali ya wanachama kujitokeza kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya Chama.

Miongoni mwa makundi hayo ni kundi la Watumishi wa Umma kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Serikali Kuu ambao wengi wao waliomba ridhaa kupitia kwa CCM. Aidha kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo mbalimbali, watumishi hao walitumia haki yao ya Kikatiba kuomba ridhaa hiyo.

Aidha, ninaamini kuwa karibu watumishi wote walizangatia maelekezo na muongozo uliopo katika Waraka wa Utumishi wa mwaka 2015 ulioelekeza ni jinsi gani Watumishi wa umma watakavyoshiriki katika uchaguzi ngazi ya chama.

Miongoni mwa maelekezo hayo ni pamoja na kwa mtumishi anayetaka kugombea, ni lazima aombe ruhusa ambayo ni lazima akubaliwe pamoja na kukubali kuwa, kipindi atakachokuwa katika mchakato wa kugombea, atahesabiwa kuwa alikuwa likizo bila ya malipo. Yote hayo hayakuwa na tatizo kwa watia nia hao.

Changamoto mpya iliyojitokeza ni kuwa, Msajili wa Hazina ametoa maelekezo yanayokinzana na maelekezo yaliyomo katika Waraka wa Utumishi wa 2015. Kwa mujibu wa maelekezo ya Msajili wa Hazina, amewataka Watumishi waliokwenda kutia nia ambao wengi wao walikukuwa ni kupitia CCM kufanya yafuatayo:

1. Kuomba Likizo bila ya Malipo kuanzia tarehe 01/07/2020 hadi tarehe 31/08/2020
2.Kutambua kuwa, kurudi kwao kutategemea kuwepo kwa nafasi wazi katika ofisi zao wanakotoka
3. Kuandika barua ya kuomba kurejea kazini ambayo itahitaji kujibiwa aidha kwa ukubaliwa au kukataliwa

Binafsi ninaamini kuwa, maelekezo namba 1 hapo juu, hayana tatizo kwa watia nia wote kwa sababu ni kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa 2015 pamoja na sheria na kanuni za Utumishi. Tatizo lililopo ni maelekezo yaliyopo katika vipengele vya 2 na 3 hapo juu ambavyo binafsi ninaona vinahitaji mjadala na mtazamo wa jicho chanya ili kuweza kubaini kilichopo kwenye nia ya Msaili wa Hazina alipotoa maelekezo hayo.

Mjadala huu unalenga kuangalia iwapo kuna nia ovu kutoka wa Msajili ya kuwakomoa watia nia hao au kuwachonganisha watumishi hao na chama chao au Serikali yao kwa sababu hadi wanaamua kwenda kutia nia, maelekezo hayo mapya, hayakujulikana kwao na hivyo kuonesha kuwa msajili wa Hazina ametunga Kanuni baada ya mchezo kuanza.

Kitendo hicho kinatoa taswira hasi kwa Msajili inayomuonesha kuwa aidha amevuka mipaka ya mamlaka yake (Waraka wa Katibu Kiongozi unafutwa au kurekebishwa na Katibu mwenyewe na si vinginevyo), hajui mipaka ya mamlaka yake, amedharau Mamlaka ya Katibu Kiongozi aliyetoa Waraka wa 2015 au ameamua kuwakomoa Watia Nia wote kutoka CCM kama ishara ya kuonesha chuki yake kwa Chama cha Mapinduzi na serikali yake.

Jambo hili linapaswa kukemewa na watu wote wenye mapenzi mema na nchi na serikali yetu.
 
Hebu fafanua ili tupate elimu pamoja na watia nia. Ni sheria ipi iliyofuatwa na Msajili au kuvunjwa na Watia nia?
 
Mkanganyiko wa Msajili umepelekea Naibu Katibu Mkuu Utumishi kutoa maelekezo ya kuwataka waajiri kuwaandikia barua watumishi hao kurejea kazini haraka iwezekanavyo. Huu ni ushahidi tosha kuwa kuna tatizo katika ofisi ya Msajili wa Hazina.

NB:

Mada hii haina mvuto kwa wapenda matusi aka Wachadomo kwa kuwa hawana utamaduni wa kuwatetea wanyonge.
 
Kwa kweli hata kampeni majimboni zimepoza. Hawa watia nia walikuwa mtaji muhimu kwa chama kama wangelipwa mishahara. Kwa sasa wameuchuna tu wanaangalia jinsi kampeni zinavyoenda
 
Kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama cha Msajili wa Hazina, it is obvious kwamba anajua anachokifanya na si kingine bali ni hujuma ya wazi kwa CCM na hii itawatisha wengi kwenye uchaguzi ujao iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa na mamlaka husika.

Kongole kwa Naibu Katibu Mkuu Utumishi kwa kutoa ufafanuzi unaokusudia kuondoa sintofahamu.
 
Kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama cha Msajili wa Hazina, it is obvious kwamba anajua anachokifanya na si kingine bali ni hujuma ya wazi kwa CCM na hii itawatisha wengi kwenye uchaguzi ujao iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa na mamlaka husika.

Kongole kwa Naibu Katibu Mkuu Utumishi kwa kutoa ufafanuzi unaokusudia kuondoa sintofahamu.

Katika kipindi cha hivi karibuni hali ya kuridhika na utoaji haki za kimsingi zilizoainishwa kwenye Sheria zetu imezorota mnooo hutaki kukubali no wewe.
 
Katika kipindi cha hivi karibuni hali ya kuridhika na utoaji haki za kimsingi zilizoainishwa kwenye Sheria zetu imezorota mnooo hutaki kukubali no wewe.
Sio kwamba sijaridhika, bali ukweli uko bayana kuwa huyu Msajili ana lake jambo na ndio maana Utumishi wametoa maelekezo stahiki. Otherwise nawe yaonekana una maslahi na maumivu wayapatayo Watumishi walio tia nia.
 
Viongozi wooote wa NEC pamoja na Jecha wooote ni wa kusukumia ndani
 
Back
Top Bottom